Na. Atley Kuni- Afisa habari Mwanza.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella amesema ifikapo tarehe 30. Mei, 2016 endapo
viongozi wa Wilaya za mkoa huo watakuwa bado wanakabiliwa na Ugonjwa wa Kipindupindu
katika wilaya zao basi wajiandae kuwajibika.
Alitoa kauli hiyo wakati akizungumza kwenye kikao cha kujitambulisha kwenye ukumbi wa ofisi
ya mkuu wa Mwanza mara baada yakuwasili mkoani humo na kuanza kazi mara moja.
Mongella alisema moja ya jambo lililonikera nikuona mkoa huo bado unakabiliwa na adha ya
kipindupindu huku Wakuu wa Wilaya, wakurugenzi na wataalam wakiwa hawana mipango
madhubuti yakutokomeza janga hilo “sasa tutaanza Operesheni maalum ijulikanayo Tukomeza
Kipindupindu Mkoa wa Mwanza kuanzia tarehe 01 Aprili,2016 na hatutakuwa na simile na
yeyote atakayetukwamisha” alisema na kusisitiza “Nina Machinery zote kwa nini nishindwe?
Mongela amesema Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi ambaye kufikia tarehe 30, Mei atashindwa
kudhibiti kipindupindu itabidi wawiane radhi kwani hata kuwa tayari kuona anaadhibiwa kwa
makosa ya mtu mwingine kwa uzembe.
“ Jamani suala la Kipindupindu tatizo lake kubwa ni
uchafu” Mnataka mkuu wa mkoa kila siku aende kufagia, no haiwezekani, sitaweza kufanya
hivyo, mimi mkuu wa mkoa nitatoka siku moja, nitaonesha mfano lakini sio kila siku, haya
nikifagia Nyamagana na Sengerema nikafagie lini? Alihoji Mongella, “lazima kila mmoja
awajibike kwa majukumu yake”.
Kwa mujibu wa taarifa za ugonjwa wa kipindupindu kutoka ofisi ya Mganga mkuu wa Mkoa hadi
kufikia tarehe 17, Machi, 2016 jumla ya wagonjwa 1,775 walikuwa wameugua ugojwa wa huo
ilihali wagonjwa waliopo kwenye matibabu ni kumi nanne (14) wagonjwa wapya wakiwa 5,
wagonjwa hawa wanatokea katika Wilaya za Ukerewe (11), Ilemela (2) na Nyamagana (1).
Mongella katika hatua nyingine ameomba kupewa ushirikiano na watendaji wote, huku
akisema katika kutekeleza majukumu yake ya ukuu wa mkoa hata muonea mtu kwani kufanya
hivyo nikumkosea hata Mungu.
“ Najua wananchi huko nje wakisikia fulani katumbuliwa
wanafurahi kweli kwakuwa ndio haja ya mioyo yao wanayo yapata wao, wananchi huunganisha
na huduma tunazo zitoa” hivyo ni vizuri tu ukatekeleza wajibu wako kwa kufuta kanuni kama za
jeshini, “wenzetu jeshini mimi nawapenda kweli kweli maana kule ni Usimamizi, Maelekezo na
Utendaji hakuna blablaa alisema Mongela.
John Mongella anakuwa Mkuu wa mkoa wa Mwanza wa ishini na mbili, tangu mkoa huo ulipo
anzishwa mwaka 1961, huku akiwa ni miongoni mwa wakuu wa mikoa 26 walioteuliwa na Rais
wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli kushika
wadhifa huo siku ya jumapili tarehe 13. Machi. 2016, akichukua nafasi iliyo achwa wazi na
Magessa Mulongo aliye teuliwa na kuhamishiwa katika Mkoa wa Mara.
No comments:
Post a Comment