Tuesday, April 26, 2016



Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali watu katika Jumuiya ya Afrika Mashariki Ruth Mtoi Simba akikabidhi msaada  wa vifaa tiba kwa  Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Ngarenaro  Dkt. Hosea Naaman msaada uliotolewa na Umoja wa Watanzania wanaofanya kazi katika jumuiya ya Afrika Mashariki  maarufu kama (WATJAM)jana jijini Arusha.

Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali watu katika Jumuiya ya Afrika Mashariki Ruth Mtoi Simba akikabidhi msaada  wa vifaa tiba kwa  Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Ngarenaro  Hosea Naaman ,msaada uliotolewa na Umoja wa Watanzania wanaofanya kazi katika jumuiya ya Afrika Mashariki  maarufu kama (WATJAM)jana jijini Arusha.

Na Woinde shizza,Arusha.
Hospitali ya Ngarenaro iliyoko wilaya ya Arusha mjini mkoa wa Arusha
inakabiliwa na uhaba wa vifaa tiba pamoja na ukosefu wa miundombinu ya maji katika wodi ya wazazi jambo ambalo linapunguza ufanisi wa
upatikanaji wa huduma za afya kwa wagonjwa.
Muuguzi Mkuu wa Hospitali hiyo Hosea Naaman  amesema kuwa uchache wa vifaa tiba umekua ukiathiri ari ya wauguzi katika kuwahudumia wagonjwa licha ya juhudi zinazofanywa na serikali bado hospitali hiyo ina mahitaji ya vifaa tiba hasa katika wodi ya wajawazito
Kufuatia Changamoto hizo Umoja wa Watanzania wanaofanya kazi katika jumuiya ya Afrika Mashariki  maarufu kama (WATJAM) wameitikia wito na kujibu changamoto hizo kwa kutoa msaada wa vifaa tiba mbalimbali ikiwemo gloves,mashuka,ambavyo vitawezesha upatikanaji wa huduma bora kwa mama na mtoto.
Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali watu Ruth Mtoi Simba amesema kuwa
Watanzania wanaofanya kazi katika jumuiya wameamua kuchangia huduma za kijamii ili kuwasaidia watanzania wenye kipato cha chini kupata huduma bora za afya.
Mwanachama wa  Umoja huo  Fadhili Mganya na Katibu wake Costantini Mashauri wamesema kuwa umoja huo umelenga kuwasaidia watanzania kutatua changamoto mbalimbali za afya ,kijamii na kiuchumi kwa kushiriki katika kutatua changamoto hizo.
Umoja wa Watanzania wanaofanya kazi katika jumuiya ya Afrika Mashariki leo wamesheherekea sikukuu ya Muungano kwa kutembelea hospitali ya Ngarenaro na kutoa msaada wa vifaa tiba ili kusaidia kuboresha huduma za afya .

No comments: