Sunday, March 6, 2016

MWIGULU NCHEMBA APANGA KUBORESHA UZALISHAJI SHAMBA LA KITULO

Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mh.Mwigulu Nchemba akiwa na Mbunge wa Makete Mh.Noramn Sigalla wakati alipowasili kwenye shamba la Kitulo ambalo ni moja ya Mashamba makubwa ya kufuga Ng'ombe wa kisasa aina ya Mitamba.Huwa ni mfano wa Ng'ombe wa kisasa aina ya Mitamba wanaopatikana shamba la kitulo wenye uwezo wa kutoa maziwa lita 15 hadi 20 wanapokamuliwa mara moja kwa kila mmoja.Mwigulu Nchemba akipewa maelekezo kutoka kwa meneja wa shamba la kitulo kuhusiana na uzalishaji wa Ng'ombe aina ya mitamba.Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Makete Ndg.Mh.Mwigulu Nchemba akiwa kwenye shamba la kitulo akipewa maelezo mbalimbali yanayohusiana na kuyumba kwa ufugaji wa ng'ombe kwenye shamba hilo.Moja ya Farasi ambaye anafugwa kwenye shamba la Kitulo,Idadi ya Farasi wanaofugwa imepungua kutokana na wengi kuuzwa kwa wananchi.Moja ya Dume la Ng'ombe la kisasa ambalo limezalishwa Shamba la kitulo.Mh.Mwigulu Nchemba akiangalia namna ukamuaji wa maziwa unavyofanyika kwenye shamba la kitulo.Akiwa njiani kutokea shamba la Kitulo,Mh.Mwigulu Nchemba alipata nafasi ya kuzungumza na wananchi wa kata ya kikondo ambao walikuwa na malalamiko ya kulipwa fidia baada ya kuhamishwa kutoka hifadhi ya Kitulo,Madai yao ya fidia ni fedha ya Tanzania Bilion 1.8,Mwigulu amewaahidi kuwasaidia wananchi hao kwa kuzungumza na waziri wa Mali asili na Utalii aweze kuprocess malipo hayo.Mbunge wa Makete,Dr.Norman Sigalla akiomba kwa Waziri wa kilimo,Mifugo na Uvuvi kufanikisha zoezi la kuboresha shamba la kitulo ili uchumi wa wananchi wake wa Makete na wanaozunguka shamba hilo uimarike.

Shamba la Kitulo la Ufugaji wa Ng'ombe aina ya Mitamba lilianzishwa mwaka 1963 na Mwl.Nyerere kama eneo la kuzalisha maziwa ya kusambaza nchi nzima,Ng'ombe aina ya Mitamba wanaopatikana kwenye shamba hilo waliingizwa nchini kutokea Marekani na nchi za Ulaya Mashariki ambazo hali yake ya hewa inaendana na ile ya kitulo ambayo kuna wakati ni 0 centgrade,na hali ya juu zaidi inaweza kuwa 19 Centgrade.
Kuanzia miaka hiyo ,Shamba la kitulo ambalo linauwezo wa kulisha ng'ombe elfu nne (4000),Shamba hilo kwa sasa lina ng"ombe mia saba tu(700).
Mbali zaidi,nyenzo za kutunzia ndama na kukamua maziwa haziridhishi na ukuziaji wa nyasi zilizopandwa kwaajili ya malisho haulidhishi.
Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mh.Mwigulu Nchemba,baada ya kusikiliza na kuona changamoto zinazolikabili shamba la kitulo kwa ufugaji wa ng'ombe,Ameahidi kuhakikisha analiboresha na kusaidia upatikanaji wa ng'ombe wa kutosha,huduma za kutosha ili eneo la kitulo liwe ni shamba darasa hata kwa mashamba mengine ndani na nje ya nchi yetu.
Picha/Maelezo na Festo Sanga Jr.

No comments: