Sunday, March 13, 2016

SIMBA YAIFUNGA TANZANIA PRISONS 1-0

 Golikipa wa Tanzania Prisons, Beno Kakolanya akiokoa hatari langoni mwake mbele ya beki wa Simba, Justice Majabvi wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo ambapo timu ya Sima  imeweza kuchomoza na ushindi wa bao 1-0 na kujitika kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo kwa kufikisha pointi 54. (Picha na Francis Dande)
 Mshambuliaji wa Simba, Ibrahim Ajib akimtoka beki wa Tanzania Prisons, Jumanne Elfadhil
 Benki wa Simba, Mohamed Hussein akimiliki mpira.
 Beki wa Prisons, Laurian Mpalile akichuana na Daniel Lyanga.
 Daniel Lyanga akimiliki mpira.
 Benjamin Asukile wa Prisons akichuana na mshambuliaji wa Simba, Daniel Lyanga.
 Ibrahim Ajib akimtoka beki wa Prisons.
 Golikipa wa Prisons, Beno Kakolanya akionyeshwa kadi ya njano na mwamuzi Jocob Adongo kutoka Mara.
  Golikipa wa Prisons, Beno Kakolanya akionyesha hasira baada ya kuonyeshwa kadi ya njano.
 Golikipa wa Prisons, Beno Kakolanya akiokoa moja ya hatari langoni mwake.
 Masahabiki wa Simba wakishangilia timu yao.

No comments: