Waziri
wa Maliasili Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) akizungumza katika kikao
na Balozi wa Marekani hapa nchini Mhe. Mark Childress (kulia) na Ujumbe
wake katika ukumbi wa Selous Makao Makuu ya Wizara hiyo Mpingo House leo
tarehe 23 Machi, 2016. Waziri Maghembe amemuomba Balozi huyo wa
Marekani kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kukuza sekta ya
utalii nchini kwa kuwakaribisha wawekezaji kutoka Marekani kuwekeza
katika sekta hiyo.
Balozi
wa Marekani hapa nchini Mhe. Mark Childress (kulia) akizungumza na
Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe (kushoto). Balozi
huyo wa Marekani ameahidi kuendeleza ushirikiano uliopo baina ya
Tanzania na Marekani katika kuendeleza sekta ya uhifadhi hapa nchini.
Ameahidi pia kusaidia katika vita dhidi ya ujangili.
Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) akisisitiza jambo kwa Balozi wa Marekani hapa nchini Mhe. Mark
Childress (wa pili kushoto). Mhe. Maghembe alimueleza balozi huyo kuwa
Tanzania haiko tayari kuteketeza meno ya Tembo yaliyohifadhiwa mpaka
hapo itakapoona namna bora zaidi ya kufanya kwani kwa sasa Meno hayo
yanaweza kutumika kwa ajili ya tafiti mbalimbali za kisayansi na
kusaidia pia katika utambuzi na vielelezo vya mashtaka ya ujangili. Mhe
Maghembe alisema hayo baada ya Balozi Childress kutoa pendekezo kwa
Serikali kuona uwezekano wa kuteketeza sehemu ya meno ya Tembo
yaliyohifadhiwa ili kutoa ujumbe duniani wa namna Serikali ya Tanzania
ilivyodhamiria katika vita dhidi ya Ujangili.
Sehemu
ya wajumbe kutoka ubalozi wa Marekani walioongozana na Mhe. Balozi Mark
Childress wakifuatilia mada katika kikao hicho. Wajumbe hawa kila mmoja
aliwasilisha mada ikionyesha ushirikiano wa Serikali ya Marekani na
Tanzania katika sekta ya uhifadhi hapa nchini.
Baadhi ya wajumbe kutoka ubalozi wa Marekani na Wizara ya Maliasili na Utalii katika kikao hicho.
Wajumbe kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii walioshiriki katika kikao hicho. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu Bi. Angelina Madete.
(Picha na Hamza Temba - Wizara ya Maliasili na Utalii)
No comments:
Post a Comment