Friday, May 20, 2016

MWENYEKITI MJI MDOGO WA HIMO AFANIKISHA UZINDUZI WA KIKUNDI CHA MTAA WAKE WA MIEMBENI

Mwenyekiti wa Mji Mdogo wa Himo ambaye pia ni mwenyekiti wa mtaa wa Miembeni akizungumza wakati wa uzinduzi wa mfuko wa kikundi cha Miembeni kilijulikanacho kama Miembeni Uchumi Society.
Baadhi ya wananchi ambao ni wakazi wa Mtaa wa Miembeni katika mji mdog wa Himo mkoani Kilimanjaro wanaounda kikundi cha Miembeni Uchumi Society.
Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rwaichi Kaale akizungumza wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa mfuko wa Miembeni Uchumi Society.
Baadhi ya wanakikundi.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM wilaya ya Moshi Grace Mzava akizungumza wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa kikundi hicho.
Baadhi ya wanakikundi.
Mwenyekiti wa Mji Mdogo wa Himo,Hussein Jamal akitoa pesa kiasi cha Shilingi Milioni moja kama mchango wake wa kutunisha mfuko wa kikundi.
Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rwaichi Kaale akionesha hundi ya kiasi cha shilingi Milioni moja aliyotoa kwa ajili ya kutunisha mfuko wa kikundi.
Mama Kaale akikabidhi Hundi ya kiasi cha shilingi Milioni moja kwa Mwenyekiti wa mji Mdogo wa Himo.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM wilaya ya Moshi Grace Mzava akikabidhi fedha kiasi cha shilingi Milioni moja kama mchango wake katika kutunisha mfuko wa kikundi hicho.

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM wilaya ya Moshi Grace Mzava akikabidhi pikipiki mbili kwa Mwenyekiti wa kikundi cha Miembeni Uchumi Society,Nelson Gabriel ikiwa ni sehemu ya miradi iliyoanzishwa na kikundi hicho.
Mwenyekiti wa Kikundi hicho Nelson Gabriel akifurahia msaada wa pikipiki uliotolewa kwa kikindi hicho na Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Moshi,Grace Mzava.
Mwenyekiti wa Mji Mdogo wa Himo ,Hussein Jamal akikabidhi kwa Mweka hazina wa kikundi hicho Grace Silayo kiasi cha shilingi Milioni tatu zilizopatikana wakati wa uzinduzi rasmi wa mfuko wa kikundi hicho.
Wananchi katika Mtaa wa Miembeni wakiwa wamembeba juu Mwenyekiti wao Hussein Jamal kwa kubuni njia ya kuweza kuwakwamua wakazi wa mtaa huo kiuchumi.Picha na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

No comments: