Monday, May 2, 2016

YANGA YAANGUKIA PUA, YACHAPWA 3-1 NA SIMBA UGHAIBUNI, RENATUS NJOHOLE ATUPIA 1, NICO USIPIME

Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi akikabidhi kombe kwa nahodha wa Simba Bagasa
Mhe. Balozi Wilson Masilingi na mkewe Marystela Masilingi wakiwa katika picha ya pamoja na Timu ya Simba walioibamiza Yanga kwa bao 3-1 mechi iliyoanaliwa na DICOTA 2016 Dallas Texas.
Kikosi cha Simba Ughaibuni
Kokosi cha Yanga Ughaibuni.
Timu ya Simba iliendeleza ubabe kwa mara ya nne mfululizo nje ya DC baada ya jana Jumamosi April 30, 2016 kuibanjua timu ya Yanga bao 3-1 katika mechi iliyoandaliwa na kongamano la DICOTA 2016 lililomalizika siku ya Juamamosi jijini Dallas, Texas nchini Marekani.

Wanandugu wawili Nico Njohole na Renatus Njohole waliowahi kuichezea Simba ya jijini Dar es Salaam na timu ya Taifa kwa nyakati tofauti, walikua kizingiti kikubwa kwa Yanga ambao jana waliuanza mchezo kwa kasi na kupata bao la kuongoza kupitia mchezaji wao hatari Dulla Makubeli.

Baada ya bao hilo Simba ilitulia na kucheza soka la kitabuni huku ikiongozwa na wakongwe wawili ambao walicheza soka lililowashangaza wengi lililosaidia Simba kusawazisha bao safi katika dakika 44 ya kipindi cha kwanza kupitia mchezaji James Kitia. Bao hilo lillisababishwa na mchezaji Renatus Njohole baada ya kuambaa na mpira wingi ya kushoto na kutia krosi iliyomkuta James Kitia na kufunga goli zuri la kideo kwa kichwa,

Kipindi cha pili Simba walitulia zaidi na kucheza mpira wa kisasa kwa pasi fupi fupi huku wakiwasoma Yanga ambao muda mwingi walifanya mashambulizi ya kushutukiza huku wakitumia mipira mirefu.

Katika dakika ya 74, Renatus Njohole aliifungia Simba bao la tatu baada ya kuwatoka mabeki na kumpiga shuti nayvu ndogo na kumwacha kipa wa Yanga asijue la kufanya.

Bao la tatu la Simba lilifungwa na mchezaji Everist aliyefunga baada ya mabeki wa Yanga kuijisahau.

Mpaka dakika 90 Simba 3 Yanga 1.

Mchezaji Renatus Njohole akiambaa na mpira pembezoni mwa uwanja.

Wachezaji wa Simba wakisimama kwa dakika moja kwa ajili ya misina iliyotokea Houston, Texas kwa Watanzania Henry Kiherile na Andrew Sanga waliopoteza maisha kwa ajali ya kupigwa  risasi. Picha na Vijimambo/Kwanza Production.
Wachezaji wa Yanga wakisimama kwa dakika moja kwa ajili ya misina iliyotokea Houston, Texas kwa Watanzania Henry Kiherile na Andrew Sanga waliopoteza maisha kwa ajali ya kupigwa  risasi

Mchezaji Renatus Njohole akiwatoka mabeki wa Yanga.
Mke wa Balozi Marystela Masilingi akiwa uwanjani kuishabikia Simba.
Michezo si uadui ni furaha baada ya mechi tizu zote zikipiga picha ya pamoja huku kukiwa na bango la Njohole Legend Foundation.
Renatus Njohole akifunga goli la pili.



No comments: