Friday, May 20, 2016

KAMPUNI YA TEKNOLOJIA YA UJENZI YA PERI YAZINDULIWA HAPA NCHINI.

KAMPUNI ya Peri hapa nchini inayojihusiaha tecknolojiia ya ujenzi hapa imezinduliwa jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Mkurugenzi wa Uvumbuzi wa shirika la Nyumba nchini, Issack Peter.


Kampuni ya Peri ni ya nchini Ujerumani yenye makao makuu yake maeneo ya Makumbusho jijini Dar es Salaam 
kampuni hiyo inaweza kupunguza uharibifu wa mazingira kutokana na teknolojia wanayoitumia katika ujenzi wa Majengo marefu mbalimbali kuwa katika teknolojia yao haitumii mti kwaajili ya ujenzi.

Mkurugenzi wa Mkurugenzi wa Uvumbuzi wa shirika la Nyumba nchini (NHC), Issack Peter (katikati) Mkurugenzi wa Kampuni ya Peri, Theunis Visser  (Kushoto) na kulia Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Peri, Giuseppe Rosiello wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa kampuni ya Peri hapa nchini.





Mkurugenzi wa Mkurugenzi wa Uvumbuzi wa shirika la Nyumba nchini, Issack Peter akizungumza katika uzinduzi wa Kampuni ya Kijerumaji hapa nchini ya Peri  jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa  Shirika la nyumba hapa nchini lipo katika mpango wa kuendeleza nyumba 6000 hapa nchini kwaajili ya makazi na  Biashara  na nyumba hizo zipo za Gharama nafuu, gharama za kati pamoja na gharama za juu.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Peri, Theunis Visser akizungumza katika ufunguzi wa kampuni ya Peri jijini Dar es Salaam, amesema kuwa kampuni ya Peri ni kampuni inayo saidia katika kupunguza uharibifu wa mazingira  hasa kupunguza ukataji wa miti pia inaendeleza majengo mbalimbali.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Peri, Giuseppe Rosiello akizungumza katika uzinduzi wa kampuni ya Peri jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Mkurugenzi wa Uvumbuzi wa shirika la Nyumba nchini (NHC), Issack Peter (katikati) Mkurugenzi wa Kampuni ya Peri, Theunis Visser  (Kushoto) na kulia Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Peri, Giuseppe Rosiello wakijipongeza na kinywaji mara baada ya uzinduzi wa kampuni ya Peri hapa nchini.
Mkurugenzi wa Mkurugenzi wa Uvumbuzi wa Shirika la Nyumba nchini (NHC), Issack Peter (wa Pili kutoka kushoto)  na kushoto ni  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Peri, Giuseppe Rosiello wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wageni waliohudhuria katika uzinduzi wa kampuni hiyo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wageni wakiwa katika picha ya Pamoja katika uzinduzi wa kampuni ya teknologia ya ujenzi ya Peri jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wageni waliohudhuria uzinduzi wa kampuni ya Peri jijini Dar es Salaam.
Picha na Avila Kakingo.

No comments: