Monday, May 30, 2016

19 WATAJWA KUSHIRIKI SHINDANO LA MAMA SHUJAA WA CHAKULA MSIMU WA TANO 2016


Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Oxfam Tanzania Jane Foster(aliyesimama) akiwapongeza washiriki wote waliojaza fomu za kushiriki shindano la mama shujaa wa chakula msimu wa tano 2016 kutoka mikoa mbalimbali nchini. 
Meneja utetezi kutoka Oxfam Tanzania Eluka Kibona akitoa maelezo kuhusu Shindano la Mama Shujaa wa Chakula kuwa linaendeshwa Tanzania,Nigeria na Ethiopia ambapo alisema lengo la shindano ni kutambua mchango wa wanawake katika mapambano dhidi ya umasikini na kuleta uhakika wa chakula.
Afisa uhakiki wa ubora kutoka TBS Stela Mroso akisisitiza jambo kuhusu ushirikiano wao kama Shirika la Viwango la TBS na Oxfam Tanzania kuhakikisha wanatetea wanawake.
Mwakilishi kutoka Wizara ya Kilimo Paskarina Kayuma akitoa Shukurani kwa Shirika la Oxfam Tanzania kwa kuendelea kuwanyanyua wanawake katika kilimo na amewaomba juhudi hizo ziendelee.
Miongoni mwa majaji Edna Kiogwe mshiriki wa mama Shujaa wa Chakula msimu uliopita(Kulia) pamoja na Fredy Njeje kutoka Blogs za Mikoa (Kushoto) wakielezea namna usaili ulivyofanyika mpaka kuwapata washiriki 19 katika shindano la Mama Shujaa wa Chakula msimu wa tano kwa mwaka 2016.
Aliyekuwa mshiriki wa shindano la Mama Shujaa wa Chakula msimu uliopita Ester Kulwa akionesha kanda zote ambazo washiriki wametokea.
Mabalozi wa Chakula na Kampeni ya Grow inayoendeshwa na Shirika la Oxfam kwa upande wa Tanzania Shamim Mwasha ambaye pia ni Fashion Blogger(wa kwanza kushoto), Jacob Stephen 'JB' Msanii Maarufu wa Bongo Movie(wa katikati) na Khadija Mwanamboka wakitangaza majina 19 ya washiriki wa shindano la Mama shujaa wa chakula 2016 msimu wa tano.
Baadhi ya wageni wakiwa katika Hafla fupi ya kutangaza majina 19 ya washiriki katika shindano la Mama shujaa wa chakula msimu wa tano 2016.
Mshindi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 linaloendeshwa na Shirika la Kimataifa la Oxfam Tanzania kutoka Morogoro Caroline Chelele akizungumza jambo katika hafla hiyo.
Aliyekuwa Mshiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula Pili Kashinje akizungumza jambo wakati wa Hafla fupi ya kutangaza washiriki shindano la Mama shujaa wa chakula msimu wa tano 2016.
Suhaila Thawer ambaye ni 'Public Forum Officer' kutoka Shirika la Oxfam Tanzania akitoa neno la Shukurani.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Oxfam Tanzania Jane Foster (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Majaji,Wafanyakazi wa Oxfam pamoja na Mabalozi wa Chakula na Kampeni ya Grow.
Waliosaidia katika kupitia Fomu za Mama shujaa wa Chakula kwa hatua ya Mwanzo kutoka Taasisi mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Oxfam Tanzania Jane Foster (wa saba kutoka kulia).

Hatimaye 19 watajwa kushiriki katika shindano la Mama Shujaa wa Chakula Msimu wa tano kwa mwaka huu 2016, ambapo fomu 3000 zilizotumwa na wakulima wanawake kote nchini, fomu 1795 zilipitiwa na kuwapata washiriki hao ambao wataanza kutembelewa mmoja mmoja ili kuhakiki iwapo kile walichokijaza kwenye fomu kinaoana na hali halisi. Mashindano ya Mama Shujaa wa Chakula 2016, linatarajiwa kufanyika katika kijiji cha Enguiki kilichopo Monduli mkoani Arusha, kuanzia Septemba 25 hadi Oktoba 16 na kurushwa katika Runinga ya ITV.

Akizungumza wakati wa kutangaza majina hayo, mmoja wa majaji wa shindano hilo Jacob Stephen ‘JB’ ambaye ni muigizaji maarufu wa Filamu Tanzania alisema katika uchambuzi wa fomu hizo walikuwa ni wanawake wakulima ambao wanaelimu ya juu na baadhi ya viongozi wa kisiasa na wale wadogo wadogo. 

Mkurugenzi Mkazi wa Oxfam Tanzania Jane Foster alisema shindano hilo limeanza kuendeshwa kuanzia mwaka 2011 na sasa ni msimu wa tano na limefanikiwa kuwaunganisha wanawake wakulima wadogo wadogo ambao ni asilimia 70 ya wanawake nchini. Alisema majaji wamefanya kazi ya kuchambua fomu hizo na kuwapata washiriki ambao watakuwa mabalozi wa kuwasilishwa matakwa yao ili changamoto zilizopo zitatuliwe. 

Alisema majaji wamefanya kazi ya kuchambua fomu hizo na kuwapata washiriki ambao watakuwa mabalozi wa kuwasilishwa matakwa yao ili changamoto zilizopo zitatuliwe. Aliongeza kuwa shindano la mama shujaa wa Chakula linaendeshwa katika nchi tatu Afrika ikiwemo Nigeria, Ethiopia na Tanzania. Ambapo Tanzania wamepita katika mikoa mbalimbali na kukusanya wanawake wakulima wadogo wadogo ambao tunaamini kwa kuwa pamoja wanaweza kupaza sauti kwa watunga sera kuhusu changamoto wanazokutana nazo. 

Afisa Uhakiki wa Ubora TBS, Stela Mroso alisema shirika la viwango nchini liliungana na Oxfam mwaka jana ili kuhakikisha wanawaleta wanawake pamoja na kutoa elimu zaidi kuhusu kilimo chenye ubora na mazao yanayoweza kuwa na viwango vya kimataifa. Alisema bila viwango wanawake hawawezi kufanya biashara, huku akitoa wito kwao kujitokeza ili kuangalia ubora wa mazao wanayozalisha. Aliongeza kuwa asilimia 80 ya wanawake nchini wanajishughulisha na Kilimo kwa hiyo ni muhimu chakula kinachozalishwa kiwe katika ubora na afya pia kiweze kuzaliswa Kimataifa. 

Washiriki wa Mama Shujaa wa Chakula 2016 kuwa ni Betty Nyange (62) Mkoa wa Morogoro, Monica Charles Mduwile (44) Mkoa wa Dodoma, Neema Gilbet Uhagile (29) Mkoa wa Njombe, Mary Christopher Lyatuu (29) Mkoa wa Arusha, Loyce Daudi Mazengo (39) Mkoa wa Singida, Anjela Chogsasi Mswete (48) Mkoa wa Iringa, Lucina Sylivester Assey (54) Mkoa wa Shinyanga, Marta Massesa Nyalama (50) Mkoa wa Kaskazini Unguja, Christina Machumu (42) Mkoa wa Mara, Happiness Paulo Raulent (35) Mkoa wa Kagera. Mary Bony Soko (42) Mkoa wa Ruvuma, Mary Ramadhani Mwiru (39) Mkoa wa Kilimanjaro, Mwanaid Alli Abdalla (53) Mkoa wa Mjini Magharibi, Maria Alfred Mbuya (43) Mkoa wa Mbeya, Eliza Richard Mwansasu (30) Mkoa wa Rukwa, Mwajibu Hasani Binamu (46) Mkoa wa Mtwara, Eva Haprisoni Sikaponda (40) Mkoa wa Songwe, Hidaya Said Musa (40) Mkoa wa Tanga na Mwasiti Salim Mazuri (40) Mkoa wa Dar es salaam Wilaya ya Kinondoni.

No comments: