Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA), Dominic Rwekaza (pichani)
akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa
majukumu ya wakala huo kwa mwaka wa
fedha 2015/2015 mbele ya Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini na watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini (hawapo pichani)
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA), Dominic Rwekaza (mbele)
akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa
majukumu ya wakala huo kwa mwaka wa
fedha 2015/2015 mbele ya Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini pamoja na watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini.
Sehemu
ya wajumbe wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini pamoja na watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini wakifuatilia kwa
makini taarifa utekelezaji wa majukumu
ya Chuo cha Madini Dodoma (MRI) kwa
mwaka wa fedha 2015/2016, iliyokuwa inawasilishwa na Kaimu Mkuu wa Chuo hicho,
Musa Magufuli (hayupo pichani)
Sehemu
ya maofisa kutoka Wizara ya Nishati na Madini na Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA)
wakifuatilia kwa makini taarifa
mbalimbali zilizokuwa zinawasilishwa katika kikao hicho.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) Profesa Abdulkarim Mruma
akisisitiza jambo katika kikao hicho.
Naibu
Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (kushoto) na Kaimu Kamishna
wa Madini Nchini Mhandisi Ally Samaje (kulia) wakifuatilia kwa makini taarifa
mbalimbali zilizokuwa zinawasilishwa katika kikao hicho.
Kaimu
Mkuu wa Chuo cha Madini Dodoma (MRI) Musa Magufuli (pichani) akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya chuo
hicho kwa mwaka wa fedha 2015/2016, mbele ya
wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini na watendaji
wa Wizara ya Nishati na Madini (hawapo
pichani).
Naibu
Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani akifafanua jambo katika kikao
hicho.
TMAA
yang’ara katika sekta ya madini
Kamati
ya Bunge yaipongeza
Yatakiwa
kuongezewa fedha zaidi
Na
Greyson Mwase, Dar es Salaam
Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini hivi karibuni iliupongeza Wakala wa Ukaguzi wa Madini Nchini (TMAA) kwa kazi nzuri ya kudhibiti madini
yanayotoroshwa nje ya nchini
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wajumbe wa
kamati hiyo mara baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya wakala
huo kwa kipindi cha mwaka wa fedha
2015/2016, walisema kuwa wakala umechangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la mapato
katika sekta ya madini na kuitaka serikali kuuwezesha zaidi ili uweze kuzalisha
zaidi na hivyo kuwa na mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa nchi kwa
kupitia sekta ya madini.
Mjumbe
wa kamati hiyo, Suzan Kiwanga alisema kuwa TMAA ina uwezo mkubwa wa kufanya
kazi ya kudhibiti madini yanayotoroshwa nje ya nchi kupitia
wataalam wake walioko migodini na
viwanja vya ndege, hivyo ni vyema
wakawezeshwa ili kufanya kazi hiyo kwa
bidii na uaminifu mkubwa.
“Kulingana
na ripoti yao, TMAA imefanya kazi kubwa
ya kuokoa mabilioni ya shilingi kupitia
ukamataji wa madini yaliyokuwa yanatoroshwa nje ya nchi, kazi waliyoifanya ni kubwa yenye kuhitaji uaminifu mkubwa, hivyo wakiwezeshwa zaidi wana uwezo wa
kufanya vizuri zaidi,” alisema Kiwanga
Naye
mjumbe mwingine wa kamati hiyo, Ikupa
Alex aliongeza kuwa wahalifu
wanaokamatwa na TMAA wanatakiwa kufikishwa katika vyombo vya sheria
na kutozwa faini kubwa ili
iwe fundisho wa watoroshaji wengine.
“
Huu wakala ndio unaowezesha Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA) kubaini
kodi inayostahili kulipwa na makampuni yanayojishughulisha na utafutaji na uchimbaji
wa madini nchini, rai yangu ni wakala huu kuwezeshwa zaidi katika nyanja zote
ikiwamo rasilimali fedha na rasilimali watu ili uweze kufanya kwa ufanisi zaidi,” alisema Alex.
Awali akielezea
mafanikio ya TMAA
tangu kuanzishwa kwake Mtendaji Mkuu wa wakala huo, Dominic Rwekaza alisema kwa kipindi cha mwaka 2009 hadi Januari 2016, kampuni
mbalimbali zimelipa jumla ya Shilingi bilioni 680.5 kama kodi ya mapato.
Alifafanua kampuni hizo kuwa ni pamoja na Geita Gold Mining
Limited iliyolipa jumla ya Shilingi bilioni 502.7 tangu kampuni hiyo ilipoanza
kulipa kodi ya mapato mwaka 2009; Resolute Tanzania Limited iliyolipa kodi ya
mapato kiasi cha Shilingi bilioni 100.4 katika kipindi cha mwaka 2010 hadi 2013
na Mgodi wa Dhahabu wa Tulawaka uliolipa Shilingi
bilioni 77.4 kama kodi ya mapato mwaka 2012.
Aliongeza kuwa mafanikio mengine yaliyopatikana ni pamoja
na kuongezeka kwa malipo ya mrabaha kutokana na madini ya ujenzi na
viwandani baada ya kufanyika kwa ukaguzi ambao umewezesha kiasi cha Shilingi bilioni 14 kulipwa kama
mrabaha katika kipindi cha Juni 2011 hadi Januari 2016.
Alisema malipo hayo yametokana na uzalishaji wa jumla ya tani
milioni 33.6 za madini ya ujenzi na viwandani yenye thamani ya Shilingi bilioni
465.7 kulingana na uhakiki uliofanywa na Wakala.
Aliendelea kueleza kuwa wakala ulichangia kwa uongezeko la malipo ya mrabaha kutokana na shughuli za uchenjuaji wa marudio
kwa kutumia teknolojia ya vat leaching ambapo kiasi cha shilingi bilioni 7.5 kililipwa kama mrabaha katika kipindi cha Julai 2012
hadi Januari 2016.
Alifafanua kuwa malipo hayo yalitokana na uzalishaji na
mauzo ya dhahabu kutoka kwa wazalishaji wanaotumia teknolojia ya “vat leaching” katika mikoa ya Mwanza,
Geita na Mbeya ambapo kulikuwa na jumla ya kilo 3,046 za dhahabu zenye thamani
ya Shilingi bilioni 179.8 kulingana na uhakiki uliofanywa na Wakala.
Alisisitiza kuwa
wakala uliwezesha serikali kupata mrabaha na takwimu sahihi za madini
yaliyozalishwa na migodi mikubwa nchini
kupitia ukaguzi na uhakiki madini
yaliyozalishwa na kuuzwa na migodi mikubwa ya Biharamulo, Bulyanhulu, Buzwagi,
Geita, New Luika, North Mara, TanzaniteOne, Mwadui na Ngaka, ambapo ukaguzi huo
ulisaidia kujua kiasi na thamani halisi ya madini yaliyozalishwa na kuuzwa.
“Ukaguzi huo umewezesha kukusanywa kwa jumla ya Dola za
Marekani milioni 430 kama mrabaha kutoka kwenye migodi hiyo katika kipindi cha
kuanzia mwaka 2009 hadi 2015,” alisema
Rwekaza.
Akielezea udhibiti
wa utoroshwaji wa madini kupitia viwanja vya kimataifa vya ndege hapa nchini,
Rwekaza alifafanua kuwa wakala ulianzisha ukaguzi maalum wa kukagua madini
yanayosafirishwa nje ya nchi kupitia Viwanja vya Ndege vya Julius Nyerere - Dar
es Salaam, Kilimanjaro na Mwanza na kuwakamata watu wasio waaminifu wanaojaribu
kusafirisha madini nje ya nchi kinyume cha sheria.
Alisema kupitia
ukaguzi huo jumla ya matukio 89
ya utoroshaji wa madini yaliripotiwa hadi Desemba 2015 ambapo madini hayo
yalikuwa na thamani ya Dola za Marekani milioni 10.8 na Shilingi bilioni 1.1.
na kuongeza kuwa wahusika wamechukuliwa hatua za kisheria kwa mujibu wa Sheria
ya Madini ya Mwaka 2010.
Aliongeza kuwa
wakala umekuwa ukifanya ukaguzi wa mara kwa mara wa shughuli za
ukarabati na utunzaji wa mazingira katika maeneo ya migodi mikubwa, ya kati na
midogo ambapo wahusika wamekuwa wakipewa maelekezo yenye lengo la kuboresha
hali ya mazingira kwenye maeneo yao.
No comments:
Post a Comment