Saturday, April 9, 2016

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AZINDUA MRADI WA UJENZI WA NYUMBA ZA PALM VILLEGE MSASANI BEACH WATERFONT LEO



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikata utepe kuzindua rasmi Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Palm Village Msasani Beach Waterfront Leo April 09,2016. Kulia Afisa Muandamizi Ubalozi wa China Hapa Nchini Guo Haodong, wa tatu kushoto Mwenyekiti wa Kampuni Uwekezaji ya Group 6 Jonson Huang wa pili kushoto Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. Geoge Simbachawene, na Waziri Biasha na Uwekezaji Mhe. Chales Mwinjage.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiondoa Pazia kuzindua rasmi Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Palm Village Msasani Beach Waterfront Leo April 09,2016. Kulia Afisa Muandamizi Ubalozi wa China Hapa Nchini Guo Haodong, wa tatu kushoto Mwenyekiti wa Kampuni Uwekezaji ya Group 6 Jonson Huang.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na Uongozi wa Kampuni ya Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Palm Village unaodhaminiwa na kujengwa na Kampuni ya Uwekezaji ya Group 6 ya China unaojengwa katika eneo la Msasani Beach Waterfront, Leo Aapril 09,2016.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza jambo na Afisa Muandamizi wa Ubalozi wa China Hapa Nchini Guo Haodong, wakati wa ghafla ya uzinduzi wa Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Palm Villege unaodhaminiwa na kujengwa na Kampuni ya Uwekezaji ya Gropu 6 ya China zinazojengwa Msasani Beach Waterfront.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akitembelea Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Palm Village unaodhaminiwa na kujengwa na Kampuni ya Uwekezaji ya Group 6 ya China. Mradi huo unaojengwa katika eneo la Msasani Beach Waterfront unategemewa kutoa ajira jumla ya watu 2000 utakapokamilika. Kuli Mwenyekiti wa Kampuni hiyo Jonson Huang, Leo Aapril 2016.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizindua Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Palm Village unaodhaminiwa na kujengwa na Kampuni ya Uwekezaji ya Group 6 ya China. Mradi huo unaojengwa katika eneo la Msasani Beach Waterfront unategemewa kutoa ajira jumla ya watu 2000 utakapokamilika. Leo Aapril 09,2016.(Picha na OMR).


Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan  ameyataka makampuni yanayowekeza hapa nchini kufuata misingi ya kisheria ya uwekezaji ili kusiwe na changamoto katika kipindi chote cha kutekeleza miradi hadi kukamilika.

Makamu wa Rais ametoa kauli hiyo leo (08-04-2016) kwenye hafla ya uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa "Palm Village" eneo la Msasani Beach, Jijini Dar es salaam.

Mradi huo ambao unahusisha ujenzi wa nyumba kwa ajili ya kuuzia wananchi unatekelezwa na Kampuni ya Group Six kutoka China ambayo pia inaadhimisha miaka 10 ya uwepo wake hapa nchini.

Kwa hali hiyo, Samia aliitaka kampuni hiyo kuweka bei rafiki ili Watanzania wengi waweze kuzinunua nyumba hizo jambo ambalo lilisitizwa na Afisa Mwandamizi kutoka Ubalozi wa China hapa nchini Gou Haodong mapema wakati akizungumza katika hafla hiyo.

Makamu wa Rais aliipongeza kampuni hiyo kwa ubora wa kazi zake zilizofanyika katika kipindi cha miaka 10 walichokuwepo nchini wakifanya kwa pamoja na Watanzania na kuelezea matumaini yake kuwa kampuni hiyo itahamishia ujuzi na teknolojia kutoka kwa Wachina kwenda kwa Watanzania ili hatimaye waweze kuajiriwa na mashirika mengine au kujiajiri wenyewe.

"Naendeleza pongezi zangu...Kampuni ya Group Six, mmefanya kazi nzito kwa ubora wake, mradi ukikamilika mtalipa kodi kubwa hivyo kuongeza mapato,"alisema Samia na kuongeza

"Mradi utaongeza idadi ya mali zisizohamishika nchini, mali ambayo itongeza thamani ya Tanzania na kutusogeza katika hatua ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii; vile vile utaleta haiba ya mwonekano mzuri kwa nchi yetu, na kwa ujumla utachangia kukuza hadhi ya Taifa letu mbele ya uso wa dunia."

Makamu wa Rais aliiambia kampuni hiyo kuwa serikali itatoa ushirikiano unaohitajika kuhakikisha mradi unakamilika kama ulivyopangwa kwa sababu urafiki kati ya Tanzania na China, ni urafiki wa kweli, haujawahi kuwa na vikwazo, masharti wala vigingi.  

"Kituo cha Uwekezaji Nchini (TIC) mpo hapa na Wizara ya Ardhi nawaagiza mhakikishe vikwazo vitakavyojitokeza katika utekelezaji wa mradi huu vinaondoka," alisema Makamu wa Rais.

Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri wa Viwanda na Biashara Charles Mwijage alisema mradi huo utagharimu kiasi cha dola za Kimarekani milioni 70 mpaka utakapokamilika na kuiomba kampuni hiyo iangalie uwezekano wa kuwekeza katika ujenzi wa nyumba katika mikoa mingine nchini.

Waziri Mwijage aliieleza hadhara hiyo kuwa sekta ya ujenzi hapa nchini imechangia kwa kiasi kikubwa katika pato la Taifa na kusema tafiti za takwimu za kiuchumi za kitaifa zinaonesha kuwa mwaka 2014 sekta ya ujenzi ilichangia asilimia 8.6 ya pato la Taifa ikilinganishwa  na asilimia 6.4 kwa mwaka 2006 na kuifanya sekta hiyo kushika nafasi ya tatu kwa kuchangia pato la Taifa ikilinganilishwa na sekta nyingine.

Pamoja na ujenzi wa "Palm Village" Kampuni ya Group Six imetekeleza miradi ya ujenzi wa nyumba za biashara kama vile, supermarket, hotel, villa, shule ya Pwani Kusni, baadhi ya shule za sekondari za Zanzibar, Chuo Kikuu cha Dar es salaam na Chuo Kikuu cha Dodoma.

Imetolewa na
 Ofisi ya Makamu wa Rais

Dar es salaam

No comments: