Sunday, January 10, 2016

SIMU TV: BODI YA MIKOPO ELIMU YA JUU YATUPIWA LAWAMA

Mkurugenzi wa kitengo cha maafa ofisi ya waziri mkuu auagiza uongozi wa wilaya ya Kilosa kushughulikia kwa haraka upimaji wa viwanja kwa ajili ya waathirika wa mafurko wilayani humo ili kupata suluhisho la kudumu. https://youtu.be/J3xwAqulsQ4

Bodi ya mikopo ya elimu ya juu yaendelea kutupiwa lawama na shirikisho la wanafunzi wa vyuo vikuu nchini TAHLISO kutokana na kutokuweka hadharani vigezo vinavyopaswa kutimizwa na wanafunzi wanaoomba mikopo hiyo.https://youtu.be/TfYEiCZKRS8

Mamlaka ya udhibiti wa mafuta na nishati EWURA yawatoa hofu wananchi juu ya akiba ya mafuta iliyopo nchini. https://youtu.be/uAoP7u1P9lo

Kukithiri kwa uvuvi haramu, gharama za usafirishaji, uuzwaji wa samaki katika masoko ya nje pamoja na ongezeko kubwa la watu katika manispaa ya Musoma kwaelezwa kuwa sababu kubwa za kupungua kwa samamki na kupanda kwa bei ya kitoweo hicho.https://youtu.be/wyo6e3LcF2E

Wananchi mkoani Geita waombwa kuilinda na kuitunza miundombinu ya umeme kufuatia changamoto zilizobainishwa wananchi hao ikiwemo uhujumu wa mradi wa REA. https://youtu.be/Z6Mv8cEH4-g  

Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma yaelezwa kukabiliwa na njaa kali huku wakazi wilayani humo wakielezwa kula wadudu na matunda aina ya zambarau.https://youtu.be/o6iEt3yk80M

Baadhi ya wakazi wa wilaya ya Maswa mkaoni Simiyu waiomba serikali kuwajengea daraja baada ya miundombinu iliyokuwepo awali kusombwa na maji kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha. https://youtu.be/mxE9w-h9HZw

Mkuu wa mkoa wa Kagera awataka wakazi mkoani humo kuacha kutafsiri visivyo mpango wa serikali kutoa elimu bure kwa kuacha kuchangia miradi ya maendeleo.https://youtu.be/zijRMu2GenA

Mkuu wa wilaya ya Sikonge mkoani Tabora awataka wakuu wa shule wilayani humo kutobadili matumizi ya fedha za ruzuku zilizotolewa na serikali kwa ajili ya mpango wa elimu bure wilayani humo. https://youtu.be/JZprbM1EojU  

Nusu fainali ya michuano ya kombe la Mapinduzi yafikia patamu kufuatia timu kongwe nchini Yanga na Simba kushuka dimbani kusaka tiketi ya fainali. https://youtu.be/_ZUyPX_GpS0

No comments: