Wednesday, February 24, 2016

AIRTEL MONEY YAINGIA UBIA NA TOTAL KUWEZESHA WATEJA KUFANYA MALIPO KWA USALAMA ZAIDI


Mkurugenzi wa huduma ya Airtel Money Bw, Aijaz khan wakipongezana na Mkurugenzi wa Biashara wa Total Bw, Romee De Villeneve mara baada ya kuingia ubia na kuzindua Rasmi kadi maalum ya Airtel Money Tap Tap kwaajili ya kufanyia malipo ya bidhaa mbalimbali katika vituo vya TOTAL. anaeshudia kulia ni Meneja wa Biashara Total Bi Maria Lebby. Airtel imezindua kadi hiyo jana ili kupunguza wimbi la wateja na watumiaji wa Airtel Money kutembea na pesa taslim kwaajili ya usalama wao pia kuwawezesha kufanya malipo hata kama simu zimezima.

Mkurugenzi wa huduma ya Airtel Money Bw, Aijaz khan wakionyesha kadi na kifaa cha malipo cha Tap Tap na Mkurugenzi wa Biashara wa Total Bw, Romee De Villeneve mara baada ya kuingia ubia na kuzindua Rasmi kadi maalum ya Airtel Money Tap Tap kwaajili ya kufanyia malipo ya bidhaa mbalimbali katika vituo vya TOTAL. alieshikilia kifaa cha malipo cha Airtel Tap tap kulia ni Meneja wa Biashara Total Bi Maria Lebby. Airtel imezindua kadi hiyo jana ili kupunguza wimbi la wateja na watumiaji wa Airtel Money kutembea na pesa taslim kwaajili ya usalama wao pia kuwawezesha kufanya malipo hata kama simu zimezima. 
Mmoja wa watangaziji mahiri wa kituo cha EFM redio Gadner G Habash akitumia kadi ya kwanza kutolewa mara baada ya Airtel na Total kuingia ubia na kuzindua Rasmi kadi maalum ya Airtel Money Tap Tap kwaajili ya kufanyia malipo ya bidhaa mbalimbali katika vituo vya TOTAL. anaemuhudumia mtoa huduma wa Total Bi Saumu Othmani (kati) na Meneja wa Airtel Money Bw, Asupya Nalingigwa. Airtel imezindua kadi hiyo jana ili kupunguza wimbi la wateja na watumiaji wa Airtel Money kutembea na pesa taslim kwaajili ya usalama wao pia kuwawezesha kufanya malipo hata kama simu zimezima.


Kampuni ya simu za mkononi ya imeingia ubia wa kibiashara na kampuni ya kimataifa nchini ya TOTAL inayojihusisha na kuuza mafuta ya magari pamoja na bidhaa za vilainisha ingini na mitambo, Ushirika huo wa Airtel wa Total ni kupitia huduma ya kifedha ya Airtel Money wenye lengo la kuwawezesha wateja wao kutumia kadi ya kugusisha ijulikanayo kama ‘AIRTEL MONEY TAP TAP’ kufanyia malipo yabidhaa katika vituo vyote vya Total .

Kadi ya Airtel Money ya Tap tap imeunganishwa moja kwa moja na akaunti ya Airtel money ya mteja ili mteja aweze kuitumia mahali popote anaponunua bidhaa yoyote katika vituo vya Total nchini. Kutokana na ushirika huo wateja wote wa Airtel na Total watafurahia kupata huduma zote kwa usalama zaidi bila kulazimika kubeba pesa taslimu.

Huduma hii ya kadi ya malipo kwa kugusisha ya Airtel Money Tap tap imetokana na ugunduzi wa utafiti wenye dhamira ya kuendelea kutumia teknolojia za kisasa ili kuwezesha wateja kufanya malipo kwa urahisi na usalama zaidi. Mteja atagusisha kadi tu kwenye kifaa maalumu cha kufanyia malipo na kulipa papo hapo baada tu ya kuingiza namba yake ya siri ya Airtel Money, teknolojia hiyo inajulikana kwa lugha ya kiingereza kama (Near Field Communication).

Akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo Meneja wa Huduma ya Airtel Money Tap tap hiyo Bw, Stephen Kimea alisema “tunajisikia fahari sana leo kuingia ubia na Total ili kuwaweze wateja wetu kufaidi kutumia huduma ya Airtel Money Tap tap. Hii ni huduma yakwanza kutolewa nchini Tanzania na Airtel ili kuboresha usalama zaidi kwa wateja pale wanapofanya malipo ya huduma na bidhaa mbalimbali. Kila kwenye kituo cha Total wateja wetu wataweza kutumia kadi hii, lengo letu ni kufanya wateja wetu wafurahie huduma zetu zaidi”.

Kimea aliendelea kueleza “Airtel tutahakikisha kuwa huduma hii ya kufanya malipo kwa kutumia kadi ya Airtel Tap tap inapatikana kwa wafanyabiashara na watoa huduma wakubwa na wakati zaidi ya elfu 25 nchini, hii nikutaka kutoa suluhisho la usalama wa raia kwa kuondokana na tatizo la kubeba pesa nyingi wanapokwenda kufanya manunuzi na badala yake sasa watatumia kadi hii” 

“sasa kadi hizi zitapatikana katika vituo vyote vya mafuta vya Total na katika baadhi maduka yaliyo na nembo ya Airtel Tap Tap hapa nchini, tunaamini huu ni mwendelezo wa kuboresha mfumo wa uhakika wa malipo kwa teknolojia inayoendana na sasa” alimaliza kwa kusema Kimea.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Biashara wa Total Nchini, Romee DE VILLENEUVE alisema “Total tunazaidi ya vituo vya mafuta 30 nchini, hivyo basi tunawahakikishia wateja wetu wote kupata huduma ya uhakika kila watakapotembelea vituo vyetu vyote na kununua mafuta au kupata huduma yoyote kwa kutumia kadi hizi za Airtel Money Tap tap. Tumeona umuhimu kuboresha mfumo wetu wa malipo kwaajili ya kuwapa wateja urahisi na usalama zaidi katika vituo vyetu, Tunaishukuru sana Airtel kwa kutuletea teknolojia hii ya kisasa ya mfumo kufanya malipo kwa kadi yaAirtel Money Tap tap”.

Huduma ya Airtel Money Tap tap imeanza kutumika kwanza jijini Dar es salaam kwa sasa na baadae itasambazwa nchi nzima katika vituo vyote vya Total

No comments: