Sunday, March 13, 2016

DIWANI WA KATA YA VIGWAZA AWAPIGA TAFU WANANCHI WAKE VIFAA VYA KUSAMBAZIA MAJI

DIWANI wa Kata ya Vigwaza wilayani Chalinze, Mohsin Bharwani ameokoa maisha ya wanafuzi wa Shule ya Msingi Kidogozero waliokuwa wakikabiliwa na tatizo la kushambuliwa na mamba. Tayari wanafunzi kadhaa wamepoteza maisha kutokana na kushambuliwa na mamba katika Mto Ruvu, wakati wakichota maji. 

 Kutokana na hilo, diwani huyo alitekeleza ahadi yake ya kuwanunulia wanafunzi hao mashine za kuvuta maji kutoka katika mto huo hadi shuleni.
Diwani wa Kata ya Vigwaza wilayani Chalinze, Mohsin Bharwani (kushoto) akimkabidhi na Mwenyekiti wa Kijiji cha Kidogozero, Ali Mwanga, msaada wa vifaa vya mradi wa maji toka Mto Ruvu vyenye thamani ya sh. milioni 5 ili kusaidia wanafuzi wa Shule ya Msingi Kidogozero ,wilayani Chalinze Mkoa wa Pwani jana. Katikati Mwalimu Mkuu wa shule hiyo. Hilda Ngakuka.
Diwani wa Kata ya Vigwaza wilayani Chalinze, Mohsin Bharwani (katikati) na Mwenyekiti wa Kijiji cha Kidogozero, Ali Mwanga (kushoto) na Mtendaji wa Kata hiyo, Masukuzi Masukuzi, wakisikiliza maoni ya wananchi baada ya kukabidhi msaada wa vifaa mradi maji toka Mto Ruvu vyenye thamani ya sh. milioni 5 kwa ajili ya kusaidia wanafuzi wa Shule ya Msingi Kidogozero iliyopo wilayani Chalinze Mkoa wa Pwani jana.
Diwani wa Kata ya Vigwaza wilayani Chalinze, Mohsin Bharwani, akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kwazoka, wilayani Chalinze Mkoa wa Pwani jana alipowatembelea kusikiliza kero zao.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Kidogozero, Ali Mwanga, akimshukuru Diwani wa Kata ya Vigwaza wilayani Chalinze, Mohsin Bharwani (kushoto) baada ya kuwakabidhi vifaa hivyo jana.
Diwani wa Kata ya Vigwaza wilayani Chalinze, Mohsin Bharwani (kushoto),akikagua mtaro utakaopitisha bomba la maji toka mto Ruvu hadi Shule ya Msingi Kidogozero, baada y kukabidhi vifaa vya mradi huo vyenye thamani ya Sh. milioni tano jana

No comments: