Monday, April 4, 2016

BENKI YA TADB YAINGIA MAKUBALIANO NA PASS KATIKA UCHOCHEAJI WA KILIMO CHENYE TIJA KWA WAKULIMA.

 Mkurugenzi wa Mipango, Sera na Utafiti Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB), Francis Assenga (Kushoto) akizungumza wakati wa hafla ya kuwekeana saini makubaliano kudhamini mikopo kwa wakulima wanaokopa TADB. Kulia ni viongozi waandamizi wa TADB na PASS.
 Mkurugenzi wa Biashara na Mikopo wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Robert Pascal (Katikati) akizungumza wakati wa hafla ya kuwekeana saini makubaliano kudhamini mikopo kwa wakulima wanaokopa TADB. Kulia ni viongozi waandamizi wa TADB na PASS. Kushoto ni Mkurugenzi wa Mipango, Sera na Utafiti wa TADB, Bw. Francis Assenga (Kushoto) na Mkuu wa Sheria na Huduma wa Benki hiyo, Bibi Neema Christina John (Kulia).
 Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Thomas Samkyi (Kushoto) akizungumza kabla ya kutiliana saini makubaliano yatakayowezesha wakulima wanaokopa TADB kupata dhamana kutoka PASS. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa PASS, Bw. Nicomed Bohay.
 Mkurugenzi Mkuu wa PASS, Bw. Nicomed Bohay (Katikati) akizungumza kabla ya kutiliana saini makubaliano yatakayowezesha wakulima wanaokopa TADB kupata dhamana kutoka PASS. Kushoto ni Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Thomas Samkyi na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa PASS, Bw. Killo Lussewa (Kulia). 
 Wanahabari wakiwajibika wakati wa hafla ya kuwekeana saini makubaliano kudhamini mikopo kwa wakulima wanaokopa TADB.
 Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Thomas Samkyi (Kushoto) akitia saini makubaliano yatakayowezesha wakulima wanaokopa TADB kupata dhamana kutoka PASS. Katkati ni Mkurugenzi Mkuu wa PASS, Bw. Nicomed Bohay na na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa PASS, Bw. Killo Lussewa (Kulia).
 Mkuu wa Sheria na Huduma wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB),, Bibi Neema Christina John (Kushoto) akigonga muhuri makubaliano yatakayowezesha wakulima wanaokopa TADB kupata dhamana kutoka PASS. Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Thomas Samkyi (Katikati) na Mkurugenzi Mkuu wa PASS, Bw. Nicomed Bohay (Kulia).
 Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Thomas Samkyi (Kushoto) akibadilishana hati za makubaliano yatakayowezesha wakulima wanaokopa TADB kupata dhamana kutoka PASS na Mkurugenzi Mkuu wa PASS, Bw. Nicomed Bohay (Kulia).
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Thomas Samkyi (Kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa PASS, Bw. Nicomed Bohay (Kulia) wakionesha hati za makubaliano yatakayowezesha wakulima wanaokopa TADB kupata dhamana kutoka PASS katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya TADB. 

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
BANKI ya Maendeleo Kilimo nchini (TADB) imesema kuwa wakulima imewataka wakulima wadogo wajiunge katika vikundi ili waweze kupata mikopo  yenye masharti nafuu ya kuendeleza kilimo ambacho kitawabadilisha kiuchumi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati makubaliano ya kati ya Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) na Taasisi  ya Sekta Binafsi ya Kusaidia Wakulima (PASS), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Thomas Samkyi amesema kuwa wakulima wakitumia benki hiyo watakwamka na umasikini kutokana na kulima kilimo chenye tija.

Amesema kuwa kwa wakulima wakiwa na vigezo watapata mkopo kutokana na benki hiyo iko kwa ajili yao katika kuendesha kilimo chenye tija katika kuondokana na kilimo cha kujikimu.

Samkyi amesema kuwa PASS kutoa udhamini kwa wakulima watasidia benki kutoa mikopo kwa kutokana  dhamana hiyo.
Mazao ambayo yanapata mkopo katika benki hiyo ni Mpunga,Mahindi,Mazo ya Misitu, Ufugaji, Usindikaji Alizeti,Uwere isipo kuwa tumbaku.

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa PASS, Nicomed Bohay amesema kuwa kuanza na udhamini kwa wakulima wametenga bilioni tatu kadri wanavyokwenda na benki hiyo wataongeza udhamini huo.

Amesema kuwa udhamini waliofanya katika kipindi kilichopita wakulima wameweza kukua kiuchumi kwa kubadilisha maisha kutokana na kilimo.

Aidha amesema kuwa katika makubaliano hayo ni kwa miaka mitano na baada ya kuisha wanaweza kuendelea ikiwa ni lengo la kusaidia wakulima kukua kiuchumi.

No comments: