Sunday, January 10, 2016

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

Mtu mmoja amefariki dunia na wengine wanne kujeruhiwa katika ajali ya basi iliyotokea mkoani Singida; https://youtu.be/BcYg7V9loc0

Kesi inayowakabili waliokuwa madiwani wa halmashauri ya wilaya Kahama  ya mwaka 2009 kwa tuhuma za kupokea posho pasipo kuhudhuria kikao yaendelea kushika kasi wilayani humo; https://youtu.be/RF0UhcvJvy0

Mgodi wa dhahabu wa Geita, GGM waridhia kuwapatia wananchi mawe yenye masalia ya dhahabu; https://youtu.be/q2mC8EwkNkY

Serikali yaaanza kutekeleza miradi ya ujenzi ya umma katika maeneo ya  bonde la mto msimbazi jijini Dar es Salaam; https://youtu.be/zRXBwH0K4_I

Chama cha wafanyakazi wa malori Tanzania, CHAWAMATA chapinga punguzo la posho lililofikiwa na kamati ya kudumu ya kusimamia usafiri barabarani;https://youtu.be/ycA-bh4JZtU

Wenyeviti wa vyama vya msingi na ushirika vya tumbaku KACU, wilayani Kahama wameitaka serikali kuongeza makapuni ya ununuzi wa zao la tumbaku ili kuongeza ushindani wa bei; https://youtu.be/zfYTku7yjRE

Washambuliaji Ibrahim Ajibu na Elias Maguli wako mbioni kujiunga na klabu ya Zamalek ya nchini Misiri kwa ajili ya kufanya majaribio;https://youtu.be/ZS6Snx1toEg

Kocha Zinedine Zidane amesema amefurahishwa na ushindi ulioupata klabu yake ya Real Madrid dhidi ya Deportivo la Coruna. https://youtu.be/j_MSBp-O2oU

Serikali yasisitiza kuwa zoezi la bomoabomoa kwa nyumba zilizojengwa ndani na pembezoni mwa mito litafuata sheria; https://youtu.be/Ucss-PcPg3o

Inaelezwa kuwa wananchi wilayani  Ngorongoro mkoani Arusha wameanza uvamizi wa maeneo ya wawekezaji katika mkoa huo;https://youtu.be/aKz1j1lLnvE

Halmashauri ya wilaya ya Kaliua mkoani Tabora imetakiwa kuwapatia wananchi maeneo ya kufanyia biashara; https://youtu.be/_XgTyJdsiMg

Baadhi ya wakulima mkoani Singida waiomba serikali iwatafutie sumu itakayoweza kuwasaidia kuua wadudu wanaoshambulia mimea;https://youtu.be/9RFMSoY0h8o

Wahitimu wa jeshi la kujenga taifa JKT wametakiwa kushiriki katika kuthibiti ubadhilifu wa mali za umma; https://youtu.be/hgIE4oJM_JE

Mwanasoka bora wa Afrika kwa wachezaji wa ndani, Mbwana Samatta amesema bado safari yake ya kutimkia ulaya haijakamilika;https://youtu.be/G_LlQfn7uUE

Timu ya Mtibwa ya mkoani Morogoro imefanikiwa kutinga fainali ya kombe la Mapinduzi kwa kuitandika Simba goli 1-0; https://youtu.be/2nMkiQqi0B8

Waziri wa mazingira asema serikali itawashirikisha na kuwapatia tarifa wananchi waishio mabondeni kuhusu zoezi la bomoa bomoa.http://simu.tv/7myVU2v

Imeelezwa kuwa wanafunzi waliofaulu kwenda kidato cha kwanza na kukosa kupangiwa shule, wataanza masomo ifikapo mwezi wa 3 mwaka huu.https://youtu.be/u0VFTHgKLVw

Zaidi ya familia 491 zilizopoteza makazi kufuatia mvua kubwa iliyonyesha wilayani Tandahimba waiomba serikali na jamiii kuwapatia msaada ili waweze kukarabati makazi yao. https://youtu.be/b6wdCILoSXE

Mgogoro wa matumizi mabaya ya mapato waibuka huko Kiguruwe CCM Temeke jijini Dar es salaam baada ya wanachama kuwatuhumu viongozi wao.https://youtu.be/0KVuqEp5Gmo

Mamlaka ya elimu nchini TEA, yatoa zaidi ya shilingi bilioni 2.3 kwa ajili ya mafunzo kwa walimu wa shule za sekondari ili waweze kuwatambua wananfunzi wenye uwezo mdogo na kuwasaidia ili waweze kufanya vizuri.https://youtu.be/4JjF_7lcR40

Wajasiriamali wadogo wilayani Bariadi mkoani Simiyu walalamikia bomoa bomoa ya vibanda vyao vya kibiashara wilayani humo kwa inawarudisha nyuma kimaendeleo. https://youtu.be/lrVMtg3mwEE

Asasi za kiraia nchini zawataka viongozi wa Zanzibar kutoa mrejesho wa mazungumzo yao katika maadhimisho ya mapinduzi.https://youtu.be/CHWcj9d4mls

Wajawazito wa kijiji cha Namambi walazimika kutembea kwa umbali mrefu kutafuta huduma za afya kufuatia ukosefu wa zahanati kijijini hapo.https://youtu.be/WH12UZIFaHY

Wakazi wamanispaa ya Kigoma ujiji wamuomba Rais Magufuli kuingilia kati kusua sua kwa mradi wa maji katika manispaa hiyo kunakopelekea adha kubwa kwa wananchi. https://youtu.be/CtiDj0-n7Ag

Chama cha ADC kinachopitia katika mgogoro chapata unafuu baada ya bodi ya udhamini kuamua kuchukua chama na kukiendesha yenyewe.https://youtu.be/F_5Cq7eWMIQ

No comments: