Thursday, March 17, 2016

KAMATI YA BUNGE YA MAENDELEO YA JAMII YATEMBELEA MFUKO WA BIMA YA AFYA (NHIF)

01
Mbunge wa Busega na Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Maendeleo ya jamii Mh. Raphael Chegeni akisaini kitabu cha wageni mara baada ya wajumbe wa kamati hiyo kuwasili katika ofisi za Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa jijini Dar es salaam ambapo kamati hiyo imekutana na uongozi wa mfuko huo ili kusikiliza mipango yao ya baadae na changamoto mbalimbali zinazoikabili taasisi hiyo ikiwa ni pamoja na mafanikio na kuangalia mambo kadhaa yanayokwamisha shughuli za mfuko huo ili hatua za kurekebisha zichukuliwe na kwa ajili ya kufanya mfuko huo kusaidia jamii katika suala zima la afya , Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa mfuko huo Bw. Michael Muhando.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM).
1
Mbunge wa Busega na Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Maendeleo ya jamii Mh. Raphael Chegeni akisaini kitabu cha wageni na mbunge wa Kigoma mjini Mh. Zitto Kabwe wakati wajumbe wa kamati hiyo walipowasili katika ofisi za mfuko huo Kurasini jijini Dar es salaam.
2
Mbunge wa Busega na Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Maendeleo ya jamii Mh. Raphael Chegeni pamoja na wajumbe wa kamati hiyo wakiendelea na utaratibu wa kusaini kitabu cha wageni.
3
Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii wakielekea mwenye ukumbi wa mkutano kwa ajili ya kupewa taarifa na Kaimu Mkurugenzi wa mfuko huo Bw. Michael Muhando wa kwanza kulia.
5
Kutoka kulia ni Mbunge wa Ilala Mh. Azzan Zungu, Mbunge wa Kigoma Mh. Zitto Kabwe, Kaimu Mwenyekiti wa kamati hiyo na Mbunge wa jimbo la Busega Dk. Raphael Chegeni, Mbunge wa Kigamboni Mh. Dk. Faustine Ndugulile, Kaimu Mkurugenzi wa Mfuko wa Bima ya afya NHIF Bw. Michael Muhando na Mkurugenzi wa huduma za utabibu na ufundi Dk.Frank Lekey wakielekea kwenye mkutano.
6
Mbunge wa Busega na Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Maendeleo ya jamii Mh. Raphael Chegeni akizungumza katika mkutano huo huku Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati) akifuatilia mkutano huo, kulia ni mjumbe wa kamati hiyo Mbunge wa Kigamboni Mh. Dk. Faustine Ndungulile.
7
Wajumbe wa kamati hiyo wakisikiliza wakati Kaimu Mkurugenzi wa NHIF alipokuwa akiwasilisha ripoti ya shirika hilo kwa kamati hiyo leo.
8
Baadhi ya wakurugenzi wa vitengo NHIF wakifuatilia mambo kadhaa wakati wa uwasilishaji wa ripoti hiyo mbele ya Makamti ya Bunge Maendeleo ya Jamii, kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa NHIF, Rehani Athumani na Ali Othman Mkurugenzi wa TEHAMA NHIF.
9
Mjumbe wa kamati Mbunge wa Buchosa Mh. Dk Charles Tizema akitoa mchango wake katika mkutano huo.
11
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akifafanua jambo mbele ya kamati hiyo wakati wa mkutano huo kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa NHIF Bw. Michael Mhando na katikati ni Kaimu Mwenyekiti wa Kamati na Mbunge wa jimbo la Buseka Dk. Raphael Chegeni.
12
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk . Mpoki Ulisubisya akifafanua jambo mbele ya kamati hiyo huku wabunge wakifuatilia.
13
Kaimu Mkurugenzi wa NHIF Bw. Michael Mhando akitoa ufafanuzi wa mambo kadhaa yaliyojadiliwa na kamati hiyo pamoja na uongozi wa NHIF.
15
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akikagua kituo cha huduma kwa wateja kwa njia ya simu kilichoanzishwa kwa ajili ya kuwafanya wateja kupata taarifa mbalimbali kuhusu mfuko huo bila kulazimika kufika ofisini.
16
Katibu Mkuu wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Mpoki Ulisubisya akiongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa NHIF Bw. Michael Muhando wakati akielekea kukagua eneo linaohifadhi kumbukumbu za mfuko huo.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM).

No comments: