Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni
(kulia), akisalimiana na maafisa wa Idara ya Uhamiaji wakati wa ziara
aliyoifanya katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
Katikati ni Mkuu wa wa Ofisi ya Uhamiaji katika Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Abuu Mvano.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni,
akisalimiana na Maafisa wa Jeshi la Polisi, alipotembelea Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kukagua shughuli zinazofanywa na
Idara za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Kushoto ni Kamanda wa Polisi
wa Viwanja vya Ndege, ACP Martin Otieno.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni,
akizungumza na watendaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani waliopo katika
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na Waandishi wa Habari
wakati wa ziara yake aliyoifanya kutembelea Idara za Wizara hiyo
zilizomo katika Uwanja huo.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni
(kushoto), akisalimiana na Kamanda wa Kanda Maalum ya Kipolisi Mkoa wa
Dar es Salaam, Simon Sirro alipotembelea Kituo cha Polisi Buguruni
wakati wa ziara yake katika Kituo hicho.
Mkurugenzi
wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Paul
Rwegasha (katikati), akiongozana na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) wakati Waziri huyo
alipotembelea Uwanja huo. Kushoto ni Kamanda wa Polisi wa Viwanja vya
Ndege, ACP Martin Otieno.
Mkuu
wa Ofisi ya Uhamiaji katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere, Abuu Mvano (kulia), akiongozana na Naibu Waziri wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), alipotembelea
Idara za Wizara hiyo zilizopo katika Uwanja huo. (Picha na Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi)
No comments:
Post a Comment