Monday, May 16, 2016

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA UHAULISHAJI FEDHA KWA JAMII AFRIKA

Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amefungua Mkutano wa nchi za Afrika zinazotekeleza Mpango wa Uhawilishaji Fedha kwa kusisitiza kuwa serikali ya Tanzania inatambua umuhimu wa kushirikisha wadau katika mapambano dhidi ya umaskini barani Afrika.

Mheshimiwa Samia amesema licha ya juhudi kubwa kufanywa na mataifa mbalimbali barani Afrika dhidi ya umaskini, tatizo hilo limeendelea kuwakabili wananchi hivyo kuweko kila sababu ya kubuni mbinu thabiti za kutokomeza adui huyo wa ustawi wa wananchi.Amesema kuanzishwa kwa mipango ya uhawilishaji fedha ambayo imeanza kutekelezwa na nchi mbalimbali barani Afrika katika miaka ya karibuni kutasaidia kwa kiwango kikubwa jitihada za kutokomeza umaskini.

Ameto mfano wa Tanzania kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii -TASAF - ambao umepata mafanikio makubwa katika kipindi kifupi tangu kuanza utekelezaji wa Mpango wa Uhawilishaji fedha ambapo hadi sasa zaidi ya kaya maskini Milioni Moja na Laki Moja zimeandikishwa na kuanza kupata ruzuku ya fedha kwa ajili ya kuboresha maisha na mkazo ukiwekwa katika sekta ya elimu, afya na lishe huku kaya husika zikijengewa uwezo wa kukuza shughuli za kiuchumi ili hatimaye ziweze kujitegemea.

Mapema waziri wa nchi ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora mheshimiwa Angellah Kairuki amesema mafanikio makubwa yamepatikana katika utekelezaji wa shughuli za Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF katika utambuzi, uandikishaji na utoaji wa Ruzuku kwa wakati kwa kaya za walengwa nchini kote, na kuwa changamoto chache zilizojitokeza zinafanyiwa kazi ili kuboresha zaidi Mpango huo.

Mkutano huo unaoshirikisha nchi 17 na mashirika mbalimbali ya kimataifa umeitishwa nchini Tanzania kufuatia mafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya maskini -PSSN- ambapo pia washiriki hao watapata fursa ya kutembelea kaya za walengwa ili kuona namna wanavyonufaika na huduma za mpango huo.

Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akifungua Mkutano wa Nchi za Afrika Zinazotekeleza Mipango ya Uhawilishaji Fedha katika Hotel ya Ngurdoto, Arusha, Tanzania.
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma na Utawala Bora Mheshimiwa Angella Kairuki akitoa hotuba ya kumkaribisha Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan kufungua mkutano wa Nchi za Afrika Zinazotekeleza Mipango ya Uhawilishaji Fedha katika Hotel ya Ngurdoto nje kidogo ya jiji la Arusha.
Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia (Tanzania, Kenya Uganda na Burundi) Ms Bella Bird akitoa hotuba katika Mkutano wa Nchi za Afrika Zinazotekeleza Mipango ya Uhawilishaji Fedha katika Hotel ya Ngurdoto nje kidogo ya jiji la Arusha.
Mwenyekiti wa kamati ya uongozi taifa ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF Dr. Florens Turuka akitoa maelezo ya kabla ya ufunguzi wa mkutano wa Nchi za Afrika Zinazotekeleza Mipango ya Uhawilishaji Fedha katika Hotel ya Ngurdoto nje kidogo ya jiji la Arusha.
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bwana Ladislaus Mwamanga akitoa neno la shukrani baada ya Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan kufungua Mkutano wa Nchi za Afrika Zinazotekeleza Mipango ya Uhawilishaji Fedha .

 Naibu Mwakilishi Mkazi wa UNICEF nchini Tanzania Bwana  Paul Edwards  akihutubia washiriki wa Mkutano wa Nchi za Afrika Zinazotekeleza Mipango ya Uhawilishaji Fedha .
 Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa Nchi za Afrika Zinazotekeleza Mipango ya Uhawilishaji Fedha kutoka nchi 17 barani Afrika wakisikiliza hotuba ya ufunguzi  iliyotolewa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan(hayupo pichani) Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF bwana Ladislaus Mwamanga akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari juu ya utekelezaji wa Mpango wa kunusuru Kaya maskini unaotekelezwa na serikali kupitia TASAF .
 Baadhi ya Washiriki wa mkutano wa Nchi za Afrika Zinazotekeleza Mipango ya Uhawilishaji wakiwa katika picha ya pamoja na Mkamu wa Rais Samia Suluhu Hassan(aliyeketi katikati)

 Baadhi ya Washiriki wa mkutano wa Nchi za Afrika Zinazotekeleza Mipango ya Uhawilishaji wakiwa katika picha ya pamoja na Mkamu wa Rais Samia Suluhu Hassan(aliyeketi katikati)

No comments: