Wafanyakazi
wa Airtel katika mikoa ya Mwanza, Arusha, Dodoma, Mbeya na Morogoro leo
wameingia katika mitaa mbalimbali katika mikoa yao kuitambulisha huduma
mpya ya Airtel Jipimie Yatosha yako kwa wateja na kutoa elimu jinsi ya
kufurahia uhuru wa kutengeneza vifurushi vinavyokidhi mahitaji yao
Zoezi
hili limefanyika jana katika mkoa wa Dar es salaam ambapo wafanyakazi
wa Airtel Makao makuu waliweza kutembelia maeneo mbalimbali na kutoa
elimu hiyo, halikadhalika timu ya Airtel imefikia wateja wake kupitia
vyombo vya habari mbalimbali ikiwemo radio, Tv na mitandao ya kijamii
kwa lengo la kuwahabarisha wateja na watanzania kwa ujumla juu ya huduma
hiii ya kipekee, kibunifu na ya kwanza nchini Tanzania inayomuwezesha
wateja kununua kifurushi cha muda wa maongezi tu, au kuchanganya
kifurushi cha muda wa maongezi na MB za intaneti au Muda wa Maongezi na
SMS lakini pia bado wanaweza kupata vifurushi vyote yaani muda wa
maongezi zaidi, SMS zaidi na MB zaidi. Vifurushi hivi vinapatikana kwa
siku, wiki au mwezi
Ili kujiunga na kufurushi cha Airtel jipimie yatosha yako mteja anatakiwa kupiga *149*99# kisha kufata maelekezo.
Wafanyakazi
wa Airtel Mkoani Mwanza wakitoa elimu kwa wakazi Mwanza mjini na
wafanyabiasharaa waendesha Bodaboda kuhusu huduma mpya ya kifurushi cha
Airtel Yatosha kijulikanacho kama “Jipimie Yatosha Yako” kitakachompatia
uhuru mteja kutengeneza na kununua kifurushi kinachokidhi mahitaji
yake.
Wafanyakazi
wa Airtel Mkoani Mwanza wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuingia
mtaani kukutana na wateja na kuitambulisha huduma mpya ya kibunifu ya
Airtel jipimie yatosha yako itakayowawezesha wateja kujitengenezea
vifurushi vya yatosha wanavyovitaka
Mfanyakazi
wa Airtel Dodoma Abdul Hassn akiongea na mfanyakazi wa saloon katika
maeneo ya Dodoma Sokoni kuhusu huduma mpya ya kifurushi cha Airtel
Yatosha kijulikanacho kama “Jipimie Yatosha Yako” kitakachompatia uhuru
mteja kutengeneza na kununua kifurushi kinachokidhi mahitaji yake.
Afisa
mauzo wa Airtel Dodoma Baraka Ndelele akitoa elimu kwa muuza genge
katika maeneo ya Dodoma mjini juu ya huduma mpya ya kifurushi cha Airtel
Yatosha kijulikanacho kama “Jipimie Yatosha Yako” kitakachompatia uhuru
mteja kutengeneza na kununua kifurushi kinachokidhi mahitaji yake.
Wafanyakazi
wa Airtel Mkoani Mbeya wakiitambulisha huduma mpya ya Airtel Jipimie
Yatosha yako kwa wateja mtaani na kutoa elimu jinsi ya kujitengenezea na
kununua kifurushi kinachokidhi mahitaji yao
Afisa
masoko wa Airtel Bi Aminata Keita akimuelekeza mteja katika mkoa wa
Morogoro jinsi ya kujitengenezea kifurushi chake kupita huduma ya
“Jipimie Yatosha Yako”
Wafanyakazi
wa Airtel Mkoani Morogoro wakishuka kutoka kwenye basi kwenda kukutana
na wateja katika maeneo yao ya kazi ili kutambulisha huduma mpya ya
kibunifu ya Airtel jipimie yatosha yako itakayowawezesha wateja
kutengeneza vifurushi vya yatosha wanavyovitaka
Meneja
Uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando akifanya mahojiano na Jembe
radio mkoani Mwanza na kutoa elimu kwa wasikilizaji wa vipindi vyake juu
ya huduma mpya ya kibunifu ya Airtel jipimie yatosha yako
itakayowawezesha wateja kutengeneza vifurushi vya yatosha wanavyovitaka
Wafanyakazi
wa Airtel mkoani Arusha wakiongea na wateja sokoni na kutoa elimu
jkuhusu huduma mpya ya kifurushi cha Airtel Yatosha kijulikanacho kama
“Jipimie Yatosha Yako” kitakachompatia uhuru mteja kutengeneza na
kununua kifurushi kinachokidhi mahitaji yake.
No comments:
Post a Comment