Thursday, March 3, 2016

SIMU TV: HABARI KUTOKA VITUO VYA TELEVISHENI

 Serikali itaanza kutekeleza ahadi yake ya kutoa milioni hamsini kwa kila kijiji kama alivyoahidi Rais John Magufuli wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015;https://youtu.be/NNg3yO4LFEQ
  
Mkuu wa wilaya ya Nyamagana, Mh. Baraka Konisaga  awasimamisha watumishi wa tano wa hospitali ya Butimba kwa tuhuma ya kusababisha vifo vya watoto wawili mapacha;https://youtu.be/OnhdxY3bwwE

 Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu amesema serikali itahakikisha uchaguzi wa marudio visiwani Zanzibar unafanyika kwa amani;https://youtu.be/gHzdgnnq3qo

 Mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia chama cha ADC, Mhe Hamad Rashid athibitisha kuwa chama chake kitashiriki uchaguzi wa marudio wa Zanzibar unaotarajiwa kufanyika tarehe 20 mwezi huu;https://youtu.be/gcaoM4oju1Y

 Waziri mkuu mstaafu Mizengo Pinda awataka watumishi wa umma kufanya kazi kwa bidii kwa kuzingatia maadili ili waendane na kasi ya Rais Magufuli; https://youtu.be/itWb4HPw52Q

Waziri wa Nchi Ofisi Ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge Ajira na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama amteua Dkt.Carinan Wangwe kuwa kaimu mkurugenzi mkuu  wa mfuko wa hifadhi ya jamii NSSF;https://youtu.be/gReHNRydFcM

 Mamlaka ya mapato nchini TRA yakifunga kiwanda cha kutengeneza Mabati cha New Time Steel kinachomilikiwa na raia wa kichina kwa tuhuma ya ukwepaji wa kodi;

 Serikali mkoani Kigoma yavitaka vyama vya akiba na mikopo mkoani humo kuanzisha miradi yenye tija kiabiashara;https://youtu.be/Qt6oTAHXCEk

 Serikali visiwani Zanzibar yazitaka kampuni za simu visiwani humo kufanya utafiti wakina ili kuboresha utoaji huduma kwa wateja wao;https://youtu.be/bXqi5n4MdD8

 Timu ya taifa ya soka ya wanawake itashuka kesho dimbani kuivaa timu ya taifa ya Zimbabwe katika mchezo wa awali wa kuwania nafasi ya kushiriki miachuano ya Afrika kwa wanawake;https://youtu.be/BtGbWfoC_Lo

 Timu ya kikapu ya Toronto Raptors yaibuka na ushindi wa jumla ya pointi 104 kwa 94 dhidi ya Utah Jazz katika michuano ya kikapu ya NBA inayoendelea nchini Marekani; https://youtu.be/S5fD8jtgoao

Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu ametoa wito kwa watanzania kuendelea kudumisha amani iliyopo nchini;https://youtu.be/Es0oe4AqOSc

Serikali mkoani Mwanza yaagiza kusimamishwa kazi kwa madaktari na wauguzi 5 kwa tuhuma za kusababisha kifo cha watoto mapacha.https://youtu.be/SdsZ7Oyi2b0
   
Wabunge wa bunge la Afrika Mashariki pamoja na wale wa mabunge ya nchi wanachama wa Afrika Mashariki wakutana jijini Dar es salaam kujadili kwa undani juu ya sheria na kanuni za uchaguzi zinazotumika katika nchi hizo.https://youtu.be/RrJ9CJwHGig   
  
Wakuu wa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki waelezea adhima ya pamoja katika kuboresha maisha ya wananchi wa ukanda huo kwa kuimarisha miundombinu ya mawasiliano ikiwemo barabara na kufungua mipaka ili kuchochoea ufanisi wa kibiashara na kukuza uchumi katika jumuiya. https://youtu.be/fZmC_zXS61g  
  
Serikali inatarajia kujenga wodi za akina mama wajawazito katika vituo vyote  vya afya nchini vilivyoko maeneo ya pembezoni ili kuboresha huduma za mama na mtoto.https://youtu.be/bK1MIseCSfc  
  
Kampuni mama ya GSM Foundation yatoa msaada mbalimbali kwa wilaya ya Kinondoni ikiwemo uchimbaji wa visima 20, madawati elfu 3 pamoja na magodoro 500 katika manispaa hiyo.https://youtu.be/7fmGcSwXfFM   
  
Viongozi wa dini wa ndani na nje ya nchi pamoja na viongozi wa serikali waizindua program ya maombi maalum ya kuliombea taifa dhima ikiwa ni kulikabidhi taifa mikononi mwa Mungu.https://youtu.be/OT124WRdEYc

No comments: