Thursday, April 7, 2016

TPDC yachangia madawati 500 Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara.

Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara imepokea jumla ya madawati  500 kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC). Akiongea wakati wa kupokea madawati hayo, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Bi. Halima Dendego alisema msaada huu unamaliza kabisa tatizo la madawati kwa kata zote za kijiji cha Madimba na Msimbati. Nae Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio alisema kwamba TPDC itaendelea kutoa misaada katika maeneo ambayo inafanya shughuli zake lengo likiwa ni kuboresha maisha wa wananchi wa maeneo hayo na kufaidika na shughuli za utafiti na uendelezaji wa gesi na mafuta.  
Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio akikabidhi rasmi madawati 500 kwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Bi. Halima Dendego.
Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Bi. Halima Dendego na Mbunge wa Mtwara Vijijini. Mhe. Hawa Ghasia wakifurahia kwa pamoja baada ya TPDC kukabidhi madawati kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Madimba wakiwa wamekaa katika madawati waliyopokea kutoka TPDC.
Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio akionesha moja ya jezi ambayo TPDC ilitoa msaada kwa timu ya Wazawa FC iliyopo kijiji cha Mngoji, na Tagesh Academy zote za Mtwara.
 Wachezaji wa timu ya Wazawa FC wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Bi. Halima Dendego, Mbunge wa Mtwara Vijijini. Mhe. Hawa Ghasia, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Bi. Fatma Ally  na viongozi wengine baada ya kukabidhi msaada wa vifaa vya michezo vyenye thamani ya Tshs. 5,000,000/=

No comments: