Friday, January 1, 2016

SIMU TV: HABARI KUTOKA VITUO VYA TELEVISHENI

Mkazi mmoja wa Mkoa wa Kilimanjaro afariki dunia wakati akijaribu kujiunganishia umeme kinyemela bila ya kuwapo mafundi wa TANESCO.https://youtu.be/Vsq6kS8vHeI

Aliyekuwa mgombea wa Urais kwa tiketi ya Ukawa Edward Lowassa azitahadharisha mamlaka mbalimbali kuacha kuwaandama wafanyabiashara waliokuwa wanaunga mkono vyama vya upinzani katika uchaguzi mkuu mwaka jana. https://youtu.be/CYU9JjQsHfA

Familia 54 ambazo nyumba zao zilibomolewa na mvua kubwa mkoani Mtwara waiomba serikali na wadau mbalimbali kuwasaidia mahema na mabati yatakayo wasaidia kuondokana na athari za mvua zinazoendelea.https://youtu.be/b5LpsTuphec

Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam lazuia kufungwa kwa ndoa eneo la Mbagala baada ya bi harusi kudaiwa kuwa ni mwanafunzi.https://youtu.be/i0TYF6mLXWw

Rais John Magufuli akifuatana na mkewe wamtembelea na kumjulia hali askofu mkuu wa kanisa katoliki nchini Kardinali Pengo.https://youtu.be/Mamzay9YOgg

Ofisi ya mkuu wa wilaya ya Kilosa yalalamikiwa kwa kushindwa kuchukua hatua ya kutatua mgogoro wa ardhi kati ya wakulima na wafugaji wilayani humo.https://youtu.be/P1zC73dN7pg

Chama cha madereva wa Malori chapinga maadhimio yalitolewa juu ya maafikiano kati ya madereva na waajiri kufuatia kasoro kadhaa ikiwemo kutokushirikishwa. https://youtu.be/wp2dIoPGXgM

Baadhi ya wananchi mkoani Tabora walaani vikali kukithiri kwa vitendo vya mauaji ya raia wasio kuwa na hatia. https://youtu.be/dLL3LdikXC8

Kampuni ya uchimbaji wa dhahabu mkoani Geita GGM yaingia lawamani baada ya wananchi kudai baruti zinazolipuliwa na kampuni hiyo huathiri nyumba zao.https://youtu.be/N7e-rEGI2oc

Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam limesema hali ya usalama barabarani imekuwa shwari kipindi hiki cha mkesha wa mwaka mpya ukilinganisha na miaka iliyopita. https://youtu.be/lS5YBwkD7CM

Hatma ya mazugumzo yanayoendelea visiwani Zanzibar yaelezwa kuendelea kuwa siri licha ya wananchi visiwani humo kuwa na shauku ya kujua kinachoendelea. https://youtu.be/uFdktc1QbeM

Mchambuzi wa masuala ya kisiasa kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam atoa tathimini yake juu ya kiapo cha makatibu wakuu na manaibu katibu wakuu.https://youtu.be/zBSCSTCQR4o

Rais John Magufuli ameendesha zoezi la kuwaapisha  makatibu na manaibu katibu wakuu hii leo  Ikulu jijini Dar es Salaam; https://youtu.be/3pqStiOMhPY

Serikali imeagiza maafisa wa nishati na madini kusuluhisha mgogoro wa umiliki wa machimbo ya dhahabu katika kijiji cha Ishokelahela mkoani Mwanza;https://youtu.be/yL2xDjFuqfo

Watanzania wameshauriwa kuisadia serikali katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo ili kuiwezesha kufikia maendeleo iliyokusudia;https://youtu.be/_7hY9lYoP48

Wakazi wa Babati mkoani Manyara wameupokea mwaka mpya kwa kuwaombea viongozi wakuu wa nchi akiwemo Rais John Magufuli;https://youtu.be/vlJuNWR71aQ

Baadhi ya wakazi wa mkoa Kigoma wakiwemo viongozi wa dini waipongeza Tanzania kwa kudumisha amani na utulivu. https://youtu.be/GJq5DcCGilg

Timu ya Simba ya jijini Dar es Salaam yauanza mwaka mpya kwa kuwapa furaha mashabiki wake mara baada ya kuinyoa timu ya Ndanda ya Mtwara kwa ushindi wa goli 1-0; https://youtu.be/Ul2lCDXp7Pk

Serikali imeombwa kuongeza bajeti katika sekta ya michezo ili kusaidia maendeleo ya michezo hapa nchini; https://youtu.be/8MsNW1nnxb0

Rais Magufuli amemtembelea na kumjulia hali Askofu mkuu wa jimbo kuu la kanisa la katoriki Dar es Salaam Kardinali Pengo aliyelazwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili; https://youtu.be/Nr3XkZAh_Z0

Wakazi wa jijini Mwanza wamelipongeza jeshi la polisi jijini humo kwa kuimarisha hali ya amani katika usiku wa mkesha wa kuamkia mwaka mpya;https://youtu.be/pzPIqM02ZdE

Watu watano wamefariki katika matukio mawili tofauti wakiwemo watoto wawili wa familia moja mkoani Tabora; https://youtu.be/Knns7k0iSk8
Soko la hisa la Dare s salaam DSE limesema limepata faida mara mbili ya mauzo ya mwaka 2014; https://youtu.be/guDkiuRUgag

Kocha mkuu wa klabu ya Geita Gold, Suleimani Matola amekiri kuwepo kwa ushindani mkubwa katika ligi daraja la kwanza; https://youtu.be/_roTUi1t35M

Kocha Louis Van Gaal amesema hawezi kufanya miujiza kubadilisha hali ya mambo ndani ya klabu ya Manchester United; https://youtu.be/BYHhPYp5J20

No comments: