Mmoja ya majaji wa shindano la Airtel Trace Music Stars ambaye ni mtangazaji wa TV mahiri, Mwanamuzi, Mwigizaji na mfanya biashara , Jokate Urban Mwegelo (wa kwanza kulia) akiongea na jopo la majaji wenzake wakati wakichagua vijana waliofudhu kuingia kumi bora katika wiki hii. Zoezi hili lilifanyika katika ofisi za makao makuu ya Airtel Tanzania zilizoko Moroco jijini Dar es Saalam Jana
Mmoja ya majaji wa shindano la Airtel Trace Music Stars mtunzi wa nyimbo na mwaimu wa Muziki Anthony Joseph Namata“JOETT (aliyesimama) akisoma na kupigia maoni ya majaji wenzake juu ya washiriki waliofanya vizuri katika shindano la Airtel Trace Music Stars na kuingia katika kumi bora ya wiki hii wakati majaji hao walipokutana kufanya uchaguzi.
Mmoja ya majaji wa shindano la Airtel Trace Music Stars mtunzi wa nyimbo na mwaimu wa Muziki Anthony Joseph Namata“JOETT (kulia) akitoa hoja kwa jopo la majaji wenzake wakati wakichagua vijana waliofudhu kuingia kumi bora katika wiki hii. Zoezi hili lilifanyika katika ofisi za makao makuu ya Airtel Tanzania zilizoko Moroco jijini Dar es Saalam Jana. Pichani ni mtengenezaji wa Muziki na mfanyabiashara Luciano Gadie Tsere (katikati) na Lucy T. Ngongoseke, mratibu wa Airtel Trace Music Stars.
Washiriki 10 waingia ndani ya kumi bora ya wiki ya shindano la Airtel Trace Music Stars
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Leo imetangaza washiriki kumi bora wa wiki wa shindano kubwa barani Afika lijulikanallo Airtel Trace Music Stars lililolizinduliwa mwanzoni mwa mwezi wa pili na kuwapatia fursa vijana kuonyesha vipaji vyao.
Kabla ya kutangaza washindi hao Jopo la majaji linaloshirikisha wasanii na wataalamu wa muziki akiwemo mtangazaji wa TV mahiri, Mwanamuzi, Mwigizaji na msanii aliyejikita katika maeneo mengi, Jokate Urban Mwegelo, mtunzi wa nyimbo na mwaimu wa Muziki Anthony Joseph Namata“JOETT pamoja na mtengenezaji wa Muziki na mfanyabiashara Luciano Gadie Tsere likikaa mwishoni mwa wiki na kuchagua waimbaji 10 bora kati ya vijana walioweza kushiriki mpaka sasa.
Akitangaza baadhi ya vijana waliioingia katika kumi bora , Jaji Anthony Joseph Namata“JOETT alisema “moja kati ya vigezo vilivyotumika kuwapata hawa walioingia kumi bora ni pamoja na uwezo wao wa kuimba pamoja na sauti lakini pia idadi ya kura anazozipata kutoka kwa wasikilizaji.
Hivyo basi napenda kuchukua fulsa hii kutangaza vijana waliofanikiwa kuingia katika kumi bora ambao ni pamoja na Teddy Benedict Code 55210241, Beny Sule Code 55210243, Eddy Zone (Jack) Code 55210245, Anneth Stanley Code 55210248, Sarah Code 55210249, Nicole Grey Code 55210253, Yvone Masai Code 55210254, Adili Kwezi Code 55210115, Anneth Komba Code 552101256 , David Benson Mahenge Code 55210244”
Kwa upande wake Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando alisema “Tunafurahi kuona vijana wengi wamejitokeza kushiriki na kuonyesha vipaji vyao kwa mwaka huu, natoa wito kwa vijana kuendelea kushiriki kwani mashindano bado yanaendelea.
Sambamba na hilo tunawaomba watanzania wawapigie kura washiriki wanaowapenda pamoja na vijana hawa ili waweze kuendelea kutetea nafasi zao na hatimae kuingia kwenye tano bora na kisha kupenya kwenye fainali za kitaifa zitakazofanyika hapa jijini Dar es saalam mwishoni mwa mwezi Mei”.
‘Ili kupiga kura kwa mshiriki unaempenda unatakiwa kupiga 0901002233 Kisha kuingiza code namba ya mshiriki au tuma SMS yenye code ya namba ya mshiriki kwenda namba 15594” aliongeza Mmbando.
Huu ni msimu wa pili wa Shindano la Airtel Trace Music Stars ambapo sasa shindano hili lipo katika hatua kitaifa, fainali za taifa zinategemea kufanyika 20 Mei 2016 ambapo mshindi wa kwanza atajishindia shilingi million 50, pamoja na kupata nafasi ya kwenda kushiriki katika mashindano ya taifa mwezi Juni Lagos nchini Nigeria. Mshindi wa pili ataondoka na shilingi million 5 na watatu shilingi milioni 2 Ili kushiriki piga namba 0901002233.rekodi wimbo wako sasa .
No comments:
Post a Comment