Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Dr Kamugisha Kazaura (Kushoto) akielezea kuhusu mipango ya kampuni mbele ya Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof Faustine Kamuzora (Katikati) na Naibu Katibu Mkuu Dr Mary Sassabo (Kulia) walipotembelea kampuni hiyo.Baadhi ya maofisa wa TTCL wakiwa katika kikao na Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof Faustine Kamuzora pamoja na Naibu Katibu Mkuu wake, Dk. Mary Sassabo walipotembelea ofisi za TTCL Dar es Salaam.Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof Faustine Kamuzora na Naibu Katibu Mkuu, Dk. Mary Sassabo wakiwa katika kikao na wafanyakazi wa TTCL.Baadhi ya maofisa wa TTCL wakiwa katika kikao na Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof Faustine Kamuzora pamoja na Naibu Katibu Mkuu wake, Dk. Mary Sassabo walipotembelea ofisi za TTCL Dar es Salaam.Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof Faustine Kamuzora na Naibu Katibu Mkuu, Dk. Mary Sassabo wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa TTCL pamoja na baadhi ya maofisa kutoka wizara hiyo.Baadhi ya maofisa wa TTCL wakitoa maelezo kuhusu mambo mbalimbali yanayohusu mawasiliano kwa Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof Faustine Kamuzora na Naibu Katibu Mkuu wake, Dk. Mary Sassabo walipotembelea ofisi za TTCL Dar es Salaam.Ofisa wa TTCL upande wa mtandao, Conrad Katakweba (aliyesimama mbele) akifafanua masuala ya teknolojia mbele ya Katibu Mkuu –Mawasiliano Prof Faustine Kamuzora na Naibu Katibu Mkuu Dr Mary Sassabo walipofanya tembelea kampuni hiyo.Katibu Mkuu –Mawasiliano Prof Faustine Kamuzora (Katikati) na Naibu Katibu Mkuu Dr Mary Sassabo (Kulia), Maafisa wa Wizara hiyo na Maafisa wa TTCL wakitizama mitambo mipya iliyofungwa hivi karibuni.
KATIBU Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Faustine Kamuzora na Naibu Katibu Mkuu wake, Dk. Mary Sassabo wamefanya ziara ya kikazi katika Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kwa lengo la kufahamu na kukagua shughuli za kampuni hiyo. Katika ziara hiyo, Katibu Mkuu na Naibu Katibu, Mkuu wake waliambatana na baadhi ya maofisa kutoka wizara hiyo.
Aidha, walipata fursa ya kupata taarifa mbalimbali kuhusu maendeleo ya Kampuni, mkakati wa mabadiliko ya kibiashara na shughuli mbalimbali za usimamizi na uendeshaji wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano. Vile vile walipata fursa ya kutembelea sehemu ya mitambo ya mawasiliano ya simu na Data, pamoja na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano iliyopo katika jengo la Telephone House, Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment