Mshambuliaji Ramadhani Madebe wa Uchukuzi SC akikokota mpira katikati ya uwanja, huku Mohamed Salum wa GGM akimsogelea. Timu hizo zimetoka satre ya bao 1-1.
Issack Ibrahim (mwenye mpira) akimtoa Fernand Makanga wa GGM akimzuia asilete madhara. Timu zilitoka sare 1-1.
Mshambuliaji Oswald Binamungu wa GGM akitafuta mbinu za kumtoka Ally Poloto wa Uchukuzi SC. Timu hizo zilitoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1.
Scholastica Halisi wa Uchukuzi SC akimaliza mshindi wa tatu wa mbio za marathoni kwa kutumia muda wa 0:49.21.
Ramadhani Mwalongo wa Uchukuzi akimalizia mbio za marathoni kwa wanaume na kuibuka mshindi wa tatu kwa kutumia muda wa 0.48:17.
Ally Zongo wa Uchukuzi SC (kushoto) akiokota karata dhidi ya Kelvin Gadi wa TPDC.
Mayasa Hamidu (C) wa Uchukuzi SC akiangalia wa kumrushia mpira huku Nathereth Mwanjala (WA) wa Tanesco akisogea kumuwahi . Uchukuzi aliibuka washindi kwa magoli 31-13.
Prisca Ferdinand wa Uchukuzi SC (kulia) akilamba karata mbele ya mpinzani wake Theodora Stanslaus wa Ujenzi katika mashindano ya Mei Mosi.
Na Mwandishi Wetu Dodoma
TIMU za mchezo wa netiboli za CDA Dodoma na Uchukuzi SC jana ziliendeleza
ubabe kwa kuwafunga wapinzani wao bila huruma kwenye mashindano ya Mei
Mosi yanayoendelea kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
CDA Dodoma inayoundwa na wachezaji wazoefu iliwafunga TPDC kwa magoli
38-12. Washindi walikwenda mapumziko wakiwa mbele kwa magoli 21-6.
Nao wadada machachari wa Uchukuzi SC wakiongozwa na kocha wao maarufu,
Judith Ilunda waliwafunga Tanesco kwa magoli 31-13. Hadi mapumziko washindi
walikuwa mbele kwa magoli 19-5.
Wafungaji mahiri wa Uchukuzi SC, Matalena Mhagama alipachika magoli 17 na
Grace Mwasote magoli 14, huku Caltace Monampo wa Tanesco alifunga matano
na mwenzake Sandra Mfaume magoli nane.
Katika mchezo wa soka, timu ya Uchukuzi SC iliwahenyesha Geita Gold Mine
(GGM) na kutoka sare ya bao 1-1. GGM ndio walioanza kupata bao dakika ya 33
kwa mshambuliaji wake Oswald Binamungu aliunganisha krosi ya Quentin
George, na Ramadhani Madebe aliyekuwa akihaha uwanja mzima kusaka bao
aliisawazishia Uchukuzi katika dakika za nyongeza.
Katika mchezo mwingine wa soka, timu ya Ukaguzi waliwachapa wenyeji CDA
kwa magoli 4-1. Victor Ngalawa ndio alikuwa wa kwanza kuandika bao katika
dakika ya sita, na Pemsi Msenga alisawazisha katika dakika ya 18.
Ukaguzi waliendelea kuwashambulia CDA na Deo Masanja (mchezaji wa zamani
wa Simba SC) aliongeza bao la pili katika dakika ya 33, huku Ally Mpondo
alifunga la tatu dakika ya 82 na Yahya Salum alifungala nne dakika ya 89.
Katika mchezo wa riadha mbio za marathoni wanaume ameshinda Atson
Mbughuni wa Tamisemi kamaliza kwa 0:35.32, wapili ni Lazaro Lugano wa
tanesco katumia 0:42.45 na watatu ni Ramadhani Wakilongo wa Uchukuzi SC
katumia 0:48.17.
Upande wa wanawake riadha alishinda Stella Mroso wa TPDC kwa 0:42.36, huku
wa pili ni Beltila Genadius wa Tamisemi kwa 0:44.00 na watatu ni Scholastica
Halisi wa Uchukuzi kwa 0:49:21.
Katika michezo ya jadi kwa upande wa karata wanawake bingwa ni Sheila
Mwihava wa Tanesco alimshinda Mayasa Kambi wa UDOM katika fainali na
mshindi wa tatu ni Bupe Munisi wa Mawasiliano, kwa upande wa wanaume
ametwaa ubingwa Haji Chilo wa UDOM, huku wa pili ni Omari Said wa Tanesco
na watatu ni Ally Zongo wa Uchukuzi SC
No comments:
Post a Comment