Mbunge
Shyrose Bhanji wa Tanzania akichangia mada
bungeni
wabunge mbalimbali wakichangia mada bungeni
wakati bunge la bajeti ya jumuiya ya afrika mashariki
likiendelea
wabunge wakijadiliana jambo wakati bunge
likiendelea
Na Woinde
Shizza,Arusha
Wabunge wa
bunge la Afrika mashariki wamesema kuwa wanamuunga mkono rais wa
jamuhuri ya Mungano wa Tanzania John Magufuli na watampa
ushirikiano katika kila jambo kwani anafanyakazi kwa makini na
vizuri .
Pamoja na
kumpongeza na kumuunga mkono Magufuli pia wameomba kukutana nae na
kujadili baadhi ya mambo.
Wakiongea na waandishi wa habari wabunge baadhi ya wabunge hao walisema kuwa wanafurahishwa sana na kasi ya magufuli kwani imekuwa na manufaa makubwa sio kwa watanzania pamoja na wananchi wa nchi za jumuiya ya afrika mashariki kwa ujumla.
" kasi ya
Rais Magufuli, imekuwa na
manufaa makubwa sio kwa watanzania bali kwa wananchi wote wa jumuiya ya
Afrika ya Mashariki"alisema Mbunge
Shyrose Bhanji wa Tanzania,
Aliongeza kuwa
vita
dhidi ya rushwa na ufisadi ambayo imeanzishwa na Rais Magufuli, ambaye
pia ni mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, inapaswa kuungwa mkono na bunge
hilo.
Mbunge
Martin Ngoga wa Rwanda, alisema kasi ya Rais Magufuli ambaye ni
mwenyekitiwa jumuiya hiyo,inapaswa kuungwa mkono na sio vibaya jumuiya
ya Afrika ya Mashariki, kuonesha kwa dhati inapambana na
rushwa.
"Rais
Magufuli anafanyakazi nzuri sana na sisi kama wabunge tunamuuunga mkono
ili kuwa na manufaa katika jumuiya ya Afrika ya Mashariki mataifa yote
yanapaswa kushirikiana kuondoa rushwa"alisema
No comments:
Post a Comment