Monday, May 9, 2016

BIASHARA YA MTANDAO KUIMARISHA AFYA ZA WATANZANIA.

 Rais wa Kamouni ya Trevo Tanzania, Mark  Steven akizunumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na kuwapa zaadi washiriki wa uuzaji wa kinywaji cha Trevo hapa nchini. amesema kuwa Kampuni ya Trevo imewapa fulsa vijana wa kitanzania kuvuna fedha kutokana na juhudi zao kwa kuwa Biashara ya Trevo imeshamiri nchini na inaendelea kukita mizizi katika maeneo mbalimbali.
Amesema bidhaa ya Trevo ni maarufu duniani kote kwani  ina mchanganyiko wa matunda aina 174 ambayo kwa pamoja yanasaidia katika kuboresha afya ya mtumiaji.
Mkurugenzi wa Trevo Tanzania, David Kagoro akionesha kinywaji cha Trevo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.  amesema Kampuni  ya Trevo ambayo ina miezi 17 hivisasa nchini Tanzania imeweza kutoa kwa wananchi kiasi shilingi za kitanzania bilioni tatu na nusu ambazo ni ujira wao kutokana na mauzo waliyoyafanya kupitia biashara kwa njia ya mtandao (Network Marketing)..

Mkurugenzi huyo amesema tayari hadi sasa watu wanne wamepata fulsa ya kupata magari mapya wakiwa ni watanzania katika kipindi cha mwanzo ambapo biashara ya Trevo bado ilikuwa haijafahamika.Kushoto ni Rais wa Kamouni ya Trevo Tanzania, Mark  Steven
Rais wa Kamouni ya Trevo Tanzania, Mark  Steven  wakijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Trevo Tanzania, David Kagoro (Kulia) pamoja na Mkurugenzi wa Trevo Tanzania, Michael Ajao jijini Dar es Salaam leo.

No comments: