Monday, March 7, 2016

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

SIMU.TV: Rais John Magufuli amuapisha Balozi John Kijazi kuwa Katibu Mkuu Kiongozi hii leo Ikulu jijini Dar es Salaam;https://youtu.be/SFJEMgKVUSE
 SIMU.TV: Inaelezwa kituo cha afya cha Nanguruwe mkoani Mtwara kiko hatarini kukifunga kitengo chake cha upasuaji  kutokana na kukabiliwa na changamoto kubwa ya maji;https://youtu.be/ST8OGtTmnqI
 SIMU.TV: Inaelezwa kuwa  mkoa wa Dar es Salaam unakabiliwa na upungufu wa vyumba vya madarasa elfu tano na madawati elfu siti na nane; https://youtu.be/8m04XIfeIw4
 SIMU.TV: Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Kisimani mkaoni Arusha waipongeza serikali kwa kufanikiwa kukarabati majengo yaliyoharibiwa na upepo mkali mwaka jana;ttps://youtu.be/C7ZCdwyxxjU
 SIMU.TV: Wafanyakazi wa hospitali ya wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza wagoma  kufanya kazi kwa zaidi ya saa sita;https://youtu.be/ba5KbEXoIq0
 SIMU.TV: Waziri mkuu Kassim Majaliwa ametoa wito kwa wanafunzi wote nchini kusoma kwa bidii ili kufikia malengo yao waliojiwekea;https://youtu.be/7ITKzwY9EKA
 SIMU.TV: Mamlaka ya vitambulisho vya taifa NIDA yasitisha mikataba  yote na wafanyakazi wa mkataba walipo katika ofisi zote za NIDA nchini; https://youtu.be/ScqjlyTRTjM
 SIMU.TV: Bodi ya sukari nchini yatoa wito kwa wasambaji na wauzaji wa rejareja wa sukari nchini kuuza sukari katika bei ya kawaida; https://youtu.be/xIxZWk6tHzc
 SIMU.TV: Waziri wa fedha visiwani Zanzibar, Mhe. Omary Yusuph azishauri benki za biashara visiwani humo kupeleka huduma za kibenki katika maeneo ya vijijini; https://youtu.be/oipiT9ai6fs
 SIMU.TV: Serikali yaitaka timu ya taifa ya mchezo wa Magongo kufanya vyema katika mashindano ya Afrika yatakayoanza kutimua vumbi machi 18 nchini Namibia; https://youtu.be/fE4IrqoRyqw
 SIMU.TV: Serikali yasema itaendelea kupambana na wezi wa kazi za wasanii wa filamu nchini ili kuwawezesha wasanii kunufaika na mapato ya kazi zao; https://youtu.be/n1KgnYlLhd0
 SIMU.TV: Rais John Magufuli amemuapisha balozi John Kijazi kuwa katibu mkuu kiongozi katika viwanja vya ikulu jijini Dar es salaam hii leo. https://youtu.be/86qdqgLojw8
 SIMU.TV: Serikali imekiri kwamba bado wanawake nchini wanakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo sheria kandamizi kwa wanawake na wasichana. https://youtu.be/LSVbA-cw7GM
 SIMU.TV: Wakazi wa Kimara manispaa ya Kinondoni jijini Dar es salaam wameaswa kutoa ushirikiano wa kutosha kwa maafisa ardhi pindi utekelezaji wa mradi wa urasimishaji wa makazi utakapo anza.https://youtu.be/EWsQy6zfNRk
 SIMU.TV: Wananchi mkoani Geita wameaswa kuacha kujichukulia sheria mkononi kwa kuwapiga na kuwaua watuhumiwa wa uhalifu kwani hatua hiyo inaweza pelekea mauaji ya watu wasio na hatia.https://youtu.be/6YKhiZCUXOM
 SIMU.TV: Wizara ya maliasili nchini imeonya kuichukulia hatua kampuni ya kichina ya CHICO iliyokabidhiwa dhabuni ya uwakala wa usambazaji wa umeme vijijini iwapo kampuni hiyo itashindwa kukamilisha miradi ya usambazaji wa umeme vijijini kwa wakati.https://youtu.be/_6YGUAZHZwU
 SIMU.TV: Wimbi la kufurika kwa wanafunzi mashuleni katika shule za msingi wilayani Temeke jijini Dar es salaam Tangu serikali itangaze elimu bure limeendelea kuwatesa viongozi wa jiji hilo akiwemo mkuu wa mkoa na wakuu wa wilaya.https://youtu.be/6dDZ7gjfUxg
 SIMU.TV: Kufuatia changamoto kubwa iliyopo katika sekta ya afya hasa katika meoneo ya vijijini, baadhi ya wananchi wilayani Uyui mkoani Tabora wajitokeza kutekeleza serikali kwa vitendo kwa kujitolea kujenga kituo cha afya, hatua itakayo wapunguzia adha hususani kwa wanawake wajawazito. https://youtu.be/umpjt1-uv3k 

No comments: