Msimamizi wa ujenzi wa Mradi wa bomba jipya la maji kutoka Ruvu Juu Mlandizi hadi Dar es
salaam lenye urefu wa km 40 ambalo liko katika hatua za mwisho
za ujenzi kutoka DAWASA Mhandisi Christian
Gava akitoa ufafanuzi wa masuala ya kiufundi kuhusu mradi huo. Kushoto ni Meneja
Mawasiliano na Uhusiano wa Jamii wa DAWASA Neli Msuya.
Msimamizi wa ujenzi wa
Mradi wa bomba jipya la maji kutoka Ruvu Juu Mlandizi hadi
Dar es salaam lenye urefu wa km 40 ambalo liko katika hatua za mwisho
za ujenzi kutoka DAWASA Mhandisi
Christian Gava akitoa ufafanuzi wa masuala ya kiufundi kuhusu mradi huo.
Moja ya daraja linapopitisha
bomba hilo kutoka Ruvu Juu Mlandizi hadi Dar es
salaam lenye urefu wa km 40 linavyoonekana
mara baada ya kukamilika eneo la Kibamba.
Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Jamii wa DAWASA Bi. Neli
Msuya akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu ujenzi wa bomba hilo.
Wataalam wa ujenzi
kutoka DAWASA na kampuni ya Megha
Engineering & International Ltd inayojenga bomba jipya la maji kutoka Ruvu
Juu Mlandizi hadi Dar es salaam India wakiangalia moja ya matoleo 12 yanayopita chini ya barabara kuu ya Morogoro eneo la
kimara.
Waandishi wa Habari, Wataalam kutoka DAWASA na kutembelea eneo
Kimara na Kibamba ambako mafundi wa Kampuni inayojenga mradi huo ya Megha
Engineering & International Ltd wakiangalia umaliziaji wa ulazaji wa bomba la maji.
Na.Aron Msigwa - MAELEZO.
Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es salaam ( DAWASA)
imesema kuwa wakazi zaidi wa jiji la Dar es salaam na Kibaha mkoani Pwani
wanatarajia kunufaika na huduma ya upatikanaji
wa maji safi na salama ifikapo Juni mwaka huu kufuatia mradi wa ujenzi wa bomba
jipya la maji kutoka Ruvu Juu Mlandizi, Kibaha hadi jijini Dar es salaam kuwa
katika hatua za mwisho za ujenzi.
Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Jamii wa DAWASA Neli
Msuya ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam mara baada ya kutembelea eneo
Kimara na Kibamba ambako mafundi wa Kampuni inayojenga mradi huo ya Megha
Engineering & International Ltd kutoka India wanaendelea na kazi ya ujenzi
wa madaraja na matoleo ambayo bomba hilo linapitia katika barabara ya Morogoro.
Amesema hadi kukamilika kwake mradi huo utagharimu kiasi
cha dola za Kimarekani milioni 59.3 na utawezesha kiasi cha Lita milioni 196 za
maji kusafirishwa kwa siku ambazo zitaongezwa kwenye lita milioni 270
zinazozalishwa kwa siku na Mtambo wa Maji wa Ruvu Chini ulioko Bagamoyo mkoani
Pwani.
Ameeleza kuwa kukamilika kwa mradi huo kutaondoa kabisa
tatizo la uhaba wa maji katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam
ambayo yameunganishwa na mtandao wa mabomba ya DAWASCO ambayo yalikua hayapati
maji kwa muda mrefu au kupata kwa mgawo kufikia mwezi Juni, 2016.
Bi. Neli amesema kuwa ili kuhakikisha mradi huo unakamilika
katika kipindi kilichopangwa na kuanza kuwanufaisha wananchi, ujenzi wake
unakwenda sambamba na umaliziaji wa tenki jipya la kuhifadhia maji lililoko
eneo la Kibamba lenye uwezo wa kuhifadhi maji lita milioni 10 ambalo ujenzi
wake umekamilika kwa asilimia 98.
Aidha, amesema kuwa
kazi ya ukarabati wa matenki ya zamani yaliyoko eneo la Kimara jijini Dar es
salaam inaendelea sambamba na ubadilishaji wa mifumo ya mabomba ya zamani
ambayo sasa ni chakavu ili iweze kuhimili wingi wa maji uliopo.
" DAWASA tumeshaingia mkataba na Mkandarasi kwa ajili
kulaza upya mabomba ya maji kwa wananchi wasiounganishwa na maji ili waweze
kuingia kwenye mtandao wa mabomba yetu, kazi hii inaendelea katika maeneo
mbalimbali ikiwemo Kimara, Mlandizi,Kibaha, Kwembe, Segerea, Changanyikeni,
Mbezi na Makuburi" Amesema.
Bi. Neli ameongeza kuwa baadhi ya maeneo yataanza kupata
mabadiliko ya huduma ya maji kuanzia mwezi Mei kufuatia maji yatakayosukumwa
kutoka Ruvu, Mlandizi kuanza kutoka katika kituo cha kwanza kwenye tenki la
maji la Kibamba.
“Tunatarajia wananchi waliounganishwa
na mtandao wataanza kuona mabadiliko kuanzia mwezi Mei, japo sasa kuna maeneo
yana mgawo wa Dawasco,lakini baada ya maji haya kufika na kuanza kutoka kwenye
kituo cha tenki la Kibamba wananchi watakua na maji ya kutosha"
Amesisitiza.
Kwa upande wake Msimamizi wa ujenzi wa Mradi huo kutoka
DAWASA Mhandisi Christian Gava akitoa ufafanuzi wa masuala ya kiufundi kuhusu
mradi huo amesema kuwa ili kukamilisha ujenzi wa mradi huo imewalazimu kujenga
maungio 15 ambayo bomba hilo linavuka mito na matoleo 12 yanayopita chini ya
barabara kuu ya Morogoro.
Amesema kazi ya wekaji wa miundombinu ya kulifanya bomba
lipite juu ya mto kupitia madaraja yaliyojengwa imefanyika kwa umakini mkubwa
ili kuepuka kuathiri uasili wa mito husika.
Aidha, amesema kuwa ili kulinda bomba hilo na athari za
mafuriko katika mito hiyo ulifanyika utafiti maalum ukihusisha upimaji wa
kimaabara wa udongo ili kubaini namna udongo huo unavyoweza kubeba nguzo kubwa
zilizoshika bomba hilo.
Mhandisi Gava ameongeza kuwa ujenzi wa tenki la maji lenye
uwezo wa kuhifadhi lita milioni 10 umekamilikia kwa 98 na kubainisha kuwa
kilichobakia ni umaliziaji wa kazi ndogondogo.
“Ujenzi wa Tenki umekamilika, hatua
inayofuata ni kukamilisha kazi ndogondogo kisha kulijaza maji kama sehemu ya
uangalizi na taratibu za kiufundi, Tunatarajia wiki ijayo tutajaza maji"
Amesisitiza Mhandisi Gava.
No comments:
Post a Comment