Friday, May 20, 2016

YANGA YAWASILI NCHINI,YAPOKELEWA KWA KISHINDO NA MASHABIKI WAKE.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
MABINGWA wa soka Ligi Kuu ya Bara wamewasili jijni wakitokea Angola katika mechi ya narudiano dhdi ya Espirance Sagdrada ya Angola.

Yanga ambayo imefuzu hatua makundi wamewasili mida ya saa nane na dakika 45 na mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa kocha wa timu hiyo Hans Van Pluijim amesema timu imefanya vizuri pamoja na figisu figisu ambazo wamefanyiwa.

Amesema anawapongeza viongozi wa Yanga kwa kupambana na hujuma lakini wamefanikiwa kuingia hatua ya makundi na wamejifunza mengi Angola ambapo watayafanyiwa kazi huku akiwapongeza wachezaji wake kwa juhudi walizoonyesha uwanjani kuhakikisha wanafuzu.

"Wachezaji wamefanya vizuri na wamejituma na kuhahakikisha wanavuka hatua hiyo na wamejituma sana nawapongeza na tumejifunza mengi sana Angola,"amesema Pluijm

Amesema  kikosi kwa sasa hakina cha kupoteza kitaendeea na kambi kuhakikisha wanasonga mbele katika mashindano hayo lengo lao ni kuona wanafika hatua ya fainali.
Golikipa wa timu ya Yanga Deogratius Munish Dida akizungumza na waandishi wa habari baada y kuwasili kutoka Angola.
 Kocha Mkuu wa Yanga Hans Van De Pluijm akiwasabahi mashabiki wa timu ya Yanga waliofika kuwalaki uwanja hapo mapema leo mchana.
 Wachezaji wa Yanga wakitoka  nje ya uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wakitokea nchini Angola
 Wachezaji wa Yanga wakitoka  nje ya uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wakitokea nchini Angola
 Kocha Mkuu wa Yanga Hans Van De Pluijm akiwasabahi mashabiki wa timu ya Yanga
  Wachezaji wa Yanga wakitoka  nje ya uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wakitokea nchini Angola.Picha na Zaynab Nyamka,Globu ya Jamii.

No comments: