Saturday, April 30, 2016

CCM MWANGA WAJIVUNIA KUTOVURUGWA NA WAPINZANI

Na Woinde Shizza, Mwanga

Wanachama wa chama Mpinduzi wilaya ya Mwanga mkoa kiliimanjaro Wameeleza kuwa pamoja na kupita kimbunga cha siasa za maji taka zilizosheheni ushabiki , ubabaishaji na hujuma,Wana  CCM wilayani humo wamebaki wamoja bila kuyumbishwa na wanasiasa wasaka madaraka kwa njia za hila na fedha .

Wamesema kuwa wale wote ambao walifuata siasa za ushabiki kwa kushabikia mambo bila kupima uzani wa siasa na ubora wa kila chama,  sasa hivi wako katika dimbwi la majuto na fedheha kwani wameshaona hasara za kuhama chama hicho.

Katibu wa CCM wilaya ya Mwanga Mkoa kilimanjaro Mwanaidi Hussein Mbisha aliyasema hayo wakati akitoa neno la shukran mara baada ya Kaimu katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka kuzungumza na viongozi wa vijiji na kata pamoja na wanachama wa chama hicho wilayani Mwanga mkoani hapa.

Mbisha alisema umadhubuti wa CCM usichukuliwe kama janbo jepesi na rahisi badala yake viongozi wa upinzani na wanachama wanaoshabikia vyama hivyo wakubali ukweli kuwa CCM iko imara .

Alisema CCM iliioachwa na marehemu baba wa Taifa Mwalimu julius Nyerere , Mzee Abeid Karume,Mzee Rashid Kawawa na mzee Thabit Kombo itabaki kuwa kimbilio na tarajio la wananchi katika kufanikisha masuala yao kisiasa, kijamii na kiuchumi.

"Shaka nimekuwa nikikusikiasikia tu na kukusoma katika vyombo vya habari,wewe bado kijana mdogo, ila unatosha kubeba hata dhamana kubwa, endelea Mungu atakusaidia uthibitishwe kuwa Katibu mkuu "alisema mbisha.

Awali Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa kilimanjaro Juma Raibu Juma aliisifu wilaya ya mwanga kwa kuendelea kuwatoa mchanga wa macho kwa kuilinda jimbo hilo lisichukuliwe na upinzani.Raibu alisema heshima ya wana mwanga kwa ccm itaendelea kuenziwa na kukumbukwa kila wakati kwa sababu ni watu jasiri wenye msimamo thabiti.

"Unapokuwa vitani halafu wapiganaji wako wakakataa katakata kupokea hongo toka kwa maadui, wakasema hatutaki na hatufaiki chochote , hao ni wazalendo"alisema Juma

Hata hivyo Mwenywkiti huyo wa UVCCM mkoa wa Kilimanjaro alimpongeza Kaimu katibu mkuu shaka kwa uthubutu wake wa kupania kurudisha heshima na hadhi ya UVCCM iliyokuwa inapotea.Shaka anaendelea na ziara yake katika wilaya ya Same ambako atahitimisha katika mkoa kilimanjaro kabla ya kuanza mkoani Tanga kwa siku sita baadae Mikao ya Manyara,Kilimanjaro na Arusha itafanya majumuisho ya pamoja mkoani mkoani hapa.
Kaimu katibu mkuu wa UVCCM taifa Shaka Hamdu Shaka akiwa anapanda mti nje ya ofisi ya CCM wilaya ya Mwanga
kaimu katibu mkuu UVCCM taifa akiwa anaongea na wananchi wa kata ya Kileo iliopo ndani ya Wilaya ya Mwanga 
kaimu katibu mkuu UVCCM taifa Shaka Hamdu Shaka akiwa anamkabidhi kiongozi wa timu ya Kileo jezi ambazo UVCCM mkoa wa Kilimanjaro waliaidi timu 
Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa kilimanjaro Juma Raib Juma akiwa anapanda mti wa ukumbusho nje ya ofisi ya CCM wilaya ya mwanga 
Shaka akiongea na wanachama wa CCM wilaya ya Mwanga hii leo

No comments: