Thursday, March 3, 2016

MBUNGE LAMECK AIRO AKABIDHI VISIMA VIWILI ALIVYOAHIDI KIPINDI CHA KAMPENI MARA BAADA YA USHINDI WA KISHINDO JIMBO LA RORYA

Mbunge wa Rorya Mhe. Lameck Airo akimtwisha ndoo ya maji mama wa kijiji cha Nyanduga wilayani Rorya mara baada ya kukabidhi visima hivyo viwili vya maji kwa wanakijiji hao. 
"Miradi miwili ya maji kwa wananchi wa eneo la kijiji cha Nyanduga imekuja mara baada ya wananchi hao kukabiliana na changamoto ya uhaba wa maji ambapo kwa sasa mto waliokuwa wakiutegemea kuwazalishia maji Mto Mori kukauka na kujaa tope" Asema Mbunge wa vitendo Mhe. Lameck Airo. 

Mbunge Lameck amesema kuwa anajivunia kukamilisha miradi hiyo miwili ambayo imekuja kama sehemu ya kutimiza ahadi aliyoitoa kipindi cha kampeni za uchaguzi wa mwaka 2015 ambapo mbunge huyo aliahidi kuitimiza iwapo atapata ridhaa ya kuwaongoza tena wananchi hao.

Chama Cha Mapinduzi CCM kwenye uchaguzi huo kupitia Mbunge lameck Airo alikosa kura 18 tu kati ya kura 3600 zilizopigwa na Rais Magufuli alikosa kura 20 tu kati ya kura 3600 zilizopigwa na wananchi wa kijiji hicho.
Licha ya kuboresha pia miundombinu ya barabara kwa kiwango cha changarawe kwa kila msimu unaohitaji matengenezo pindi barabara hizo zinapopitika kwa shida, Mhe. Lameck ameamua kuwapa shukurani kwa kutimiza ahadi yake katika kutatua changamoto hiyo ya maji inayo wakabili.
Mbunge wa Rorya Mhe. Lameck Airo akikinga ndoo ya mmoja kati ya akinamama waliojitokeza kwenye uzinduzi huo wa visima viwili katika kijiji cha Nyanduga wilayani Rorya mkoani Mara. 
Mama akitwikwa maji. 
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Rorya Mhe. Samuel Kiboye al-maarufu Namba 3 akimtwisha dumu la maji moja wa akinamama waliohudhuria uzinduzi wa visima vilivyojengwa na Mbunge wa Rorya Mhe. Lameck Airo na kuvikabidhi kwa wananchi hao.
Mwaka jana katika kipindi cha msimu wa kiangazi kupitia kisima cha kale kilichojengwa miaka ya 1980, ndoo moja ya maji ilikuwa ikijaaa mara baada ya kuegeshwa bombani kuanzia saa 6 hadi 12 jioni.
Kila kisima kimegharimu kiasi cha shilingi milioni 12 na kufanya idadi ya jumla kwa gharama iliyotumika kwa visima vyote viwili kuwa milioni 24. 

No comments: