Hapa
ni katika Msikiti wa Masjid Latif Ahmadiyya Muslim Jamaat Nsalala
uliopo kijiji cha Nsalala ,kata ya Tinde wilaya ya Shinyanga ambapo leo
Jumapili Mei 22,2016 Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Mkoa wa
Shinyanga(Ahmadiyya Muslim Jamaat Shinyanga) imefanya mkutano wa Mwaka
wa Jumuiya hiyo Mkoa wa Shinyanga ukiwa na kauli mbiu ya " Love For All
Hatred For None (Mapenzi Kwa Wote Bila Chuki Kwa Yeyote".
Mgeni
rasmi alikuwakatibu tawala msaidizi idara ya uchumi na uzalishaji
aliyemwakilisha kaimu mkuu wa mkoa wa Shinyanga John Mongella huku
waumini wa dini hiyo kutoka ndani na nje ya mkoa wa Shinyanga
wakihudhuria mkutano huo.
Mkutano
huo uliolenga kuhamasisha amani katika jamii kwa kuwakumbusha waumini
kumjua mwenyezi mungu hali itakayosaidia kupunguza hata kumaliza kabisa
vitendo vya kihalifu ikiwemo mauaji ya watu wasio na hatia kama vile
vikongwe na albino, umehudhuriwa pia na Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya
Waislam wa Ahmadiyya Tanzania Maulana Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry
(pichani juu).
Akizungumza
katika mkutano huo Mkuu wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Tanzania
Maulana Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry alieleza kusikitishwa na kitendo
cha mauaji ya watu watu msikitini na kuongeza kuwa dini ya kiislam
hairuhusu vitendo kama hivyo huku akiviomba vyombo vya dola kufanya
uchunguzi ili kubaini wahusika wa kitendo hicho haramu.
Kupitia
mkutano huo jamii imeelimishwa juu ya dhana potofu dhidi ya uislamu
ambapo baadhi ya watu wamekuwa wakihusisha dini hiyo pamoja na vikundi
vya kigaidi mfano wa Boko haram, Isis, Al-shabaab na vingine vingi
ambavyo vimekuwa vikidhuru binadamu.
Mada
mbalimbali zimetolewa na viongozi wa jumuiya hiyo ikiwemo nafasi ya
dini katika maisha ya binadamu,malezi ya watoto na majukumu ya wazazi
sawa na mafundisho ya dini ya kiislamu,umuhimu wa kuwa kiongozi
(Khalifa) wa kiroho na barakaza ukhalifa pamoja na masharti ya kujiunga
na jumuiya hiyo(masharti 10 ya Baiat na wajibu wa waumini.Mwandishi mkuu
wa Malunde1 blog,Kadama Malunde alikuwepo wakati wa mkutano
huo,ametusogezea picha 55 kilichojiri..
Hapa
ndipo Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Mkoa wa Shinyanga
waumini wa dini ya kiislamu kutoka Jumuiya hiyo kutoka ndani na nje ya
mkoa wa Shinyanga wamejitokeza kwa wingi kusikiliza mawaidha mbalimbali
kutoka kwa viongozi wa Jumuiya hiyo pamoja na wageni waalikwa akiwemo
kaimu mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mohammed Idd Nchira
Bango likionesha kilichokuwa kinaendelea
Katibu
Mkuu Msaidizi wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya nchini Tanzania
Abdulrahman Mohammed Ame akitoa mada kuhusu Haja ya nafasi ya dini
katika maisha ya binadamu ambapo alitumia fursa hiyo kuitaka jamii
kutenda mambo mema na kujiepusha na vitendo vya kihalifu ikiwemo kuua
watu wenye ulemavu wa ngozi na vikongwe.
Alisisitiza
kuwa uislamu ni dini ya amani hivyo kuwataka binadamu kuishi kwa amani
na kwamba kitendo cha kuua mtu mmoja ni sawa na kuua dunia nzima.Hata
Hivyo Ame alisema sera ya jumuiya hiyo ni kutochanganya siasa na dini
Meza
kuu,wa pili kutoka kulia ni Mkuu wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya
Tanzania Maulana Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry,kushoto kwake ni mgeni
rasmi Mohammed Idd Nchira,akifuatiwa na rais wa Jumuiya hiyo Kanda ya
Ziwa Salim Thani,wa kwanza kushoto ni Naibu rais wa jumuiya hiyo Kanda
ya ziwa Yahaya Kamba Ulaya.Wa kwanza kulia ni Mbashiri wa kanda ya ziwa
wa jumuiya hiyo Sheikh Waseem Khan
Waumini wa dini ya Kiislam kutoka maeneo ya mjini na Vijijini ndani na nje ya mkoa wa Shinyanga waliojitokeza katika mkutano huo
Mgeni rasmi katika mkutano huo Mohammed Idd Nchira akiwahutubia waumini wa dini ya kiislamu wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya
Moja ya mabango yaliyokuwa katika mkutano huo
Mgeni
rasmi katika mkutano huo Mohammed Idd Nchira akiwahutubia waumini wa
dini ya kiislamu wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya ambapo alisema suala
amani katika jamii ni watu wote hivyo kuwataka watanzania kudumisha
amani ya nchi kwa kuepuka kutenda uhalifu
Aliyesimama
ni Afisa wa polisi kutoka ofisi ya mkuu wa upepelezi na makosa ya jinai
mkoa wa Shinyanga Issa Ramadhan akitoa neno ambapo alisema jamii yenye
malezi mema haiwezi kuwa na vitendo vya kihalifu na kuwaomba wananchi
kuendelea kushirikiana na jeshi la polisi kuwafichua watu wote
wanaofanya vitendo vya uhalifu
Wanawake
wa Kiislam wakiwa katika Msikiti wa Masjid Latif Ahmadiyya Muslim
Jamaat Nsalala uliopo kijiji cha Nsalala ,kata ya Tinde wilaya ya
Shinyanga wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea katika mkutano huo wa
mwaka,ambapo kwa mara ya pili sasa mkutano kama huo unafanyika mkoani
Shinyanga,mkutano mwingine ulifanyika mwaka 2014
Wanawake wakiwa msikitini
Mkuu
wa kituo cha polisi Tinde Mkaguzi Msaidizi wa polisi Wilbert Sichone
aliyemwakilisha mkuu wa polisi wilaya ya Shinyanga,akitoa neno katika
mkutano huo ambapo aliwaomba viongozi wa dini mbalimbali kuendelea kutoa
elimu ya dini kwani vitendo vingi vya kihalifu vimekuwa vikijitokeza
kutokana na jamii kutokuwa na hofu
Mwenyekiti
wa Kijiji cha Nsalala kilichopo katika kata ya Tinde Sandeko Machongo
akitoa shukrani kwa jumuiya hiyo kwa kushirikiana na wananchiwa kijiji
hicho katika masuala mbalimbali ikiwemo ujenzi wa visima vitatu vya maji
Waumini wakifutilia kilichokuwa kinaendelea kwenye mkutano huo
Mbashiri/Sheikh
wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya mkoa wa Morogoro Asif Butt akitoa
mada ya Masharti kumi ya Baiat na wajibu wa waumini wa jumuiya
hiyo.Miongoni mwa masharti hayo ni pamojana waumini kutojihusha na
vitendo vya kishirikina akieleza kuwa ushirikina ndiyo chachu ya
maovu/mabaya yote katika jamii
Tunamsikiliza Mbashiri wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya mkoa wa Morogoro Asif Butt
Mbashiri
wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya mkoa wa Morogoro Asif Butt alitumia
fursa hiyo kuwataka wanadamu kuwapuuza baadhi ya watu wanaodai kuwa
jumuiya hiyo haifuati misingi ya dini ya kiislam huku akiongeza kuwa
tofauti yao na wengine wao wanafanya misingi ya dini kwa vitendo badala
ya maneno
Meza kuu wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea katika mkutano huo
Tunafuatilia kinachoendelea hapa......
Waumini wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea katika mkutano huo
Watoto wakiwa msikitini wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea katika mkutano huo
Mkuu
wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Tanzania Maulana Sheikh Tahir
Mahmood Chaudhry akitoa hotuba yake ambapo pamoja na mambo mengine
alisema jumuiya hiyo ambayo ipo katika nchi 207 duniani kila siku
imekuwa ikiwakumbusha waumini kuishi katika misingi ya kumfuata mwenyezi
mungu,kwasisitiza waumini kushika mafundisho kwa vitendo badala ya
maneno ili wawe raia wema ili jamii iishi kwa amani
Mkuu
wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Tanzania Maulana Sheikh Tahir
Mahmood Chaudhry alieleza kusikitishwa na mauaji ya watu watatu jijini
Mwanza katika msikiti na kusema kuwa dini ya kiislamu hairuhusu watu
kuuana na kuwaomba wakazi wa Mwanza na nchi kwa ujumla kuendelea kuwa
watulivu wakati vyombo vya ulinzi na usalama vikifanya uchunguzi ili
kujua chanzo cha mauaji na kuwabaini wahusika wa mauaji hao
Mkutano unaendelea
Mkutano unaendelea
Tunamsikiliza Mkuu wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Tanzania Maulana Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry
Mkuu
wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Tanzania Maulana Sheikh Tahir
Mahmood Chaudhry akisisitiza kuwa jumuiya hiyo ya kimataifa ina uongozi
wake na inaendeshwa kwa heshima kubwa na siku zote wamekuwa wakihubiri
amani
Mkuu
wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Tanzania Maulana Sheikh Tahir
Mahmood Chaudhry akiwaomba watanzania kuachana na vitendo vya kihalifu
ikiwemo kuua albino na vikongwe kwa imani za kishirikina
Kulia
ni Katibu Mkuu Msaidizi wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya nchini
Tanzania Abdulrahman Mohammed Ame akitafsiri hotuba ya Mkuu wa Jumuiya
ya Waislam wa Ahmadiyya Tanzania Maulana Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry
aliyokuwa anaitoa kwa lugha ya Kiingereza
Kulia
ni Katibu Mkuu Msaidizi wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya nchini
Tanzania Abdulrahman Mohammed Ame akitafsiri hotuba ya Mkuu wa Jumuiya
ya Waislam wa Ahmadiyya Tanzania Maulana Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry
aliyokuwa anaitoa kwa lugha ya Kiingereza.Chaudhry alisema ili jamii
iishi kwa amani ni vyema binadamu wakaishi kwa kupendana na kuacha
vitendo vya kishirikina na kulipishana visasi
Mabango yakiwa katika eneo la mkutano
Mabango yakiwa na ujumbe wa aina mbalimbali katika eneo la mkutano
Jumuiya
ya Waislam wa Ahmadiyya ina kiongozi mkuu duniani ambaye sasa anaitwa
Khalifatul Masih v Hazrat Mirza Masroor Ahmad ambaye miongoni mwa
majukumu yake ni kujitahidi kuwaomba wanadamu kuishi kwa kuzingatia
misingi ya amani.
Viongozi
wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya wakijiandaa kuomba dua wakati wa
mkutano,kushoto ni Mkuu wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Tanzania
Maulana Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry katikati ni Katibu Mkuu Msaidizi
wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya nchini Tanzania,kulia ni rais wa
Jumuiya hiyo Kanda ya Ziwa Salim Thani
Kulia
ni rais wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Kanda ya Ziwa Salim Thani
akiteta jambo na kiongozi wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Mkoa wa
Shinyanga Shaaban Luseza (kushoto)
Kulia
ni rais wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Kanda ya Ziwa Salim Thani
akiteta jambo na kiongozi wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Mkoa wa
Shinyanga Shaaban Luseza (kushoto)
Waumini wa Jumuiya hiyo wakiwa wamesimama wakati wa kuomba dua
Waumini wakiwa tayari kuomba dua
Waumini wakiwa wamesimama wakati wa kuomba dua
Tunaomba dua
Akina mama wakiwa ndani ya msikiti wakiomba dua
Viongozi
wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya wakiomba dua wakati wa
mkutano,kushoto ni Mkuu wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Tanzania
Maulana Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry katikati ni Katibu Mkuu Msaidizi
wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya nchini Tanzania,kulia ni rais wa
Jumuiya hiyo Kanda ya Ziwa Salim Thani
Kushoto
ni Yusuph Mgeleka kutoka mkoa wa Shinyanga ,Mubarak Nyamihasi kutoka
mkoani Mwanza(katikati) na Mussa Kaswezi kutoka mkoa wa Kagera(kulia)
wakiimba shairi la kuagana wakati wa kufunga mkutano huo
Wanawake na watoto wakiwa nje ya msikiti baada ya mkutano kufungwa
Bango katika mkutano huo
Picha ya kumbukumbu baada ya mkutano huo kumalizika
Bango likiwa katika mkutano huo
Bango likiwa katika mkutano huo wa mkoa wa Shinyanga ulioandaliwa na Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Mkoa wa Shinyanga
Bango likionesha ujumbe mzuri
Bango jingine lilokuwa katika mkutano huo
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
No comments:
Post a Comment