Mgodi
wa Dhahabu wa Geita (GGM) kwa kushirikiana na Tume ya kupambana na Ukimwi
nchini (TACAIDS) imemteua msanii maarufu Mrisho Mpoto kuwa balozi wa kampeni ya
Kili Challenge.
Kili
Chalenge ni kampeni inayolenga kukusanya fedha kwa ajili ya kutunisha mfuko wa
mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI. Kampeni hiyo ilianzishwa miaka 15 iliyopita na
hufanyika kila mwaka kwa wadau mbalimbali kupanda mlima Kilimanjaro.Mwaka uliopita
2015 watu 39 walifanikiwa kupanda Mlima na kuchangisha fedha zaidi ya Sh
bilioni 1.2 ambazo zitagawiwa kwa Asasi
mbalimbali tarehe 20 Mwezi huu pale Hyatt Regency Dar es Salaam,Mgeni rasmi
atakuwa makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia
Suluhu Hassan.
Mrisho
Mpoto ameteuliwa kuiwakilisha na kuitangaza kampeni hii ili kusaidiana na
serikali pamoja na wadau mbalimbali ndani na nje ya Tanzania kupambana na janga
hili la Taifa. Mrisho Mpoto anakuwa Balozi mpya katika Kampeni hii kwa sababu ni
msanii mwenye ushawishi ndani ya jamii na kupitia kazi zake za kisanaa
tunaamini ataweza kuihamasisha jamii ipasavyo kuona umuhimu wa kumaliza tatizo
la VVU na UKIMWI hasa katika masuala ya unyanyapaa.
Kwa
mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS, Dkt. Fatma Mrisho, “Inakadiriwa kuwa
watu milioni 1.6 nchini wanaishi na VVU & Ukimwi. Ugonjwa huo umewaathiri
zaidi vijana na watoto yatima zaidi ya milioni 1.3. Tunahitaji kubadilisha hali
hii. TACAIDS kwa kushirikiana na Mgodi
wa Dhahabu wa Geita (GGM) na wadau wengine kwa kupitia mpango huu wa
Kilimanjaro Challenge tunapenda kutoa mchango na ushirikiano wetu kwa Taifa ili
kutunisha mfuko utakaowezesha kuendeleza mapambano dhidi ya ugonjwa huo”.
Napenda
kuupongeza Mgodi wa Dhahabu wa Geita kwa
kushirikiana na wadau wengine kwa kuamua kwa dhati kwa kipindi cha miaka 15
kuwekeza katika mradi huu kwa kuuwezesha kuwa mradi wa kitaifa na si wa GGM,
hivyo pamoja na balozi wetu hivi sasa Mrisho Mpoto, tuungane nao ili kuongeza chachu kwa wadau
wengine kujitokeza kuongeza nguvu katika mapambano dhidi ya janga hili”
alisisitiza Dkt Fatma Mrisho.
“Kwa
kushirikiana na Mpoto tuna matumaini ya kujenga timu imara yenye hamasa ya
kupambana na janga hili. Tunatoa wito kwa makampuni na wadau mbalimbali wa
ndani na nje ya nchi, wajitokeza ili tushirikiane kutunisha mfuko wa
Kilimanjaro Challenge na mwishowe kufikia ndoto au malengo ya nchi yetu ya
kuhakikisha tunakuwa na kizazi kisicho na maambukizi ya VVU na Ukimwi” alisema
Bw. Simon Shayo Makamu wa Raisi wa miradi endelevu wa Anglogold Ashanti (GGM).
Shayo
alisisitiza kwa kusema “GGM iko tayari kushirikiana na wadau wengine wenye nia
ya dhati, kuungana pamoja kupitia mfuko wa Kili Challenge katika kuhakikisha
maambukizi haya hayaendelei kuleta athari kwa jamii yetu kwa sababu serikali
yenyewe haitaweza kutokomeza tatizo hili”.
Naye
Balozi mpya wa Kili challenge, Mrisho Mpoto alisema; “Nashukuru sana kwa kupata
fursa hii ya kuweza kutoa mchango wangu katika kuisaidia jamii kuepukana na
janga hili. Changamoto kubwa inayotokana na janga hili la VVU &UKIMWI ni
ongezeko la maambukizi ya VVU kwa vijana ambao ndio nguvu kazi ya Taifa letu
pasipo kila mmoja wetu kujitoa kwa dhati hatutalimaliza janga hili. Napenda
kuwaambia watanzania wenzangu kwamba tushirikiane kwa pamoja ili tuangamize
janga hili”
Pamoja
na hatua kubwa zilizopigwa na serikali ikishirikiana na wadau, kumekuwapo na
ongezeko la maelfu ya watoto yatima wanaohitaji misaada baada ya wazazi wao
kufariki, wajane wasiokuwa na kipato, pamoja na wazee wanaolazimika kuwalea
wajukuu walioachwa na watoto wao ambao walifariki kutokana kwa ugonjwa huo
alisisitiza Mkurugenzi mtendaji wa TACAIDS.
Kilimanjaro
Challenge ni mradi unaolenga kutoa elimu kwa jamii kuhusu ugonjwa wa Ukimwi na
Virusi Vya Ukimwi (VVU). Pia inalenga kuchangisha fedha ili kujenga timu imara
itakayoendeleza mapambano dhidi ya ugonjwa huo.Ili
kuweza kuwa sehemu yawatakaopanda Mlima Kilimanjaro, kwa kupitia Kili Challenge
mwaka huu, uwe Mtu binafsi au kupitia shirika kulipia wafanyakazi wake kupanda
mlima mchango ni $5,000 tu ambazo zitalipia gharama za upandaji na kuchangia
mfuko wa Kili Challenge.
Kilimanjaro
Challenge imebakia kuwa chombo muhimu kinachoshirikiana na taasisi za nje na
ndani ya nchi katika mapambano dhidi ya VVU&Ukimwi kwa jamii ya Kitanzania
na dunia kwa ujumla ili kuwapa matumaini ya kuhakikisha jamii inabaki bila
kuathiriwa na ugonjwa huo katika miaka ijayo
Mpango
huo pia unalenga kuisaidia Serikali kukabiliana na VVU & Ukimwi pamoja na kutoa nafasi kwa watalii wa ndani kuupanda
mlima Kilimanjaro.
KUHUSU Kili Challenge:
Kwa
maelezo zaidi tembelea tovuti ya www.anglogoldashanti.com
na www.geitakilichallenge.com
No comments:
Post a Comment