Monday, March 14, 2016

SHULE YA MSINGI JESHI LA WOKOVU YAPIGWA JEKI.

Baadhi ya wadau wakitoa zawadi na vitu mbalimbali kwa Madam Sophy ambavyo vitagawiwa kwa wanafunzi wa shule hiyo ya Jeshi la Wokovu na wale wa Makumbusho Sekondari.

Taasisi mpya ya Kijamii ijulikanayo Madam Sophy Charity Events yenye malengo ya kusaidia jamii hasa ile yenye uhitaji maalum ikiwemo watu wasiojiweza imezinduliwa rasmi mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam sambamba na kutoa misaada mbalimbali kwa watu na watoto wenye uhitaji huo maalum.

Tukio hilo la kipekee lililoandaliwa na kuratibiwa na Mwanadada, Sophia Mbeyela pia lilijumuisha wadau na marafiki mbalimbali walioungana na Madam Sophy katika kufanikisha tukio hilo lililofanyika katika ukumbi wa shule ya Msingi ya Jeshi la Wokovu ambayo ilishirikisha watoto wanafunzi wa kituo cha Matumaini wenye Ulemavu wa viungo na ngozi.

Madam Sophy na marafiki zake kwa pamoja waliweza kutoa misaada ya vitu mbalimbali kwa watoto hao ambapo pia walipata wasaha wa kuzindua taasisi hiyo huku mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni ambaye aliwakilishwa na Mbunge Kibaha Vijijini, Mh. Amoud Abduul Jumaa ambaye aliahidi kufikisha kilio cha walemavu na watu wenye mahitaji maalum Serikalini paamoja na kwenda kuwasilisha Bungeni ilikuona utekelezaji wake kwa ukaribu.

“Madam Sophy Charity. ni taasisi ambayo zaidi ni kuona wenzetu wenye uhitaji maalum hasa walemavu wanapata nafuu katika kuendana na majukumu ya nchi hii kwani sote tuna haki sawa kama wengine na ulemavu wetu usitutenganishe. Tunahitaji Serikali kuhakikisha inashusha bei vifaa vyote vya walemavu ikwemo viungo vya bandia ikiwemo mikono na miguu ambayo kwa kiungo mimoja pekee yake kinakaribia hadi milioni moja” alieleza Madam Sophy.

Madam Sophy aliongeza kuwa, Serikali inayo wajibu wa kujenga shule nyingi zaidi za watu wenye ulemavu kwani zilizopo sasa bado ni chache na watu wenye ulemavu wamehamasika kujitokeza kusoma hivyo jukumu lililopo ni kuhakikisha wanaongeza shule za watu hao pamoja na kutengeneza miundombinu ambayo inakuwa rafiki kwa walemavu kuanzia mashuleni na hata maeneo muhimu.

Aidha, Kwa upande wake, mgeni rasmi huyo aliweza kuchangia kiasi cha Sh Laki tano kwa ajili ya kuunga mkono juhudi na harakati za Madam Sophy ambapo alieleza kuwa, licha ya ulemvu wake ameweza kuonesha njia ya kujikwamua pamoja na kuwasaidia wenzake.

Madam Sophy ambaye kitaaluma ni Mwalimu, ni miongoni mwa wanafunzi waliopata kusoma katika shule hiyo na kumaliza hapo darasa la saba mwaka 2002 ambapo pia aliendelea na shule mbalimbali ikiwemo Sekondari ya Jangwani na baadae chuo, ameomba wadau kujitokeza kuungana naye katika kuhakikisha wanasaidia watu na jamii yenye uhitaji maalum kwani kutoa ni moyo.
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni ambaye aliwakilishwa na Mbunge Kibaha Vijijini, Mh. Amoud Abduul Jumaa akitoa nasaha zake kwa niaba ya Mh. Masauni. wakati wa uzinduzi rasmi wa taasisi hiyo ya Madam Sophy Charity Events. Upande wa kulia ni Madam Sophy.
Baadhi ya viongozi wa Jeshi la Wakovu wanaosimamia shule hiyo ya Msingi wakifuatilia tukio hilo..
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika mkutano huo.
Wageni waalikwa.
Wanafunzi wenye ulemavu wa viungo na ngozi wakiwa katika tukio hilo.
Wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi wakitoa burudani kwa mgeni rasmi (hayupo pichani
Mtoto Emmanuel Anthony 'Rais' akifurahia jambo katika tukio hilo. Emmanuel ameeleza kuwa, licha ya kuwa mlemavu, ndoto yake ni kuja kuwa Rais.
Meja wa Wilson Chacha wa Jeshi la Wokovu ambaye pia aliwahi kumfundisha Sophy miaka ya nyuma akitoa salamu zake katika tukio hilo.
Mtoto akisoma risala maalum kwa mgeni rasmi
Mgeni rasmi Mbunge wa Kibaha Vijijini, Mh. Amoud Abduul Jumaa akikata keki kwa pamoja na Madam Sophy kuashiria uzinduzi rasmi wa tukio hilo.
Mgeni rasmi Mbunge wa Kibaha Vijijini, Mh. Amoud Abduul Jumaa akimlisha keki Madam Sophy.
Madam Sophy akimlisha keki mgeni rasmi Mbunge wa Kibaha Vijijini, Mh. Amoud Abduul Jumaa 
Madam Sophy akimlisha keki mama yake mzazi wakati wa tukio hilo..
Mama Mzazi wa Sophy akimkumbatia mwanae
Mwanadada, Hoyce Temu aliyejitoa kusaidia watanzania kupitia kipindi maalum cha 'MIMI NA TANZANIA' akilishwa keki na Madam Sophy katika tukio hilo
Hoyce Temu akimpongeza Madam Sophy kwa kuanzisha taasisi hiyo pamoja na kuandaa shughuli hiyo.
Madam Sophy akitoa nasaha zake juu ya hatua aliyofikia hadi kuanzisha taasisi hiyo.
Baadhi ya watoto waliofika katika tukio hilo wakifanya maombi maalum kuwaombea wenzao wenye mahitaji maalum.
Baadhi ya watoto hao wenye ulemavu wa viungo.
Madam Sophy akitoa nasaha zake.
Madam Sophy akikabidhi baadhi ya zawadi kwa wanafunzi wa shule ya Makumbusho ambayo anafundisha pamoja na watoto wa shule hiyo ya Jeshi la Wokovu.

No comments: