Tuesday, May 24, 2016

WAKAZI WA MWANZA KUPATA HUDUMA ZA MAWASILIANO ZA VODACOM NDANI YA ROCKY CITY MALL.

 Mgeni rasmi wa uzinduzi wa duka jipya la Vodacom Tanzania, lililopo katika sehemu ya maduka makubwa(Rocky City Mall)jijini Mwanza, Mkuu wa Mkoa huo,John Mongella(watatu kushoto) Mkurugenzi wa Usambazaji bidhaa wa Vodacom Tanzania,Hassan Saleh(kushoto)pamoja na Meneja wa duka hilo,Yohana Mswahili wakifafanuliwa jambo na Mkuu wa kitengo cha wateja wa rejareja wa kampuni hiyo,Brigita Stephen(kulia) wakati wa uzinduzi wa duka hilo jana.
  Mkuu wa kitengo cha wateja wa rejareja wa kampuni hiyo, Brigita Stephen(kulia)akimuonesha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,John Mongella(wanne kushoto)   moja ya simu inayopatikana  kwa bei nafuu baada ya kuzindua duka jipya la kampuni hiyo, lililopo katika sehemu ya maduka makubwa(Rocky City Mall)jijini Mwanza jana,wengine katika picha ni wateja pamoja na Mkurugenzi wa Usambazaji bidhaa wa  kampuni hiyo,Hassan Saleh(kushoto).
 Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella(watatu kushoto) akikata keki kuashiria uzindua duka jipya la kampuni hiyo, lililopo katika sehemu ya maduka makubwa(Rocky City Mall)jijini Mwanza jana,Wengine katika picha kushoto Mteja wa duka hilo,Miraji Mtaturu,Meneja wa duka hilo,Yohana Mswahili na Mkurugenzi wa Usambazaji bidhaa wa  kampuni hiyo,Hassan Saleh.
 Mgeni rasmi wa Uzinduzi wa duka jipya la Vodacom Tanzania, lililopo katika sehemu ya maduka makubwa(Rocky City Mall)jijini Mwanza, Mkuu wa Mkoa huo,John Mongella(watatu kushoto)akimshuhudia Mkurugenzi wa Usambazaji bidhaa wa kampuni hiyo,Hassan Saleh(kulia)akimlisha keki Sara Jeremia,ambaye alikuwa Mteja wa kwanza kununua bidhaa katika  duka hilo baada ya kuzinduliwa rasmi jana.  Na Mkuu wa mkoa huo,katikati Meneja wa duka hilo,Yohana Mswahili.
  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella(watano kushoto) akigonganisha glasi na baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania,Ikiwa ni ishara ya Uzindua wa duka jipya la kisasa la kampuni hiyo lililopo katika sehemu ya maduka makubwa(Rocky City Mall)jijini humo jana.

No comments: