Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Alex Nkenyenge akizungumza na wadau wa riadha wakati wa ufungaji wa
mbio za Heart Half Marathon zilizofanyika jana katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam. Kulia ni Rais wa Kongamano la Afya Tanzania na Mratibu wa mbio hizo Dkt. Omary
Chillo.
Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Heart Marathon Dkt. Chakao Khalfan
akizungumza na waandishi wa Habarai mara baada ya kumalizika kwa mbio hizo jana jijini
Dar es Salaam. Heart Marathon hii imejumuisha mbio za urefu wa 21Km, 10Km, 5Km, mita
700 kwa ajili ya watoto, Baiskeli Kilomita 21 na Baiskeli walemavu.
Wanariadha washiriki wa Heart Marathon wakichuana katika mbio za urefu wa
kilomita 21 jana jijini Dar es Salaam.
Washiriki wa mbio za Heart Marathon kwa waendesha Baiskeli wakiwa katika
mashindano hayo jana jijini Dar es Salaam.
Watoto wakiwa katika mashindano ya Heart Marathon mbio za urefu Mita 700 jana
jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Alex Nkenyenge akimvalisha Medali mshindi wa kwanza kwa wanaume
mbio za Kilomita 21 Bw. Dickson Marwa wakati wa ufungaji wa mbio za Heart Marathon
zilizofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Alex Nkenyenge akimvalisha Medali mshindi wa kwanza kwa wanawake
mbio za Kilomita 21 Bibi. Failuna Abdi wakati wa ufungaji wa mbio za Heart Marathon
zilizofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Alex Nkenyenge akikabidhi Tuzo kwa mdhamini mkuu wa mbio za Heart
Marathon, Taasisi ya Tindwa Medical and Health Services wakati wa ufungaji wa mbio za
hizo jana jijini Dar es Salaam. Mbio hizo zilikuwa na kauli mbiu ya “Kuwa huru katika
magonjwa yasiyo ya kuambukiza”.
Picha na: Frank Shija, WHUSM.
No comments:
Post a Comment