Tuesday, March 8, 2016

Waziri Mahiga afungua Mkutano wa Pili wa Vyama vya Kijamii vya ICGLR



Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Masahriki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine Mahiga (Mb.) akizungumza katika ufunguzi wa Mkutano wa Pili wa Jukwaa la vyama visivyo vya Kiserikali (Vyama vya Kijamii), kutoka Nchi za Jumuiya ya Ukanda wa Maziwa Makuu (ICGLR) uliofanyika mapema leo katika Hoteli ya Ramada Jijini Dar es Salaam. Katika ufunguzi huo Waziri Mahiga aliwashukuru wajumbe kwa kuchagua kuufanyia mkutano wao hapa nchini vilevile kuwa na ushirikiano katika masuala ya kijamii ambayo yatapelekea kuondoa machafuko ya wenyewe kwa wenyewe katika nchi wanachama.
Sehemu ya wajumbe wakimsikiliza kwa makini Balozi Mahiga (hayupo pichani) alipokuwa akifungua Mkutano huo. 
Sehemu nyingine ya wajumbe kutoka Sudan Kusini nao wakifuatilia kwa makini ufunguzi huo. 
Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa UN eneo la Maziwa Makuu Balozi Said Djinnit naye alipata fursa ya kuzungumza katika ufunguzi wa mkutano huo. 
Sehemu ya Watumishi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa nao wakifuatilia kwa makini hotuba  iliyokuwa ikitolewa na Mhe. Waziri Mahiga (hayupo pichani), wa kwanza kulia ni Katibu wa Waziri Mahiga, Bw. Adolf Mchemwa, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Bi. Mindi Kasiga (wa kwanza kushoto) na katikati ni Afisa Mambo ya Nje, Bw. Ally Ubwa 
Mwenyekiti wa Kikanda wa Jukwaa la Vyama visivyo vya Kiserikalikutoka nchi za Maziwa Makuu, Bw. Joseph Butiku naye akizungumza katika ufunguzi wa Mkutano huo.
Mwakilishi wa Umoja wa Afrika eneo la Maziwa Makuu Bi. Altine Traore naye akizungumza 
Meza kuu wakimsikilza Bi. Traore (hayupo pichani) alipo kuwa akitoa hotuba yake.
Waziri Mahiga akizungumza na Waandishi wa Habari.
Picha ya Pamoja.Picha na Reginald Philip

No comments: