Naibu
Waziri wa Afya, Dkt Hamisi Kigwangalla katika ufunguzi wa Kongamano la
tatu la Kisanyansi na Utafiti wa ugonjwa wa kisukari Africa,
lililozinduliwa leo katika ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere
(JNICC),Kongamano hilo ambalo litamalizika tarehe 16 March 2016,
linaendeshwa na Asasi inayojihusisha na Masuala ya Ugonjwa wa kisukari
Afika Mashariki na Kusini,asasi inayojulikana kama (EADSG) The Eafrica
diabetes study group.Asas hii ilianzishwa mwaka 2011 ili kuhamasisha
jamii kuhusu ugonjwa huo na kuutafiti pamoja na kutafuta tiba.Kushoto
kwake ni Mratibu wa Kongamano hilo Doctor Kaushik Ramaiya,na baadhi ya wageni kutoka Mfuko wa kusaidia Kisukari Duniani (NCD Symposium),kutoka Denmark.
Kongamano la tatu la Wanasanyansi wa ugonjwa wa kisukari limezinduliwa leo na Naibu Waziri wa Afya, Dkt Hamisi Kigwangalla katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere (JNICC)
Kongamano hilo ambalo litamalizika tarehe 16 March 2016, linaendeshwa na Asasi inayojihusisha na Masuala ya Ugonjwa wa kisukari Afika Mashariki,asasi inayojulikana kama (EADSG) The Eafrica diabetes study group.Asas hii ilianzishwa mwaka 2011 ili kuhamasisha jamii kuhusu ugonjwa huo na kuutafiti pamoja na kutafuta tiba.
Akiongea na waandishi wa Habari, Mratibu wa Kongamano hilo Doctor Kaushik Ramalya, Kongamano hilo limekaribisha wageni kutoka nchi nyingine za Afrika ya Mashariki na kusini kushiriki katika majadiliano na uchunguzi huo wa Kisayansi, ikiwa ni pamoja na kubadilishana uzoefu wa namana ya kutua matatizo yatokanayo na ugonjwa huo.
Alisema kongamano hilo ambalo linahusisha East African Diabetes study Group (EADSG) kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, litafuatiwa na mkutano Maalum wa wadau wa kisukari duniani utakaofanyika, Machi 17 hadi 18 2016 katika ukumbi huo huo wa Kimataifa wa Julius Nyerere Convention Centre jijini Dar Es Salaam, Tanzania.
Mkutano huo ulioandaliwa na Mfuko wa kusaidia Kisukari Duniani (NCD Symposium),kutoka Denmark kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia wazee na Watoto nchini Tanzania, pamoja na Shirika la Afya Duniani Ofisi za Mikoa kwa Afrika pamoja na Shirikisho la Kisukari duniani utajadili mambo mbali kuhusu namna ya kusaidia wagonjwa wa ishio na Kisukari kwa kuwa gharama zake ni kubwa mno.
Mikutano hiyo miwili inalenga kutatua tatizo kubwa la Kisukari linalooendela kukua barani Afrika kwa sasa ambalo limeonekana kukua mara tatu zaidi ndani ya miaka mitano iliyopita.
Dk. Kaushik alisema kuwa, mbali na mjadala wa uchunguzi wa kisayansi, Mambo mengine yatakayo jadiliwa ni pamoja na
• Kuongezeka kwa ugonjwa wa kisukari katika nchi zinazoendelea, na lengo hasa juu Africa na namna ya kutatua matatizo yatokanayo.
• Kujadili kuhusu mzigo wa kijamii na kiuchumi unaotokana na watu wenye ugonjwa wa kisukari , familia zao na jamii kwa ujumla.
• Umuhimu wa kutafuta ufumbuzi wa Ugonjwa huu.
• Taarifa za uchunguzi za wataalam ngazi za mkoa.
Aidha utafiti uliotolewa hivi karibuni umeonyesha kuwa katika kila sekunde sita mtu mmoja hufa kutokana na ugonjwa wa kisukari ( vifo zaidi ya milioni 5.0 hutokea duniani)
- Mmoja katika watu wazima 11 ana ugonjwa wa kisukari ( watu milioni 415 duniani kote wanaishina Kisukari)
- Moja katika vizazi saba, huadhirika na ugonjwa wa kisukari katika kipindi cha ujauzito na kujifungua.
- Robo tatu (75%) ya watu wenye ugonjwa wa kisukari wanaishi katika nchi chini na kipato cha kati.
- Zaidi ya watu wazima wengi wanakufa kutokana na ugonjwa wa kisukari kuliko kutokana na VVU / UKIMWI, kifua kikuu na hata malaria.
- wastani wa milioni 14.2 watu wazima wenye umri kati ya 20-79 wana ugonjwa wa kisukari katika Kanda ya Afrika.
- Afrika inaongoza kwa wagonjwa wa kisukari ambao haujatambuliwa, kutokana na kutocheki afya zao; zaidi ya 66.7 % ya watu wenye ugonjwa wa kisukari hawajui kuwa wana ugonjwa wa kisukari.
- Mtu na kisukari aina ya 2 (Type 2 Diabetes) anaweza kuishi kwa miaka kadhaa bila kuonyesha dalili yoyote, madhara yanayoweza kujitokeza ni pamoja na ugonjwa wa figo , moyo kushindwa kufanya kazi, ugonjwa wa jicho na kusababisha upofu na matatizo ya mguu na kusababisha ulema.
- Mataifa ya Afrika kwa idadi kubwa ya watu wenye ugonjwa wa kisukari ni pamoja na Afrika Kusini (2.3 milioni ), Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (1.8 milioni ) , Nigeria ( milioni 1.6 ) na Ethiopia (1.3 milioni).
No comments:
Post a Comment