Friday, April 15, 2016

MAMLAKAYA YA HIFADHI YA NGORONGORO YAINGIA MGOGORO NA WANANCHI

Na Woinde Shizza, Karatu

Wananchi wa kijiji cha Losteti kilichopo katika kata ya mbulumbulu wilayani karatu mkoani Arusha wamelalamika mamlaka ya hifadhi ya ngorongoro kwa kitendo cha kuwanyanganya eneo lao la kuchungia mifugo lijulikanalo kwa jina la Olorieni lililopo ndani ya kijiji hicho.

Wananchi hao waliyasema hayo juzi wakati wakiongea na waandishi wa habari kijijini hapo na kusema kuwa mamlaka hiyo ya hifadhi ya ngorongoro wamewanyanganya eneo hilo ambalo walikuwa wanatumia kama eneo la malisho ya mifugo yao kwa kipindi cha muda mrefu kwani walianza kulitumia tangu enzi za mababu zao .

Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Aron Saiteu Alisema kuwa eneo hilo la malisho ya mifugo ni lakwao kwa mdua mrefu lakini wanashangaa kuona hifadhi hiyo ya ngorongoro imekuja na kuwanyanganya hali ambayo inawafanya hata wao kukosa sehemu ya kufugia mifugo yao.

Walisema kuwa walishapeleka malalamiko mara kwa mara katika ofisi za viongozi wa serekali pamoja na ofisi za hifadhi hiyo lakini amna hatua yeyote ambayo imechukuliwa wala kupewa majibu ambayo yanawapa matumaini hali ambayo imepeleka wananchi hao kuumia na kukata tamaa ndani ya nchi yao.

Kukataa tamaa huku kumetokana na wananchi hao kutoruhusiwa kujihusisha na shughuli zozote za uzalishaji pamoja na kutoongezeka kwa mifugo.

“unajua ndugu waandishi sisi hapa tumeanza kufuga tangu enzi za mababu zetu lakini tunashangaa hapo juzi mamlaka ya ngorongoro inakuja na kusema eneo ni lao kwakweli huu ni unyanyasaji mkubwa kwa sisi wananchi ndani ya nchi yetu yenye uhuru wa kudhamini kila binadamu,ivi kama kweli eneo ni lao walikuwa wapi siku zote hizo mpaka leo ndio wanakuja wanasema eneo letu la kufugia ni la kwao kwakweli huu ni unyanyasaji kabisa tunaomba ndugu magufuli atusaidie kutuangalia sisi wafugaji wa kata ya mbulumbulu” alisema Lomani Sabaya.

Aidha walisema kuwa pindi wanapopeleka mifugo yao eneo hilo ata kwa bahati mbaya upigwa faini ya shilingi 10000 kwa kila ng’ombe mmoja na iwapo wakikataa mmiliki wa mfugo huo uliokamatwa upelekwa mahakamani.

Akijibu tuhuma hizo kwa njia ya simu mkuu wa idara ya uhifadhi ambaye pia ni kaimu muhifadhi mkuu wa mamlaka ya ngorongoro Izrael Namani alisema kuwa ni kweli eneo hilo ni la hifadhi hiyo ya ngorongoro nanikweli lina mgogoro mkubwa na wananchi wanao zunguka eneo hilo kwa madai kuwa eneo hilo ni la kwao kwa ajili ya ufugaji kwani walianza kulimiliki tangu enzi za mababu zao

Alisema kuwa mgogoro huu ni wa siku nyingi na unajulikana na serekali ya wilaya pamoja na ofisi ya ardhi na mpaka sasa ofisi ya ardhi walishazungumza na wapo kwenye harakati za upimaji na kumilikishwa kisheria eneo hilo kwa mamlaka ya hifadhi ya ngorongoro.

“unajua eneo hili linamipaka sasa tatizo kubwa lipo kwenye mipaka wananchi wa eneo hilo hawakubali mipaka iliopo tatizo ndio linakuja hapa sasa sisi mamlaka ya hifadhi ya ngorongoro tulishaenda wizarani kwani muhifadi mkuu alishaagiza maeneo yote yeyenye migogoro yapatiwe ufumbuzi kwa kupimwa na kumilikishwa kisheria na uzuri watu wa wizara ya ardhi wameshakuja na mpaka navyoongea na wawe zoezi limeanza ila wameanzia uko meatu ambapo napo kunatatizo kama hili na wakitoka hapo wanakuja huku kwetu kwa ajili ya kupima na kujua mipaka hiyo, sasa tatizo linalokuwepo apa ni kwamba pamoja tulifanyia kazi swal ahili lakini awa wananchi wanaona kama sisi atulifanyiii kazi kwa wakati ila sisi wenyewe tunatamani sana mgogoro huu uishe mapema kwakweli” Israel Naman

Aliwataka wananchi kuwa wavumilivu wakati tatizo hili likiwa linashughulikiwa ili kupatiwa ufumbuzi na wao kuwa walinzi wa rasilimiali za asili kwa sera ya ujirani mwema.

No comments: