Saturday, April 23, 2016

WIZARA YA UJENZI ,UCHUKUZI NA MAWASILIANO YAENDELEA NA MCHAKATO WA UKUSANYAJI MAONI JUU YA UBORESHAJI SERA YA TAIFA YA (TEHAMA)MKOANI MBEYA


Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia masuala ya Simu katika Wizara ya Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano Ndugu John Mwera akizungumza na wanahabari katika viwanja vya Chuo Cha Uhasibu jijini Mbeya( TIA ) juu ya zoezi la uchukuaji maoni na ushauri kwa wadau katika kuboresha sera ya Taifa ya Habari ,Teknologia na Mawasiliano (TEHAMA). 
Mhandisi Enock Mpenzwa Idara Mawasiliano toka Wizara ya Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Forest jijini Mbeya waliofika kwa ajili ya zoezi la utoaji maoni na ushauri juu ya uboreshaji wa sera mpya ya Taifa ya TEHAMA katika viwanja vya Chuo Cha Uhasibu TIA jijini Mbeya April 22, 2015. 
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Forest jijini Mbeya wakiwa katika foleni ya kujiandikisha ili kutoa maoni yao na ushauri juu ya uboreshaji wa sera ya Taifa ya TEHAMA,zoezi ambalo limefanyika katika viwanja vya Chuo Cha Uhasibu Mbeya (TIA) April 22 ,2015.
Mwanafunzi shule ya sekondari Forest jijini Mbeya Mariam Jordan akijiandikisha kwa ajili ya kutoa maoni yake katika zoezi la uboreshaji wa sera ya Taifa ya TEHAMA zoezi ambalo limeratibiwa na Wizara ya Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano ,katika viwanja vya Chuo Cha Uhasibu Jijini Mbeya (TIA).
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Cha Uhasibu Jijini (TIA)wakijibu baadhi ya Maswali kama sehemu ya ukusanyaji maoni ili kuboresha sera ya TEHAMA . 

Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Cha Uhasibu Jijini (TIA) na wadau mbalimbali kutoka Mkoani Mbeya wakijibu baadhi ya Maswali kama sehemu ya ukusanyaji maoni ili kuboresha sera ya TEHAMA .

Na Emanuel Madafa,Mbeya (Jamiimojablog)

Wizara ya Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano imetoa wito kwa wananchi na wadau mbalimbali kuendelea kutoa maoni na mapendekezo ili yatumike kuboresha Sera mpya ya Taifa ya Habari Teknologia ya Mawasiliano(TEHAMA) ya (2016) ili kuisaidia serikali kutatua changamoto za upatikanaji wa habari na mawasiliano katika jamii 

Wito huo umetolewa jijini Mbeya na Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia maswala ya simu katika Wizara ya Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano Ndugu John Mwera wakati wa zoezi la uchukuaji maoni lililofanyika katika viwanja vya chuo cha Uhasibu (TIA) jijini Mbeya .

Amesema Teknolojia ya habari na mawasiliano hapa nchini imekuwa ikikua kwa kasi kubwa katika kipindi cha miaka kumi tangu serikali ilipotunga sera kwa mara ya kwanza mwaka 2003.

Amesema hali hiyo imechangia kuwepo kwa miundombinu ya huduma za mawasiliano kila mahala na kufanya matumizi kuwa makubwa ambapo zaidi ya watu milioni 39 wanatumia mawasiliano ya simu hivyo kufanya kuibuka kwa changamoto mbalimbali katika sekta hiyo.

Amesema ili kufahamu changamoto wanazo kutananazo wananchi pamoja na mtizamo wao katika utumiaji wa mawasiliano, wizara hiyo imeamua kuweka utaratibu wa kuweka vituo vya kukuza ubunifu katika jamii katika kila mkoa ambapo kila mwananchi anakuwa huru katika kutoa maoni yao na ushauri ili kuisaidia serikali katika kupanga mikakati ya kuweza kuzitatua changomoto hizo. 

“Huwezi kukaa ofisini ukatunga sera ambazo haziwahusu mwananchi wa kawaida hivyo lazima twende kwa wananchi na kujua wanahitaji nini ili kutunga sera na kuweza kuzitatua”Alisema Mwela 



Aidha amesema kuwa kila maoni yanayotolewa na wananchi serikali inayathamini katika kuweza kutoa muelekeo wa sekta ya mawasiliano kwani sekta hiyo bado inamchango mkubwa sana katika kutoa huduma mbalimbali kwa wananchi.

Hata hivyo amesema bado wizara inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni elimu ndogo kwa waanchi juu ya utunzaji wa miundombinu ya sekta ya mawasiliano hususani mkongo wa taifa sanjali na wizi wa mafuta kwenye minara ya simu hivyo amewataka wananchi kuwa walinzi wa miundombinu hiyo ili kuendelea kukuza sekta hiyo sanjali na kulahisisha upatikanaji wa huduma kwa jamii.

Amesema zoezi hilo la uchukuaji maoni kwa wananchi juu ya uboreshaji wa sera ya TEHAMA itaendelea inchi nzima katika mikoa yote ya Tanzania bara na Visiwani.

No comments: