Sunday, May 29, 2016

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

SIMU.tv: Baadhi ya wakazi katika halmashauri ya Momba mkoa mpya wa Songwe wameitaka serikali kuwawajibisha viongozi wao kwa kushindwa kutoa taarifa za mapato na matumizi; https://youtu.be/LJAvNtaNAqg

SIMU.tv: Waziri wan chi ofisi ya makamu wa rais muungano na mazingira January Makamba amewataka watanzania kutunza mazingira hususani misitu ili kuwezesha kutunza vyanzo vya maji; https://youtu.be/KFb4Ij5gc2s

SIMU.tv: Baadhi ya wananchi wilayani Bukoba mkoani Kagera wameiomba serikali kuboresha usikivu kwa shirika la habari Tanzania TBC hili kuendana na kasi ya teknolojia;https://youtu.be/22oMGWV4i_A

SIMU.tv: Basi la Mwendokasi limegongwa na gari dogo katika eneo la Magomeni baada ya dereva wa gari dogo kukatisha barabara bila kuzingatia alama za barabarani;https://youtu.be/KPWSfCLD46A

SIMU.tv: Tanzania inakadiriwa kuwa na uwezo mkubwa wa kujitegemea kwa chakula chake baada ya kuzinduliwa kwa mpango wa Vuna utakaowezesha vijana kujikita katika kilimo; https://youtu.be/k7PrQX4AIVk

SIMU.tv: Baadhi ya wakulima wa zao la tumbaku wilayani Uvinza mkoani Kigoma wameitaka serikali kufanya uchunguzi kwa chama cha msingi cha Sagara Amcos  kwa kufanya ubadhilifu wa zaidi ya shilingi milioni 30; https://youtu.be/-qZF6AAwvVs

SIMU.tv: Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa ndugu George Mbijima amewataka wanafunzi wa kike kuwekea bidii katika masomo ya sayansi;https://youtu.be/rudnALzEosM

SIMU.tv: Mwanamke mmoja mkoani Ruvuma anadaiwa kumtupa mtoto mchanga jalalani mara baada ya kujifungua mtoto huyo; https://youtu.be/FpokZH2KQpI

SIMU.tv: Timu ya soka ya taifa Taifa stars imetoka sare ya kufungana goli 1-1 na timu ya taifa ya Kenya harambee stars kwa magoli ya Maguli na Wanyama kwa upande wa Kenya;https://youtu.be/BeR4OGpOJeQ  

SIMU.tv: Mashindano ya mkuu wa majeshi yamefikia wiki moja sasa huku ushindani ukiwa unazidi kuongezeka na kuwaridhisha wandaaji wa mashindano hayo;https://youtu.be/1Yr4ylPKtGw

SIMU.tv: Maonyesho ya nguo za stara nchini Tanzania yanatarajia kufanyika tena nchini kuanzia tarehe 1-5 nwezi ujao huku washiriki wakiwa wabunifu wa ndani pekee;https://youtu.be/KV9RqXASxZQ

SIMU.tv: Taasisi ya michezo na burudani yazinduliwa nchini Tanzania huku kukiwa na malengo ya kuweka afya za wananchi fiti; https://youtu.be/CZAxVzT_BDk

SIMU.tv: Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Ben Pol amesema wimbo wake wa Sophia umemsaidia kufika mbali kimuziki na kumuongezea umaarufu kwa jamii ya kitanzania; https://youtu.be/lkH7r1zAQiI

SIMU.tv: Mabasi ya mwendo kasi jijini Dar es Salaam yamezidi kuandamwa na ajali za mara kwa mara kutokana na madereva wazembe kutozingatia sheria za barabarani.https://youtu.be/lVEH79rGGKM

SIMU.tv: Makamu wa rais mstaafu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr Gharib Bilal amewataka waumini wa dini ya kiislamu kuzingatia mafunzo na maonyo ya dini katika kuelekea mwezi mtukufu wa Ramadhani. https://youtu.be/M4RVmHM2USs

SIMU.tv: Ongezeko la ushiriki wa mashirika ya kigeni kwenye maonesho ya biashara ya kimataifa ya Karibu Fair yanayofanyika katika mkoa wa Arusha ni ishara tosha la ongezeko la watalii kutoka nje ya nchi. https://youtu.be/cigMcJblhkA

SIMU.tv: Wakazi 174 kati ya 864 waliohamishwa na manispaa ya Ilala kupisha upanuzi wa uwanja wa ndege wamelalamikia kupewa viwanja hewa na serikali kama fidia.https://youtu.be/D3gWO-dLu38

SIMU.tv: Viongozi wa halmashauri za vijiji wanoshindwa kuchukua hatua mathubuti na kuchukua sheria kwa wanaoharibu misitu wametajwa kuwa waochangia uharibifu huo kuendelea. https://youtu.be/gIQHEhThQxI

SIMU.tv: Tatizo la upungufu wa madawati nchini limetajwa haliwezi kwisha kama serikali na shule husika hazitaweka utaratibu wa kukarabati madawati yanayoharibika.https://youtu.be/dMedd_TwlYc

SIMU.tv: Mkuu wa wilaya ya Kinondoni amewaonya wafanya biashara wanaotegemea kupandisha bei ya vyakula wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani. https://youtu.be/-khnKwxyLjY

SIMU.tv: Kikwazo kinacho wakabili wakulima kushindwa kukopa fedha kutoka katika mabenki ili waweze kuendeleza kilimo cha kisasa kimetajwa kuwa ni masharti magumu yanayowekwa na asasi hizo za kifedha. https://youtu.be/6bADU5veDyo

SIMU.tv: Waalimu na wanafunzi wa shule ya msingi Genesis iliopo jijini Dar es Salaam wametoa msaada wa vyakula na vifaa vya shule kwa watoto wenye shida mbali mbali wanaoishi katika  makao ya taifa ya watoto wenye shida Kurasini.https://youtu.be/5SzltvJwgJg

SIMU.tv: Wazazi nchini wametakiwa kuwa na tabia ya kujali afya za watoto wao kwa kuwapima afya zao mara kwa mara na sio kusubiri mpaka waugue.https://youtu.be/3N71QZpOB8A

SIMU.tv: Taifa stars imewalazimisha timu ya Kenya Harambee stars sare ya bao moja kwa moja kwenye mchezo wa kirafiki uliochechwa kwenye uwanja wa Kasarani jijini Nairobi.https://youtu.be/K4WBrQ1TqIQ

SIMU.tv: Mbio za baiskeli mkoani Simiyu zimebaini ubovu wa viwanja ambapo mkuu wa mkoa wa Simiyu akalazimika kutoa agizo kwa mkurugenzi wa halmashauri ya Bariadi kuhakikisha anarekebisha viwanja hivyo ndani ya siku kumi na nne. https://youtu.be/-KC9IW-2sfE

SIMU.tv: Mafunzo ya utawala wa uongozi wa michezo yaliyokuwa yakiendeshwa mkoani Singida yamekamilika huku washiriki wakilalamikia ushiriki mdogo wa wanawake.https://youtu.be/f7dkNO1psx4

SIMU.tv: Mabingwa mara kumi na moja wa kombe la UEFA Real Madrid wamerejea jijini Madridi na wamepokelewa kwa shangwe kubwa. https://youtu.be/QYH_ddOSwl0

No comments: