Zitto
Kabwe Mbunge wa Kigoma Kaskazini akisisitiza jambo mbele ya vijana wa
Kitanzania waishio New York. Zitto alipata nafasi ya kuongea na vijana
hao waliotaka kujua maendeleo ya nchi yao na changamoto zake ndani ya
bunge la jamhuri anavyowakilisha hoja zake kwa faida ya wananchi
kupitia upinzani, pia yeye kama mwana siasa alie upande wa upinzani nini
mtazamo wake juu ya kasi ya rais wa wamu ya 5.
Zitto ni mmoja ya vijana kwenye Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania na ni Mbunge mwenye nguvu na uwezo wa kuwakirisha hoja zenye mashiko ndani ya bunge la jamhuri na kuitikisa serikali ya chama tawala. Mfano mmoja ni suala la Escrow yeye ndiyo alikuwa chanzo cha habari hiyo iliyotikisa serikali na kupelekea wananchi kukosa imani na mwenendo mzima wa serikali ya chama tawala.
Na pia alisha wasilisha hoja ya Buzwagi ilisababisha Zitto kusimamishwa ubunge kwa miezi 4. Zitto yupo New York City kwa kivuli cha World Bank na pia alipata nafasi ya kutembelea Columbia University New York na kuongea na wasomi wa huko na pia atapata nafasi ya kutembelea Harvard University huko Boston. MA. Picha na Vijimambo Blog New York

Zitto akipata ukodak baada ya kukutana na Watanzania New York City. Kwa taswira zaidi nenda soma zaidi.
Zitto
akitafakari swali kabla kujibu, Zitto aliulizwa kama yupo tayari
kuungana na Ukawa na kama yupo tayari kungombea kiti cha urais kupitia
chama chake ACT, majibu yalikuwa yupo tayari kuungana na ukawa lakini
anaitaji kujua nini faida ya kuungana na kama kuungana ili kuing'oa CCM
basi iwe na nguvu kweli kweli na ifanikiwe kwani asinge penda kuungana
na nakubakia msindikizaji tu bila faida endelevu na kama yupo tayari
kugombea kiti cha urais basi atafanya hivyo akiwa amesha jiandaa
vilivyo ili akigombea apata ushindi wa kishimdo na kuing'oa CCM na siyo
vinginevyo.
Hapa
ni Patel akiuliza swali kwa Zitto, Patel ni Mtanzania mwenye asili ya
India ndiyo aliandaa mkutano huu kwa kushirikiana na Nasaan Chiume.
Shabani
Mseba akiuliza swali kwa Zitto swali lake nini mipango ya maendeleo
jimboni kwake.Na jibu lake lilikuwa mipango yake ni kuhakikisha elimu
inakuwa na mwamko ndani ya mkoa wake. Kwani elimu imeshuka sana na
ufaulu wa watoto umezidi kuwa chini.
No comments:
Post a Comment