Wednesday, May 11, 2016

MATUKIO KATIKA PICHA BUNGENI DODOMA.

Baadhi ya Wabunge wa Majimbo mbalimbali wakielekea katika Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma tayari kwa vikao vya asubuhi leo 11 Mei, 2016.
Mbunge Iringa Mjini, Mhe. Mchungaji Peter Msigwa (kushoto) pamoja na Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari wakiwapungia mkono Wapiga picha (hawapo pichani wakati wakiingia Bungeni kwa ajili ya vikao vinavyoendelea mjini Dodoma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (kushoto) akifurahiua jambo pamoja na Wabunge wenzie nje ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.


Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira akiingia ndani ya Bunge kwa ajili ya vikao vya asubuhi mjini Dodoma.
Naibu Waziri, Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Mhe. Mhandisi Stella Manyanya akiwasili katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma kwa ajili ya vikao vya asubuhi vya bunge hilo.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo akijibu maswali mbalimbali ya Wabunge Bungeni mjini Dodoma.

Naibu Waziri, Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mhe. Tate William Ole-Nasha akijibu maswali mbalimbali ya Wabunge Bungeni mjini Dodoma.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akisoma bajeti ya Wizara yake mbele ya Wabunge leo 11 Mei, 2016 mjini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Uutumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (kushoto) akiteta jambo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (Mb) Bungeni mjini Dodoma.
(Picha zote na Benedict Liwenga, Dodoma)

No comments: