MBUNGE wa Busanda (CCM) LOLENSIA
BUKWIMBA ameeleza furaha yake kwa kamati maandalizi ya Tamasha hilo ambalo halikuwahi kufanyika
mkoani humo na imekuwa faraja kwake kama mwakilishi wa wananchi wa mkoa huo unaokabiliwa na mauaji kwa walemavu wa ngozi.
Alisema
amefurahishwa kufanyika kwa tamasha hilo mkoani Geita na mikoa mgine kwani ana imani wakazi wa mkoa huo
watahamasika kuacha mauaji ya Watanzania
wasio na hatia ambao ni walemavu wa ngozi na vikongwe ambayo yanaendelea. Mbunge
huyo anaelezea furaha yake, ana imani wananchi wa mkoa wa Geita watafurahi
kwa sababu mkoa huo umesuswa kwa kuwapelekea matamasha ya namna hiyo na kusikia
yanafanyika katika mikoa mingine kama Dar es Salaam na Mwanza.
“Nimefurahi
sana Msama kulileta Tamasha hili litakalopiga vita mauaji ya vikongwe na
walemavu wa ngozi, nina imani wananchi wataweza kuelimika kwa njia moja au
nyingine, baada ya hapo inawezekana kabisa likaweza kubadilisha fikra na
mtizamo juu ya suala hili na kupunguza kabisa mauaji haya,” anasema Lolensia.
Alieleza
kuwa limekuwa jambo la bahati kwa mkoa huo kufikiwa na tamasha hilo ambalo lina
mafanikio makubwa katika kutimiza malengo yanayokusudiwa hivyo anaamini
kilichokusudiwa kwa Geita kitafanikiwa kwa kiasi kikubwa. “Tunawakaribisha sana na nichukue nafasi ya
pekee kumpongeza Msama kwa uamuzi wake wa kutuletea tamasha hili tunatarajia
kupata mambo makubwa pia nina imani wanageita watafurahia mno kwasababu
wanapenda mambo hayo ya muziki hasa huu wa Injili,” alisema Lolensia.
Aidha
alifafanua kuwa ana uhakika wananchi watalifurahia na watafika kwa
wingi na hata wale wa pembezoni mwa mji huo kwani kote huko wameathirika na mauaji. Lolensia
alisema kuwa Msama sio kampuni ngeni masikioni mwake anaifahamu muda mrefu huku
akisisitiza kuwa amewahi kuiandikia barua ya kuomba sapoti kwa ajili ya watu wake wa jimbo, hivyo
anafurahi kuwa Msama ameamua kwenda mwenyewe.
“Kama kampuni ya Msama imeamua
kuja Geita tunafurahi maana ataweza kutoa sapoti kwa njia hii maana wahitaji
wako wengi ukizingatia eneo lenyewe linashughuli nyingi za kiuchumi” alisema.
Alizitaja
baadhi ya shughuli hizo ni pamoja na uchimbaji wa madini na kwamba watu
wengi wanaingia na kutoka hivyo inasababisha wingi na watoto wanazaliwa kwa
wingi ambako wazazi wao wanajishughulisha na shughuli za kiuchimbaji katika
maeneo ya mbali na karibu.
Hivyo
watoto hao wanakosa matunzo ya wazazi wao na kupelekea kuwa wa mitaani na
wengine kujiingiza katika vitendo viovu . Alisema
kwa mtazamo aliokuja nao Mwenyekiti wa Kamati Alex Msama ambaye pia Mkurugenzi wa Msama Promotions wa kusaidia jamii ya Geita anamuunga mkono ili
aweze kuwafikia watu wengi zaidi.
Mbunge
huyo wa CCM, alisema pengine kufanyika kila mwaka kwa tamasha hilo huenda huo
ujumbe utaisaidia jamii kubwa hasa ile ilioingiwa na imani potofu ya kuuwa
walemavu wa ngozi pamoja na vikongwe.
“Tunaomba
kama Msama Promotions wameanza safari hii, basi isiwe mwisho iwe ni mwanzo kwa
nia ya kuendeleza jitihada za kuelimisha jamii kadri tunavyopeleka ujumbe
ndivyo itakavyowafikia wengi ukizingatia mkoa wetu unachangamoto nyingi.” alisema
No comments:
Post a Comment