Thursday, January 14, 2016

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

Aliyekuwa mgombea wa uraisi wa Chadema Edward Lowassa aahidi kuwa bado atagombea uraisi mwaka 2020 na ashaanza mipango hiyo.https://youtu.be/HD9O9XBrVSk   

Chama cha wananchi CUF, kupita jumuiya wa vijana wa chama hicho wasisitiza kutotambua uamuzi wa kurudiwa kwa uchaguzi uliofutwa visiwani Zanzibar.https://youtu.be/gmlWHcT-8iw

 Jumuiya ya Afrika Mashariki hii leo yatakiwa kuiwekea vikwazo Burundi ikiwa ni pamoja na kuisimamisha uanachama nchi hiyo ili kuishinikiza kushiriki katika meza ya mazungumzo. https://youtu.be/rmrJfbDXCA4
  
Kesi ya maombi ya kuzuia zoezi la bomoa bomoa dhidi ya serikali jijini Dar es salaam yaendelea kusikilizwa mahakamani huku pande zote zikitoa maelezo yake. https://youtu.be/_DZFl_BzseY

 Mahakama kuu kanda ya Tabora imetupilia mbali baadhi ya hoja za maombi ya kesi ya uchaguzi wa jimbo la Buyungu iliofunguliwa na Christopher Chiza.https://youtu.be/BFjmrO7NUNk

Naibu waziri wa kilimo, mifugo na uvuvi amuagiza msajili wa vyama vya ushirika nchini kutuma timu ya wachunguzi na wakaguzi ili kuchumguza madai ya wakulima wa tumbaku juu ya ubadhilifu huko Mpanda.https://youtu.be/xWwOrtqqsjU

Waziri wa nishati na madini Prof.Sospeter Muhongo aiagiza Tanesco kanda ya kusini kuangalia uwezekano wa kutumia mito katika kufua umeme ili kuepuka matumizi ya mafuta katika uzalishaji. https://youtu.be/V3joxKblPMw
  
Serikali yawataka wakuu wa shule za msingi wilayani Kilwa kutumia vuzuri fedha za ruzuku ya elimu bure kwa mujibu wa sheria na kanuni za matumizi ya fedha za umma; https://youtu.be/YSqh9vyeNAI
  
Inaelezwa kuwa idadi ya wanafunzi walioripoti kwa ajili ya kujiunga na kidato cha kwanza wilayani Karagwe mkoani Kagera ni chache; https://youtu.be/4-CRY5sFSSY
  
Uongozi wa halmshauri ya Babati wapewa siku 30 kujieleza kutokana na ubadhilifu mkubwa wa fedha za umma wakati wa ujenzi wa maabara kwa shule za sekondari wilayani humo; https://youtu.be/spkORrDAeN4

 Watu wa jamii ya Wahadzabe wanaoishi katika misituni mkoani Singida wameitaka serikali kuharakisha kuwapatia hati miliki ya ardhi yao;https://youtu.be/zLcaD3SSWp4
  
Mkutano wa chama cha wafanyabiashara  wenye viwanda na kilimo TCCIA unatarajiwa kufanyika ijumaa ya wiki hii kwa lengo la kujadili mchango wa sekta binafsi katika kukuza uchumi wa taifa; https://youtu.be/KXCyi08NAHw

Vilabu vya Simba na Yanga vimekabidhiwa vifaa vya michezo kutoka kwa mdhamini wao kampuni ya vinywaji ya bia ya Kilimanjaro;https://youtu.be/zqAoZdtw1Aw

Serikali yaahidi kupeleka miundombinu ya maji, barabara na umeme katika kijiji cha wasanii kilichopo Mkuranga mkoani Pwani; https://youtu.be/UkAI-YUt5jQ

Mtoto mmoja wa jijini Mwanza asadikiwa kufa maji kutokana na mvua kubwa iliyonyesha jijini humo hii leo; https://youtu.be/tJ0qgBbxVBA

Jopo la wanasheria kutoka nchi mbalimbali za Afrika wamesema zinahitajika hatua za haraka katika kutatua mgogoro wa kisiasa nchini Burundi;https://youtu.be/Qa6lLWJHYLU

 Waziri mkuu Kassim Majaliwa amewataka wawekezaji wa ndani kushirikiana na wawekezaji  kutoka nje ili kuongeza utaalam na ubunifu;https://youtu.be/oyDA8fQ1qvY

Fahamu kuhusu makazi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza kutokana na tuhuma zilizoenea kuwa mkuu wa mkoa huo amekuwa akiishi hotelini badala ya nyumba aliyopangiwa; https://youtu.be/ZBAYGgRFhxs

Wafanyabiashara wa madini mkoani Geita wameiomba serikali kuwasaidia kupata soko la uhakika la dhahabu; https://youtu.be/JlYQOPDbNIc

Timu ya URA ya nchini Uganda yalalamikia suala la waamuzi kutoka Tanzania kutokuwa makini  wakati wa kutoa maamuzi yao;https://youtu.be/PBEN8DjtZhQ

Kocha wa klabu ya Liverpool, Jurgen Klopp amtetea golikipa wake Simon Mignolet kwa kushindwa kutulia langoni wakati wa mchezo wao dhidi ya Arsenal uliomalizika kwa kutoa sare ya goli 3 kwa 3;https://youtu.be/jMh8n6tWf2M

No comments: