Monday, May 9, 2016

Profesa Muhongo azindua Tovuti na Mpango wa Ugawaji Madawati, Musoma Vijijini.

 Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ( wa kwanza Kulia) akielekea kupanda Boti ya kumpeleka Musoma Mjini mara baada ya kuzindua  Mpango wa ugawaji madawati katika Jimbo hilo uliofanyika katika shule ya Rukuba iliyopo katika kisiwa cha Rukuba ambayo ilipata madawati 100 huku zoezi hilo likiwa ni endelevu. Wa Pili kutoka kulia ni Mhandisi Joseph Kumburu.
 Walimu wa Shule ya Msingi Rukuba katika Jimbo la Musoma Vijijini wakiwa wamekaa kwenye madawati yaliyotolewa na Mbunge wa Jimbo hilo ambaye pia ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo mara baada ya kuzindua  Mpango wa ugawaji madawati katika Jimbo hilo ambapo shule hiyo iliyopo katika kisiwa cha Rukuba ilipata madawati 100 huku zoezi hilo likiwa ni endelevu.
 Wanafunzi wa Shule ya Msingi Rukuba katika Jimbo la Musoma Vijijini wakiwa wamekalia madawati yaliyotolewa na Mbunge wa Jimbo hilo ambaye pia ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo mara baada ya kuzindua  Mpango wa ugawaji madawati katika Jimbo hilo ambapo shule hiyo iliyopo katika kisiwa cha Rukuba ilipata madawati 100 huku zoezi hilo likiwa ni endelevu.
Wananchi wa Kijiji cha Saragana katika Jimbo la Musoma Vijijini (kushoto) wakifuatilia uzinduzi Tovuti ya Jimbo ambapo wadau mbalimbali wa ndani na nje nchi watapata taarifa mbalimbali kuhusu Jimbo hilo. Uzinduzi wa Tovuti hiyo ulifanywa na Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (hayupo pichani).
  Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ( wa Pili kushoto) akipeana mkono na mmoja wa Wanafunzi katika Shule ya Msingi Rukuba iliyopo jimboni humo ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa  Mpango wa ugawaji madawati katika Jimbo hilo ambapo shule hiyo iliyopo katika kisiwa cha Rukuba ilipata madawati 100 huku zoezi hilo likiwa ni endelevu.

MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amezindua Tovuti ya Jimbo la Musoma Vijijini ambapo wadau mbalimbali wa ndani na nje nchi watapata taarifa mbalimbali kuhusu Jimbo hilo.
Uzinduzi wa Tovuti hiyo ulifanyika katika Kijiji cha Saragana wilayani  Musoma ambapo wananchi mbalimbali na  Viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya Musoma Vijijini walihudhuria.
“Badala ya kusubiri kuangalia Luninga au magazeti, Tovuti hii itasaidia shughuli mbalimbali za Jimbo ikiwemo miradi mbalimbali tunayotekeleza kuonekana katika ulimwengu mzima”, alisema Profesa Muhongo.
Aidha alisema kuwa Tovuti hiyo inarahisisha Mawasiliano kati ya Mbunge na wananchi wa Jimbo hilo kwani sasa wataweza kuuliza maswali au kutoa maoni yao moja kwa moja kuhusu jimbo husika.
Aliongeza kuwa kuonekana kwa miradi  inayotekelezwa jimboni humo, ikiwemo ya Afya, Elimu, na Kilimo kutasaidia kuvutia wafadhili mbalimbali kuendeleza miradi husika, akitolea mfano zoezi la uchangiaji fedha za   kutengeneza madawati linaloendelea sasa ambalo litawezesha madawati 8000 kutengenezwa. 
Awali Profesa Muhongo alizindua pia Mpango wa ugawaji madawati katika Jimbo hilo la Musoma Vijijini ambapo alizindulia mpango huo katika shule ya msingi Rukuba iliyopo katika kisiwa cha Rukuba ambayo ilipata madawati 100 huku zoezi hilo likiwa ni endelevu.
Alisema kuwa Jimbo hilo lina upungufu wa madawati 8000 hivyo utengenezaji wa madawati hayo unaendelea kupitia SUMA-JKT mkoani Mwanza na kwamba fedha za kutengenezea madawati zimetoka kkwa Mbunge huyo pamoja na wadau mbalimbali walioguswa na tatizo hilo.
“ Lengo letu ni kuhakikisha kuwa ndani ya miezi mitatu ijayo kuwe hakuna mtoto anayekaa chini katika shule za msingi zote 108 zilizopo jimboni humu,  na fedha hizi za utengenezaji madawati hutumwa moja kwa moja kwenye akanti ya iliyotolewa na SUMA JKT, hii yote ni katika kuhakikisha kuwa zoezi hili linafanyika kwa ufanisi,” alisema Profesa Muhongo.


No comments: