• Wawezeshwa vitendea kazi vyenye dhamani ya shilingi milioni tano.
Dar Es Salaam Mei 21, 2016, Airtel Tanzania inaendeleza dhamira yake ya kuendelea kuwashika mkono vijana hapa nchini ambapo
mwishoni mwa wiki hii kupitia mpango wake wa kutoa semina ya mafunzo ya
ujasiriamali kwa vijana ujulikanao kama Airtel FURSA Tunakuwezesha,
uliweza kuchagua vijana wawili walioweza kuelezea na kuwakilisha
changamoto wanazozipata katika biashara wanazozifanya mbele ya jopo la
washauri ambao leo hii wamekabidhiwa vitendea kazi vyenye dhamani ya shilling milioni 5 ili kuweza kukabiliana na changamoto hizo.
Akizungumza
wakati wa sherehe ya makabidhiano hayo, Meneja wa Airtel huduma kwa
Jamii Hawa Bayumi alisema "baada ya kufanya mafunzo ya biashara ya
ujasiriamali wiki chache zilizopita na kuweza kufikia vijana zaidi ya
300 jijini Dar Es Salaam waliojitokeza
na kuzifahamu vyema FURSA zinazowazunguka ili kujitengenezea ajira na
na uwezo wa kujenga fursa nyingine. Leo hii tupo hapa kuwawezesha hawa
walioonyesha bidi zaidi”
“Na
siku hiyo ilikuwa ni siku ya faraja kwani vijana waliweza kujifunza
mambo mengi sana na mwisho wa siku waliweza kuelezea na kuwasilisha
biashara zao mbele ya jopo la washauri na ulikuwa uamuzi mgumu sana
lakini mwisho wa siku tuliweza kupata vijana wawili bora walioweza
kushinda nyoyo za jopo la washauri hao, ambao leo hii tupo hapa kwajili ya kuwakabidhi vifaa vyao ili waweze kwenda kukabiliana na changamoto walizonazo katika biashara zao. "
Mpaka
sasa Airtel imefanya semina nyingi sana za mafunzo ya biashara ya
ujasiriamli hapa nchini katika mikoa mbali mbali na kuweza kufikia
vijana wapatao 4000. Lakini hii ni mara ya kwanza kwa Airtel
kufanya semina hiyo na hapo hapo kuchagua vijana wawili walioweza
kuwezeshwa kwa kupatiwa vitendea kazi katika semina hiyo.
Huu
ni mfumo mpya ambao Airtel Fursa umeuanzisha kwani zaidi ya kuwapa
elimu ya mafunzo ya biashara ya ujasiriamali vile vile watawezeshwa
kuongezewa nguvu mali na kuimarisha biashara wanazozifanya. Airtel
kupitia mpango wake wa Airtel FURSA itaendelea kutoa warsha hizi katika
maeneo mbalimbali hapa nchini ili kuhakikisha inafikia vijana wengi
zaidi.
Hivyo tunawahamasisha vijana wanaposikia nafasi kama hii popote walipo , kuchangamkia kwa kuhudhuria kwani elimu inayotolewa ni bure kabisa bila gharama yoyote. "aliongeza Bayumi.
Nae kwa upande wake kijana Stephen Gimase, mmoja wa vijana aliyeshinda kwa kuweza kuelezea
na kuwakilisha changamoto anazozipata katika biashara waliyonayo mbele
ya jopo la washauri wiki chache zilizopita katika mafunzo hayo,
anayejishughulisha na shughuli za kutotoa vifaranga vya kuku, alisema ,”naishukuru sana Airtel kwa kunipatia vifaa vya kisasa kwa ajili ya biashara yangu. Naahidii kuwa
nitafanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha nakuza biashara yangu na
kujenga ajira kwa vijana wengine hapa nchini. Hii ni atua ya kwanza ya
mafanikio ya maisha yangu nawashukuru Airtel kwa kuwa sehemu ya maisha
safari yangu ya mafanikio "alisema Stephen.
Kijana mwingine aliyeweza kupata bahati ya kuwezeshwa na Airtel FURSA katika mafunzo hayo ni
msanii wa kuchora picha, Theresia Maliatabu ambaye amewezeshwa kwa
kupatiwa vitendea kazi kwa ajili ya kuendeleza biashara yake kwa
kupatiwa kompyuta na ubao wa kisasa wa kuchorea picha zake . Wakati wa
sherehe ya makabidhiano hayo , Theresia aliwashukuru Airtel kwa kuweza
kumshika mkono , na kuahidi kwamba ataifanya kazi yake kwa ubora zaidi
na kuweza kufikia ndoto yake ya kuwa mchoraji bora na maarufu hapa
nchini na hata nje tya nchi.
Tunaamini
kwamba kupitia mpango huu wa mafunzo ya biashara ya ujasiriamali
yanayotolewa na Airtel Fursa tunaamini vijana wengi watatoka na
kukimbilia mafunzo haya kwani watakuwa wameweza kunufaika na kupata
mafunzo haya katika nyanja mbali mbali za kuwawezesha kuanzisha na
wengine kuweza kuendeleza biashara zao kwa njia ya ufanisi zaidi.
Stephen
Gimase (Kulia) ambaye ni miongoni wa vijana waliowezeshwa na mpango wa
Airtel FURSA “Tunakuwezesha” akiangalia vifaa alivyokabidhiwa na Airtel
FURSA kwa ajili ya kuboresha biashara yake ya kutengeneza mashine za
kutengenezea vifaranga vya kuku, Kushoto ni Meneja wa huduma za jamii wa
Airtel, Hawa Bayumi
Meneja
wa huduma za jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (2 Kushoto) akimkabidhi
Theresia Maliatabu (Kulia) ambaye ni miongoni wa vijana waliowezeshwa na
mpango wa Airtel FURSA “Tunakuwezesha” vifaa vyakuboresha biashara yake
ya uchoraji ikiwemo meza ya kuchorea na kompyuta ya kisasa. Kijana huyu
Aliyechaguliwa kutoka kwenye mafunzo ya biashara ya ujasiriamali ya
Airtel FURSA yaliyofanyika Dar es Salaam wiki chache zilizopita.
Akishuhudiwa na mama yake mzazi Judith Benedicto (Katikati) na mama
mkubwa Salome Benedicto (Kulia) pamoja na Afisa mauzo wa Airtel katika
hafla iliyofanyika Mbagala kuu, jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment