Tuesday, May 24, 2016

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

Simu.tv: Serikali ya Tanzania imesema bado inaendelea kuimarisha vyombo vya ulinzi na usalama ili kumaliza kabisa tatizo la ujangili nchini ikiwa ni pamoja na kununua vifaa zaidi vya doria; https://youtu.be/EHqwnmjfAwM

Simu.tv: Waziri wa nchi ofisi ya rais utumishi na utawala bora Angela Kairuki amesema mahakama ya kushughulikia mafisadi inatarajia kuanza kufanya kazi julai mwaka huu;https://youtu.be/HjCnMVPFunU

Simu.tv: Mratibu wa mazungumzo ya kutafuta amani nchini Burundi Rais Mstaafu wa awamu ya tatu wa Tanzania Mh Benjamin William Mkapa amekamilisha awamu ya kwanza ya mazungumzo hayo na atakabidhi ripoti  kwa msuluhishi mkuu rais wa Uganda Mh Yoweri Kaguta Museveni; https://youtu.be/E4CiXA_8ouw

Simu.tv: Mkurugenzi mkuu wa shirika la utangazaji Tanzania TBC Dkt Ayoub Rioba amesema taratibu za kisheria zifuatwe ili kuwafukuza wavamizi wa kiwanja cha shirika hilo huko Tabora; https://youtu.be/7Enu6E7LkRo

Simu.tv: Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dkt Mohamed Shein amewaapisha leo wakuu wa miko na wilaya aliowateua visiwani humo;https://youtu.be/b_oJ3X_x3F0  

Simu.tv: Mwili wa aliyekuwa mkurugenzi wa jiji la Dar es salaam Wilson Kabwe umeagwa hii leo katika viwanja vya Karimjee kuelekea Same mkoani Kilimanjaro tayari kwa mazishi;https://youtu.be/QCnSmP0MhYY   

Simu.tv: Katibu mkuu ofisi ya waziri mkuu Dr Hamis Mwinyimvua amesema serikali imejitahidi kuboresha mazingira ya kibiashara ili kuweza kuvutia wawekezaji zaidi;https://youtu.be/mnLwGf_36kk

Simu.tv: Mpango wa kilimo cha kisasa kinachokabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi kinachoratibiwa na nchi za Tanzania, Zambia, Malawi umezinduliwa jijini Dar es salaam;https://youtu.be/O60MNPo2jc8
  
Simu.tv: Maonyesho ya masuala ya utalii yanayoratibiwa na Karibu travel yanatarajiwa kufanyika nchini Arusha yakijumuisha nchi mbalimbali barani Afrika na Ulaya;https://youtu.be/IIP1ucwTMc8

Simu.tv: Idadi ya wanunuzi wa magari katika viwanja vya Coco Mihogo imeongezeka kutoka magari matano mpaka kumi na tano ndani ya miezi mitatu tokea kuanzishwa kwa soko hilo; https://youtu.be/qMxbOG8sQm0  

Simu.tv: Mabingwa wa soka Tanzania bara Yanga wamepangwa kundi moja na timu tishio ya nchini Congo DRC katika michuano ya shirikisho barani Afrika;https://youtu.be/Kzt4hIK7C40

Simu.tv: Mashindano ya jeshi ya mkuu wa majeshi yamezinduliwa hii na waziri mwenye dhamana hiyo Mh Nape Nnauye na kuwataka wamanichezo kujituma ili kupata timu nzuri ya jeshi; https://youtu.be/tTMl1ct2oQg

Simu.tv: Wanariadha mbalimbali na waendesha baiskeli wameombwa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha ili kushiriki kwenye tamasha la Majimaji serebuka huko Songea mkoani Ruvuma; https://youtu.be/JIm1LBoevUA

Simu.tv: Timu ya soka ya Azam imetamba kuonyesha kiwango kizuri kuelekea mchezo wao wa fainali ya kombe la FA na dhidi ya mabingwa wa soka nchini timu ya Yanga;https://youtu.be/vn_5JjYrO1Q
Simu.tv: Bendi ya muziki wa dansi nchini Twanga Pepeta wamepenga kuzindua albamu yao wiki hii mkoani mwanza na fedha itakayopatikana itatumika kununulia madawati kwa ajili ya wanafunzi wetu nchini; https://youtu.be/J6LKuqv3QMA
Simu.tv: Cristiano Ronaldo leo aliamua mazoezini na kuzua hofu kubwa juu ya kucheza mchezo wa fainali ya UEFA dhidi ya mahasimu wao Atletico Madrid; https://youtu.be/1-J0DScgrmg

Simu.tv: Makamu wa rais Bi Samia Suluhu Hassan amewataka watendaji wa serikali kuanzia ngazi ya mawaziri mpaka chini kuhakikisha wanapambana na kuthibiti vitendo vya rushwa nchini. https://youtu.be/f2Mg7ORNzKM
Simu.tv: Wananchi wilayani Babati wametoa madai yao mbele ya mkuu wa wilaya hiyo kuhusu shamba la ekari 600 lililomilikishwa kwa mwekezaji ambae hana mchango wowote kwenye kijiji. https://youtu.be/hKfL6fR0_dE
Simu.tv: Mgogoro wa ardhi dhidi ya wananchi wa kata ya Kiseke na halmashauri ya Ilemela jijini Mwanza umeibuka upya baada ya halmashauri hiyo kuwataka walipe kodi za majengo wakati nyumba zao hazina namba. https://youtu.be/jT4tN7KfWCs

Simu.tv: Wavuvi na wachuuzi wa Samaki katika wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma wameandamana pembezoni mwa ziwa Nyasa ilikufikisha kero zao kwa serikali ikiwepo gharama za lesseni na kukosekana kwa boti ya kuokolea katika ziwa hilo.https://youtu.be/ayIXaZm9ae8

Simu.tv: Mamia ya waombolezaji Jijini Dar es Salaam wameshiriki katika kuaga mwili wa aliekua mkurugenzi wa jiji la Dar es Salaam Ndugu Willson Kabwe katika ukumbi wa Karimjee. https://youtu.be/nPnI6Ir47qo

Simu.tv: Serikali mkoani Mara imeanzisha operesheni ya kuhahakikisha inawakamata wananchi watakaoshindwa kutimiza agizo la kulima ekari mbili ili kuokoa baa la njaa.https://youtu.be/h39ytV1dH1Y

Simu.tv: Walimu wilayani Newala mkoani Mtwara wameandamana mpaka kwa mkurugenzi wa halmashauri hiyo ili kufikisha madai yao ambayo hayasikilizwi ikiwa ni pamoja na kutopandishwa madaraja kwa muda mrefu. https://youtu.be/e2fBzoI4ERY

Simu.tv: Kituo cha uwekezaji nchini TIC kimeridhishwa na eneo la hekta 72 lililotengwa na halmashauri ya mkoa wa Tanga kwa ajili ya ujenzi wa viwanda.https://youtu.be/dOTn_6Ffs-M

Simu.tv: Uuzaji wa korosho nje ya mfumo wa stakabadhi ghalani umekua changamoto ambayo imewafanya baadhi ya wakulima wa korosho wameshindwa kulipia pembejeo.https://youtu.be/hG6JynrkDWM

Simu.tv: Timu ya Yanga imepangwa katika kundi A katika michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika ambapo wapo na wababe wa soka Afrika TP Mazembe. https://youtu.be/6-FZVnQo6xw

Simu.tv: Timu ya Azam FC inauona mchezo wa fainali za kombe la FA kuwa mchezo mgumu wakati Yanga inauona kama mchezo wa kulinda heshima.https://youtu.be/ie8pb97AMaQ

Simu.tv: Waziri wa habari sanaa na michezo amezindua mashindano ya kombe la mkuu wa majeshi maarufu kama CDF na kuwakumbusha nidhamu michezoni ni muhimu.https://youtu.be/IkMUi026w0w
Simu.tv: Azam fc imezindua duka lake la vifaa vya michezo vya timu hiyo ambapo litatoa fursa kwa mashabiki wa timu hiyo kupata vifaa vyenye nembo ya timu hiyo.https://youtu.be/xl1oGqT1xXs

Simu.tv: Simu.tv: Kamati ya Olimpiki Tanzania imesema migogoro mingi ya vyama vya michezo nchini inasababishwa na viongozi wa vyama hivyo kuweka maslahi yao mbele.https://youtu.be/8mljoVnycgA

Simu.tv: Kundi la muziki wa kizazi kipya nchini maarufu kama Navy Kenzo ijuaa hii litapamba sherehe za kumtafuta Miss IFM. https://youtu.be/5d6HtD-ZOU8

Simu.tv: Shirikisho la soka duniani FIFA limemfukuza kaimu katibu mkuu wa shirikisho hilo baada ya kugundulika kutumia vibaya madaraka kwa kuidhinisha mishahara kwa viongozi bila kushirikisha wajumbe. https://youtu.be/1XB09pLo8DE

No comments: